Saturday 17 September 2016

[wanabidii] Tulijua kina Lissu watamkumbuka Kikwete, na kwa hakika watamkumbuka Rais Magufuli pia

" NINAMKUMBUKA Kikwete. Ninaposema kwamba ninamkumbuka Kikwete, sikumbuki udhaifu wa serikali yake, namkumbuka yeye. Na tumemsema sana. Tulisema Rais huyu dhaifu na mimi nikamwandika kwenye orodha ya mafisadi.

" Kama kuna legancy (urith, alama ya ya kudumu) aliyoiacha Kikwete katika uongozi wake basi kikubwa ni kuhimiza uwajibikaji wa serikali kwa kutumia bunge, hakujaribu kuwanyima watanzania wasione bunge likiivua nguo serikali. Tulimpa shida kweli kweli lakini hakuthubutu kuliingilia bunge".

"Katika miaka kumi ya Kkikwete joto lilikuwa linapanda kufikia kuchemka, ikifikia hapo, anasema njooni tuzungumze (ikulu). Sasa Rais akisema njooni tuzungumze ukikataa kwenda wewe ndio shida, mbaya"

Maneno hayo ni ya Tundu Lissu, mbunge wa Singida mashariki, mwanasheria mkuu wa chadema na mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni maneno hayo ambayo yalichapwa na gazeti moja la kila siku na kutoa ya moyoni mwake, maneno hayo kwa hakika yametuacha vinywa wazi kwa wengi wetu tunaomfahamu Tundu Lissu amabaye kwa mujibu wa maneno hayo, pengine angetamani Rais huyo na serikali yake wangerejee katika uongozi wa Tanzania ya sasa siku zijazo.

Kwa mbunge anayejua wajibu wake au mwanasiasa anayejua maana ya siasa, bunge na serikali, je; anaweza kujiona ni fahari na sifa kuishughulikia serikali? Kwa maana hiyo kazi ya bunge ni kuishughulikia serikali na si kuishauri serikali?

Na ni kweli kwa kuutumia vibaya uhuru waliopewa na serikali ya awamu ya nne kwa bunge, kina Tundu Lissu waliamua kuishughulikia kweli serikali badala ya kuishauri na matokeo yake tuliyaona. Serikali ilivunjwa, baraza la mawaziri jipya la mawaziri na kuunda lingine kwa mara kadhaa, mchezo huo wa kuishughulikia serikali ukawanogea kina Lissu kuamua kutumia vibaya uhuru huo na kuidhoofisha serikali ya ccm na kuhakikisha kila waziri wasiyemtaka na wanayemuona ni kikwazo kwao wanamshughulikia kwelikweli.

Kwa wanaofuatilia siasa za nchii hii hatutashangaa kwa kina Tundu Lissu, kumkumbuka mapaema hivi Kikwete kama mwenyewe alivyosema walikuwa wakiitwa ikulu wakati wa serikali ya wamu ya tano ya hapo kazi tu inawapuuza haitaki hata kuwaita ikulu kunywa chai na juice amabayo wamezimis sana.

LIssu kaamua kuweka wazi na kutoa kauli hiyo hadharani, lakini ukweli ni kwamba wanasiasa wengi mno kati ya wanasiasa wetu wa kambi ya upinzani hata kwa upande wa ccm, wanaomkumbuka Kikwete daima. Kina Ttundu Lissu wataachaje kumkumbnuka Kikwete katika siasa zao hizi, amabazo leo wanathubutu au kudiriki kumtaja hata Edward Lowassa kwa kutumia neon Muungwana?

Kwamba baada ya kina Freman Mbowe, John Mnyika, Peter Msingwa na Saidi Kubenea na wengine wengi tu ndani ya chadema kumtusi na kumsema vibaya Lowassa, leo wanamtaja kwa kumwita 'muungwana Lowassa' haliyakuwa walimwita fisadi na kutaka afungwe jela na wengine kufikia kusema ingekuwa China angeshanyongwa.

Wamesahau yote waliyomtendea hadi wakamtemesha uwaziri mkuu wake, kwa sababu ya kile walichokivalia njuga bungeni na kuzunguuka nchi nzima wakimwita fisadi mkuu kuhusiana na kashfa ya tata ya Richimond, kashfa ambayo pamoja na mbwembwe zote leo hii wanapomsafisha kwa madodoki lakini haitakaa imtoke pamoja na kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kumwita muungwana Lowassa.

Je jinsi Tundu Lissu walivyomyumbisha Kikwete katika uongozi wake, na kwa jinsi walivyoyumbisha bunge kiasi la kuligeuza kijwe cha mipasho ya 'wahuni' wanastahilitena kupewa kupewa tena fursa na uhuru huo?

Kwa kukumbushana tu, kila mtanzania anafahamu kuwa ili tuendelee, tutoke hapa tulipo kiuchumi tunahitaji, kijamii na kisiasa tunahitaji mambo manne, ambayo ni ardhi, siasa safi, na uongozi bora na wala hatuitaji demokrasia ya vyama vya siasa vinavyotaka kufanya mikutano na maandamano, tena yasiyokuwa na ukomo.

Tanazania ya sasa chini ya utawala wa Rais Magufuli imesheni siasa safi, na uongozi bora. Tangu kuingia madarakani kwa awamu ya tano mambo yote hayo yanakwenda kwa pamoja kwa mwendo wa mchakamchaka. Hakuna urasimu serikalini, hakuna utendaji wa ujanjaujanja wala wa kupiga dili, kuanzia ngazi ya wilaya mkoa hadi taifa.

Watanzania hatutaki kina Tundu Lissu wamcheleweshe Rais Magufuli katika uchumi wa kati na viwanda kwa kufanya mikutano na maandamano yasiyo na tija, Mwisho Rais Magufuli akaze kamba asiruhusu mazungumzo ya kunywa chai na juisi ikulu na hapo ndipo kina Kina Tundu Lissu watakapomkumbuka miaka kumi ijayo Rais Magufuli, legency, (alama ya yake kuu ya kudumu) ibakie uwajibikaji kuwa nidhamu, uwajibikaji kwa kila mtanzania awe mtumishi wa umma, mkulima, mvuvi, mfugaji na mkulima kwa ajili ya maendeleo yake popote alipo.

0 comments:

Post a Comment