Ngoja nijadili hoja hii kwa kifupi. Nakuhakikishia, Mbowe hana muda wa kukasirikia maoni yako. Ameitwa majina mengi tangu 1992. Lakini ukweli unabaki kuwa Mbowe ndiye mwenyekiti pekee wa chama cha siasa ambaye amejenga na kukuza chama chake wakati vingine vinakufa. Kwa vigezo vyote, Chadema ndicho chama pekee kinachokua kwa kasi Tanzania. Watu wengi waliokaa mbali naye hawamjui vema, na wanamdharau kwa sababu za kipropaganda, na kwa kuwa hajikwezi.
Waliokaa naye karibu wanatambua kuwa Mbowe ni kiongozi ambaye amewekeza katika kutengeneza na kutanguliza wanasiasa wenzake. Vipaji vingi unavyoona na kujua katika Chadema vimeibuliwa naye. Kwa asilimia kubwa, Chadema ya 2004 hadi sasa ni zao la ubunifu na uchapakazi wa Mbowe.
Hana makuu.Ni msikivu kupita wanasiasa wote niliowahi kukaa nao, ukimwondoa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ni mbunifu. Ni mwepesi wa kubadilika kulingana na mahitaji ya wakati. Ni mfuatiliaji asiyechoka wa mambo anayotaka. Anajua kujenga hoja kutetea anachoamini. Kwa Tanzania ya sasa na siasa zake, nadiriki kusema kuwa Mbowe is the most influential politician of current politics. Hata siasa zinazofanywa na Magufuli sasa zinaegemea katika mtazamo uliojengwa na Chadema kwa miaka 10 mfululizo. UKAWA unayoiona leo imejengwa kwa kiasi kikubwa katika mgongo wa Mbowe.
Propagandists wa CCM na usalama wa taifa wamefanya kazi kubwa kummaliza Mbowe kisiasa, wameshindwa. Wametumia magazeti yao, hasa HOJA na TAZAMA. Tangu 2004, gazeti la HOJA limempiga Mbowe kila wiki. Limeshindwa kumbomoa. Limpiga Chadema limeshindwa kukivunja. Wametumia mbinu zote walizotumia dhidi ya Augustine Mrema wa NCCR-Mageuzi na Ibrahim Lipumba wa CUF; hazikufua dafu kwa Mbowe.
Hata mwaka jana, Chadema kilipompokea Edward Lowassa, walithubutu kupandikiza sumu dhidi ya Mbowe na Chadema. Haikuwa na makali. Walitumia kila mtu waliyedhani angeweza kusaidia kubomoa Chadema. Hawakufaulu. Walijaribu kukosanisha Chadema, Mbowe na umma; wananchi ndio wakafumuka zaidi kuunga mkono Chadema, Mbowe na Lowassa.
Hata waliomhusisha na ujio wa Lowassa, hawakujua kwamba si Mbowe aliyemshawishi Lowassa kujiunga na Chadema. Lakini baada ya yeye kushawishika kuhusu umuhimu wa Lowassa katika harakati za mabadiliko, alisimama kidete kukamilisha kazi iliyoanzishwa na wenzake kwa ufanisi mkubwa. Na kweli, huwezi kupuuza nguvu ya waliomshawishi Lowassa, au Lowassa mwenyewe au Mbowe katika harakati za kuinua upya upinzani Tanzania.
Itabidi wanaomchukia Mbowe watafute mbinu mpya. Hizi za miaka 12 mfululizo zimeshindikana. Mbowe anakipanga upya chama akishirikiana na viongozi wenzake, wapya na wa zamani. Moto utakaowaka nchi nzima baada ya wiki hii si wa kubeza. Propaganda za mtandaoni zitaendelea. Matusi ya magazetini yataendelea. Lakini hayatakomesha ubunifu na uchapakazi wa Mbowe na timu yake. Nimefanya kazi naye kwa karibu. Najua ninachosema. Sihitaji kuambiwa Mbowe ni nani.
Unataka kumjua Mbowe? Tazama Chadema. Tafakari imepita katika mabonde na milima ipi. Itazame Chadema ya Edwin Mtei na Bob Makani. Ilinganishe na ya Mbowe. Ilinganishe na vyama vingine vya siasa. Utaelewa kwa nini Mbowe anapigwa vita na watawala na wapambe wao. Mbowe ni mti wenye matunda. Atarushiwa mawe tu. Bahati nzuri, hana kawaida ya kujibizana na wanaompinga. Wakati nyie mnahangaika kumtwanga mitandaoni, yeye anachapa kazi.
Ansbert Ngurumo
Mobile +255 767 172 665
Mobile +255 767 172 665
www.freemedia.co.tz
On Thursday, March 10, 2016 6:37 AM, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:
Ukiniuliza Who is Mbowe? Jibu ni rahisi sana. DALALI BORA TANZANIA.
Anisamehe kama atakasirika.
;-)
-- ;-)
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment