Saturday 17 September 2016

Re: [wanabidii] Tumekataa EPA, sasa tutaipata

Moja kati ya mapendekezo ya Souyh south commission ni kuwa nchi maskini zishirikiane kujadili na 'wafadhili' hawa. EAC ikiamua kushkamana inaweza kuja na mapendekezo yake kwa EU ambayo yananufaisha mataifa yetu. EU wakikataa tutabasamu wakati EPA inakufa. Lakini ipo haja ya kufufua ile block ya Non alighnment. Ninaamini hiyo spirit ikichomoza na mataifa yaliyoshikamana wakitaka kuleta SHIDA tunaamua kuwatembelea DPRK. Watashtuka.
Kinume shida. Na shida zaidi wakati ndani kuna wanaoona hao wafadhili ni watu muhimu kwa kila wanachosema.
--------------------------------------------
On Sat, 9/17/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Tumekataa EPA, sasa tutaipata
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, September 17, 2016, 3:55 PM

by Ezekiel
Kamwaga in Makala

KAMA mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi baina ya
nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na zile za Umoja wa Ulaya
(EU)
utaendelea kubaki kama ulivyo sasa, ni wazi kwamba Tanzania
itabaki na
msimamo wake.



Nimezungumza na baadhi ya mawaziri wa serikali ya Rais John
Magufuli na
nadhani msimamo huo utabaki ulivyo hata baada ya kupita kwa
miezi mitatu
kama ambavyo wakuu hao walitangaza wiki iliyopita.



Lakini, hivi kuna nini kibaya kwenye mikataba hiyo ya
kiuchumi ambayo
inafahamika kwa kifupi cha EPA (Economic Partnership
Agreement)?



Kuna mengi lakini nitasema machache tu. Mikataba hiyo
inataka Tanzania
iondoe ushuru wa bidhaa kutoka nje zisizokuwa za kilimo kwa
asilimia 90
na pia ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa za kilimo kutoka
kwao. Hapa
wanataka bidhaa zao zije kushindana na zetu wakati wao
wameendelea zaidi
kimtaji na kiteknolojia.



Nchi wanachama wa EAC watabaki kuwa masoko ya bidhaa za
Ulaya. Wakati
huohuo, kwa utaratibu huo wa bidhaa za kilimo, maana yake ni
kuwa nchi
hizi za Afrika zitabaki kutoa malighafi tu kwa ajili ya
viwanda vya
Ulaya kuzalisha bidhaa.



Kwa utaratibu huu wa EPA, Tanzania ya viwanda haitawezekana
asilani.
Hakuna namna ambayo viwanda vya Afrika vinaweza kushindana
na vile vya
Ulaya. Kuna kipengele pia katika mkataba huo ambacho
kinataka nchi za
Ulaya zipewe upendeleo uleule ambao watapewa wabia wengine
wa kibiashara
wa Afrika kama vile India na China.



Yaani, kwa mfano, kama tukisema India tutawapunguzia ushuru
wa bidhaa
hii kwa kiwango hiki, basi na Ulaya nao wafaidi kwa kiwango
hichohicho.
Cha ajabu, mkataba huo hausemi kwamba na wao wazungu
wakiingia
makubaliano ya namna hiyo na rafiki zao, nasi wa EAC tufaidi
vilevile.
Hakuna !



Ukiniuliza kwanini Kenya, Rwanda na Uganda wanataka kusaini
mikataba
hiyo, jibu langu litakuwa sijui. Lakini, ninachojua ni kitu
kimoja pekee
–kwamba wazungu hawataacha hili lipite hivihivi.



Jijini Dar es Salaam, Rais Yoweri Museveni alizungumza wiki
iliyopita
mbele ya wageni akiomba watu wa EU wasiiadhibu Kenya kwa
kuwa imekubali
kusubiri hiyo miezi mitatu.



Museveni anawajua wazungu. Anajua visasi vyao. Inawezekana
mara moja au
mbili kwenye utawala wake amewahi kukumbana na visanga
vyao.



Kwenye kitabu chake Trade is
War, Profesa Yash Tandon, ameandika
kwamba inawezekana Uganda na Rwanda zimebanwa na wazungu
kwamba
wakikataa kusaini, wanaweza kukosa misaada mbalimbali
mingine ambayo
haihusiani na EPA kama vile silaha na vita dhidi ya
ugaidi.



Tandon, mmoja wa wasomi mashuhuri barani Afrika, ameandika
pia kwamba
biashara ya maua; inayofanywa na matajiri wengi wa Kenya
wakiwamo
wanasiasa, itaathirika endapo viongozi wa EPA wasiposaini.
Kwa
kuishughulikia biashara hiyo, watu wa EU wanafahamu watakuwa
wanafanya
jambo ambalo linawaumiza wakubwa moja kwa moja.



Nchi za Ulaya, na mabeberu katika ujumla wao, hawapendi nchi
masikini
kujiamulia mambo yao. Wanafahamu kwamba Tanzania ikiwa na
uchumi wa
viwanda, itajikwamua kutoka kwenye makucha yao. Wanafahamu
kwamba wao
waliendeleza viwanda vyao kwa kuvilinda. Sisi wanataka
tusivilinde.



Fidel Castro si kiongozi mbaya. Lakini mabeberu hawakupenda
siasa zake
za kutotaka kulamba miguu ya wakubwa. Matokeo yake ni kuwa
nchi yake leo
inachechemea. Hali iko hivyo kwa Venezuela ya Hugo Chavez
na hata
Chile ya Salvador Allende.



Patrice Lumumba alionyesha dalili mapema kwamba atakuwa
mwiba kwa
mabeberu, akapotezwa. Hapa kwetu, mtu kama hayati
Abdulrahman Babu
aliishia kuwekwa rumande na kupewa kazi za kutangatanga tu
bila utulivu.
Mabeberu wasingekubali apewe nafasi ambayo angeonyesha njia
ya kweli ya
maendeleo.



Hatua hii ya Magufuli na serikali yake si hatua ya mchezo.
Endapo
mwishowe atakataa kabisa kusaini mikataba hiyo, afahamu
kwamba
atatangazwa kuwa adui namba moja wa mabeberu.



Habari zake zote zitakuwa mbaya. Ataandikwa kwa aliyoyafanya
na
asiyoyafanya. Atapewa majina ya kila namna na uchumi wetu
utaanza
kufanyiwa hujuma. Na kwa sababu mabeberu ndiyo wameshika
uchumi wa
dunia, safari ya huko tuendako inaweza isiwe rahisi.



Kama ameamua kwa dhati kufuata njia hii, ni muhimu ajiandae
na
yanayokuja. Ingekuwa vema pia kama angeweza kushirikisha
jamii pana ya
Watanzania katika kufahamu kiini na sababu za kuchukua hatua

anazochukua. Hii ni sawa na kusema anatakiwa pia kuwaandaa
watu wake.



Kama serikali ya Magufuli ina nia ya dhati ya kuhakikisha
Tanzania
inajenga viwanda vyake na haibaki kuwa soko la malighafi kwa
ajili ya
viwanda vya mabeberu, ni muhimu ikashikilia msimamo wake wa
kukataa
kusaini EPA kama ilivyo sasa.



Cha msingi, ni kufahamu kwamba mabeberu hawatakaa kimya wala
bwete wakati Tanzania ikichukua uamuzi mkubwa na muhimu kama
huo.



Raia Mwema




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment