Sunday 18 September 2016

[wanabidii] Baada Ya Miaka Kumi, Hatimaye ' Born Again Pagan' Ajitokeza Hadharani Na Jina Lake Halisi..!


Ndugu zangu,

Mjengwablog inatimiza miaka kumi ifikapo kesho Jumatatu, Septemba 19. 
Mmoja wa wachangiajia wa tangu kuanzishwa kwa Mjengwablog ni mjumbe wangu maarufu kama ' Born Again Pagan'.

Ingawa hivyo, hilo si jina lake kamili. Nami nilitunza ahadi iliyodumu kwa miaka kumi sasa ya kutoliweka hadharani jina lake kamili.
Hatimaye, ' Born Again Pagan' , katika kuadhimisha miaka kumi ya Mjengwablog, amejitokeza hapa ' Kijijini Mjengwablg' na kuliweka hadharani jina lake kamili. Anaitwa Romel Zakaria Mauma. 

Kwangu mimi, Rommel Zakaria Mauma, ni mmoja wa watangazaji walimu kwangu tangu nikiwa na miaka sita. 
Utotoni, kila Jumamosi, nilipenda sana kusikiliza redio Tanzania kipindi cha ' Umoja wa Mataifa wiki Hii'. Kiliendeshwa na Romel Zakaria Mauma na Abdalah Mbamba. Baadae kilifuatia kipindi cha ' Nipe Habari' kilichoendeshwa na Mkurugenzi wa RTD, marehemu David Wakati. Hivi viwili ni kati ya ' Vipindi Shule' nilivyovipena sana na vilivyonijenga kiakili kwenye misingi ya kuelewa ulimwengu ndani na nje ya mipaka yetu.

Kwanini anajiita ' Born Again Pagan'? - Fuatilia simulizi yake mwenyewe uelewe..http://mjengwablog.com/habari-za-kijamii/item/27828-baada-ya-miaka-kumi-hatimaye-born-again-pagan-ajitokeza-hadharani-na-jina-lake-halisi.html#.V97kN_krLIU

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment