Dr. Kigwangala NASHUKURU. NASIKITIKA SIKO CONNECTED NA MITANDAO MINGINE ISIPOKUWA WANABIDII.
naamini wote tumepitia muhtasari wa agenda ya Dr Kigwangara. Ninatamani kuwa wagombea wote wawe na vision kama ya Dr. kigwa ili uchaguzi hata ungekuwa influenced na upiizi wa rushwa lakini wenye akili tutaridhishwa na vision. Ukweli humuweka mtu huru.
Ujinga wakuwadanganya watanzania kuwa walipiwe walipiwe unatupumbaza. Ni kweli kuwa watanzania wako tayari kugharimia ustawi wao ili mdari kuna utaratibu usioumiza.
Kama kutakuwa na mfumo unaoinua uchumi wa watu . hakuna mizengwe ya rushwa na upendeleo basi kupishana kwa mapato kutakuwa kwa haki. Kila mtu ataweza anachotaka na atataka anachoweza.
Kuhusu afya mimi ni mpinzani wa sera kya kujenga zahanati kila kijiji. Sera ya kuelimisha watu kujikinga na maradhi kupitia mfumo bora wa kinga unafaa. Tulipokuwa kwa wakimbizi tulikuwa na lengo la mtu kutembelea huduma za afya mara nne kwa mwaka. Kama tunataka zahanati kila kijiji ili watu waendelee kuumwa minyoo, typhoid amoebiasis etc ili mradi kuna pa kwenda kutibiwa? hapana watu wajizuie kuumbwa kwa kujenga tabia ya kuzuia maji. Kuchemsha maji ya kunywa. Kuosha matunda kabla ya kula etc haya yanaweza kujulikana darasani kama ikiwa sehemu ya elimu ya msingi.
Tufanyeje ili watanzania wachague mtu kwa kuangalia vision? Kuna wenye fedha za kukusanya watu na kuwadanganya. wamenunua magazeti radio na TV zote. kuna wenye vision kama hizi. Haziwafikii wapiga kura wakaamua?
Tufanye kazi ya ziada
--------------------------------------------
On Sat, 5/30/15, Dr. Hamisi A. Kigwangalla <hkigwangalla@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] URAIS 2015: Kuhusu Mapinduzi Kwenye Sekta ya Afya!
To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, May 30, 2015, 11:13 AM
URAIS 2015: Kuhusu
Mapinduzi Kwenye Sekta ya Afya!Kama ambavyo
nimekuwa nikibainisha hapa kwamba katika vipaumbele
tutakavyoweka kwenye serikali ya awamu ijayo, cha kwanza
kikiwa kuondoa umaskini na kukuza uchumi kwa malengo ya
kuzalisha ajira za kutosha; cha pili kikiwa kutoa huduma
bora kwa jamii; na cha tatu kudumisha utawala bora, leo
nitachambua kwa ufupi nini kinapaswa kufanywa ili kuboresha
huduma za afya kwa watu wote nchini.Changamoto kubwa
kwa serikali kwenye afya ni upatikanaji wa fedha. Ilivyo
sasa, asilimia 65 ya bajeti yetu kwenye afya inalipwa na
wafadhili, fedha za ndani ni asilimia 35 tu! Hili ni jambo
la aibu. Na halikubaliki. Tumeshindwa kufikia malengo ya
azimio la Abuja kuwa bajeti ya afya kwa nchi zilizoridhia na
kusaini mkataba ule ni kuwa tutenge asilia 15 ya bajeti yetu
kwenye afya. Tumekuwa tukirusha rusha miguu kwenye kati ya
asilimia 8 na 12 tu, na tena kwa msaada mkubwa wa wafadhili.
Hii imesababisha mdororo wa huduma za afya nchini: vituo
kukosa madawa, vifaa tiba na vitendanishi; majengo kuwa
machache; huduma za afya kuwa mbali na wananchi; na
watumishi kwenye sekta hii kukosa motisha ya kazi kutokana
na kulipwa mishahara midogo na kufanya kazi kubwa, ngumu,
katika mazingira mabaya na magumu na kwa masaa ya ziada bila
posho stahiki.Kwenye afya mkakati
ninaopendekeza unapaswa kuwa na mambo makubwa yafuatayo ya
kufanya:1. Kuhakikisha kila
mtanzania anakuwa na bima ya afya ya namna moja ama nyingine
(Universal health insurance coverage).2. Kuanza kuchaji
malipo kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya (tafiti
mbalimbali zimeonesha kuwa watanzania wako tayari kulipia
gharama za afya ili mradi tu ziwe na ubora stahiki - dawa na
vipimo vipatikane, wahudumu wawe na staha na huruma kwa
wateja na zipatikane kwa haraka) - hili litapaswa kwenda
sambamba na kutengeneza mfumo wa ruzuku ambao utawalipia
wazee, mama wajawazito, watoto, na watu wengine wasio na
uwezo (siyo kusema huduma bure, naongelea makundi haya
kukatiwa bima na pesa za ruzuku toka serikalini)3. Kupeleka
madaraka halisi ya umiliki na uendeshaji wa vituo vya
kutolea huduma za afya kwenye mamlaka husika za kiutawala
(fiscal decentralisation). Madaraka ya umiliki na uendeshaji
wa vituo yatakuwa kwa wananchi wa eneo kituo kilipo, na
yatakuwa madaraka kamili.4. Kupeleka kampeni
za kitaifa (kama za chanjo, lishe, uzazi wa mpango n.k.)
kutoka juu sambamba na ruzuku za kutekelezea miradi hiyo.
Pesa hizi za ruzuku zitapelekwa kwenye vituo kwa mfumo wa
ushindani unaotokana na malengo mahsusi yaliyowekwa.5. Kuweka mfumo wa
ushindani ambao utatoa motisha kwa vituo ama maeneo ya
utawala kwa kadri yanavyofikia malengo yaliyowekwa ya kiafya
(pay-for-performance) siyo kupeleka bajeti kutoka juu kwa
mazoea. kwa kuwa vituo vitakuwa chini ya mamlaka hizo,
vikisimamiwa na bodi za afya zenye nguvu ya maamuzi yote
yakiwemo kuajiri na kufukuza, kupanga bajeti na kufuatilia
utendaji wa vituo hivyo, hakuna kituo kitazembea.
Wafanyakazi watawajibishwa na bodi zilizochaguliwa na
wananchi. Maana pia bodi zitawajibishwa na wananchi.6. Serikali kuu
itabaki na majukumu ya kuhakikisha vituo vya afya vinatoa
huduma kwa viwango na ubora unaopaswa kwa kutunga sera,
kutoa miongozo mbalimbali ya huduma, kusajili vituo na
kuvifutia usajili, na kukagua ubora wake.Kwa uchache, haya
ni mapinduzi yanayopaswa kufanyika haraka ili tupate
mabadiliko tunayoyataka kwenye #TanzaniaTuitakayo.
Ukitaka kusoma kwa kina mawazo haya yamo kwenye kitabu
changu, #Kigwanomics.Wakatabahu,
Hamisi
Kigwangalla, MD.
--
"Vision is
the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
+255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org
or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org
or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment