Wednesday, 30 March 2016

Re: [wanabidii] KUHUSU MCC KUSITISHA MSAADA WA MCC 2 NA SHUGHULI ZAKE TANZANIA: MTIZAMO

Hata Yuda alionekana wa maana aliposema 'mafuta yote kummwagia Yesu miguu si tungeuza na kuwagawia Maskini'.
Ni kwa sababu Yesu alijua ni mwizi ndiyo maana akamkanusha. Unahitaji kuwaamini wamarekani na ili kuwaamini unahitaji kuwa umesahau matendo yao kuanzia walichowafanya wahindi wekundu.
Lakini ni lazima kujua kuwa kuna muungano ambao sio wamarekani wala ushauri wao unaoulinda. Kama emokrasia haziulindi njia nyingine zitatumika, ikuwa ni pamoja na kufuta chaguzi. zilizoingiliwa
--------------------------------------------
On Thu, 3/31/16, Ezekiel J. Massanja <ezekielmassanja@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] KUHUSU MCC KUSITISHA MSAADA WA MCC 2 NA SHUGHULI ZAKE TANZANIA: MTIZAMO
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, March 31, 2016, 9:05 AM



Mwandishi
ameeleza vizuri kwa mtazamo wake anaoita wa kizalendo.
Lakini naona uzalendo anaouuhubiri ni ubaguzi mkubwa NA
kuwafanya wengine ni wajinga hawajui kitu. Uchaguzi wa
Zanzibar CUF walishinda matokeo yakafutwa NA Jecha peke
yake. Serikali ya Marekani NA wengine wote wanaopenda haki
wamejiweka pembeni na kusema hawawezi kuhusika nao.
Tuwaheshimu kwa hilo NA hawashurutishi kwa sababu hizo pesa
ni za kwao.
Kuliko
kuendelea kutoa maandishi yenye ukakasi, ni afadhali turudi
nyuma pale tulipojikwaa tuanze kutengeneza. Tusiwaendekeze
sana wanaojaribu kutuonesha kitu ambacho hakipo.

Sent from Ezekiel's iPhone
On 30 Mar 2016, at 16:33, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>
wrote:

KUHUSU MCC
KUSITISHA MSAADA WA MCC 2 NA SHUGHULI ZAKE TANZANIA:
MTIZAMO



Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu
Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.



"Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can
import. Democracy
should develop according to that particular country". June
1991 in Rio
De Janeiro, Brazil



"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza
kuagiza. Demokrasia
lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika".
Juni 1991 Rio De
Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)



"No nation has the right to make decisions for another
nation; no people
for another people". From 'A Peaceful New Year'
speech, Tanzania,
January 1968



"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa
lingine; wala
watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka
Mpya, Tanzania,
Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)



Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na
haliwezi kuua
mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani
zinashirikiana kwa
mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la
ushirikiano.
Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna
nyingine ila
kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa
wale ambao
wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na
Ujerumani
Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya
Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar.



Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka
kuingilia
Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda
Nchi Mpya
ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1965 Tulivunja
uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu
wachache
kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence)
kule
Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua
hatua stahiki.



Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru
wa nchi za
Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa
kufahamu ni
kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru
wetu. Napenda
ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa
uhusiano
wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada
wao kwetu,
lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si
Marekani au
Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.



MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila
masharti tena hela
nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa
moja na kupewa
uhuru wa kuamua tuzitumieje. Tanzania ilitakiwa kuainisha
maeneo kisha
wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo
hazikuwa
zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na
miradi ya
maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata
ufadhili. MCC 2
sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi
ya Marekani,
hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.



Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa
kushirikiana na
Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha
kwa
ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na
fedha hizo?
Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada
ya kuweka
fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.




Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa
Power
Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la
Nishati (si
uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee
wanaloweza
kushindana na wachina. Wakasema wataelekeza fedha huko
kuisaidia Afrika
kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda.
Wakaweka
sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta
Binafsi ya
Marekani.



Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama
alitangazia dhamira
ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio
kwamba alipenda
kwenda kutembea Ubungo. Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo
kubwa sana
na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post)
kutaka
kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO.
Zikaainishwa
hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na
kisera na
hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka. Kila bodi
ikikutana
wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela
hizi zikawa
zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na
ule mchoro wa
Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza
mbele ya
punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani
atayafikia
kumbe ndio anaupiga mwendo. Hatimaye wakasema wanasubiri
uchaguzi mkuu
jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya
uchaguzi
wakaibuka na suala la Zanzibar.



Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni
uamuzi wenye
madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio
ilikuwa itekeleze
miradi hiyo. Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu.
Ndio msingi
wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa.
Tumetofautiana na
Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa
maisha ya
diplomasia.



Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu
kuituliza huko
nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao
kama ambavyo
wanapaswa kuuheshimu wetu. Hatimaye baadae tutapatana.
Marekani
inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani.
Marekani
inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC
2.



Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha
na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.



Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi
Marekani
isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa
Egypt iliyo
chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa
Egypt na
Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila
mwaka kwa
yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.



Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake.
Wazalendo wasimame
na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au
Imekosea" na Makuwadi
watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko
wapi?".



Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu
kama Taifa
letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza
kukusanya
mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato
yataongezeka
maradufu kwa vyanzo vile vile.



Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke
aliyetoa tamko ni
MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au
Ikulu ya
Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya
Mitandao
(Cyber crimes Act).



Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka
kitokee nini pale
ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana? Tume ile
ile ya
Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na
kisheria
kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua
nafasi yake.
Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano
mitandaoni badala
ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana
basi
wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar. Mezani
wakashindwa,
mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi
ukaitishwa
Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali
na baraza la
wawakilishi. Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua
Zanzibar lakini
ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa
za maendeleo.
Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?



Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende
mahakamani,
bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke
hoja ya
kuifanyia marekebisho sheria hii. Sasa Marekani (MCC)
inapoweka
shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na
linaloweza
kujadilika, sijaelewa. Mbona sie hatujapiga kelele Yule
jamaa yao Trump
alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa
tena chini
ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).



INDHARI



Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni
ishara ya
ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano
yanayotweza
Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za
maendeleo
(politics of development) na sio kujikita katika katika
siasa za
madaraka (Politics of Power).



Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa
watu wenye
uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni
mnufaikaji
(alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya
Nje ya
Marekani.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment