Kuna maswali mawili mbayo sijui ipi liulizwe:
Nani alikuwa hafaidiki na mradi huu katika awamu ya nne?
Nani alikuwa anafaidika na mradi huu katika awamu ya nne.
majibu ya swali sahihi yatasaidia kwa nini mradi huu ulikuwa unalindwa bila kuathirika badala yake wananchi wakaumia kuubeba mzigo huu kama walivyobeba mizigo mingine ikiwemo ya Capacity charges iliyokuwa ikitozwa TANESCO.
--------------------------------------------
On Wed, 3/30/16, 'lang'itomoni lokomoi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Uhakiki wabaini wafanyakazi hewa 1,680
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, March 30, 2016, 9:24 AM
RAIS
John Magufuli amesema kuwa uhakiki mdogo uliofanywa hivi
karibuni kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa nchini, umebaini
wafanyakazi
hewa 1,680 waliokuwa wakilipwa Sh bilioni 1.8. Amesema ni
matarajio kuwa
uhakiki unaofanywa nchi nzima utaisaidia serikali kubaini
wafanyakazi
hewa wengi zaidi na kunusuru fedha nyingi zaidi za
Watanzania.
Machi
15, mwaka huu wakati akiwaapisha Wakuu wa Mikoa, Rais
Magufuli
alitoa siku 15 kwa viongozi hao kuhakikisha wanajumuisha
wafanyakazi
wote na kuwaondoa watumishi hewa.
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye
Uwanja
wa
Shule ya Sekondari Chato mkoani Geita jana, Rais Magufuli
alitolea mfano wa mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA)
ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17, na kueleza
kuwa mfanyakazi
huyo atafikishwa mahakamani.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Ikulu, Rais Magufuli pia alisema
serikali
yake imejiandaa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa
kupunguza kodi
kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9 kuanzia
bajeti ijayo.
Lakini
alisema kwa wale wanaolipwa mishahara mikubwa, ambayo
inafikia
hadi Sh milioni 40, itapunguzwa na kuweka kima cha juu cha
mshahara
usiozidi Sh milioni 15. Rais Magufuli ambaye amefika
nyumbani kwake
katika Kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato kwa mara ya
kwanza tangu
achaguliwe kuwa Rais, alitoa mwito kwa kila Mtanzania
kuchapa kazi kwa
juhudi ili nchi iondokane na utegemezi wa misaada ya
wafadhili ambayo
huambatana na masharti.
Dk
Magufuli alisema jukumu kubwa lililo mbele ya Watanzania kwa
sasa,
ni kushikamana na kujisimamia katika maendeleo ili kila
mmoja
ahakikishe anaongeza uzalishaji na utendaji kazi mahali pake
pa kazi.
"Kwa
hiyo ni lazima tujisimamie sisi wenyewe, na tukijisimama
sisi
wenyewe kwa kila mmoja kuwajibika mahali alipo, kama ni
mfanyakazi
afanye kazi kwelikweli, kama ni mkulima afanye ukulima wake
kwelikweli,
kama ni mfanyabiashara afanye biashara kwelikweli, kama ni
mfugaji afuge
kwelikweli, kama ni mvuvi avue kwelikweli, Tanzania hii
tutavuka,"
alisema Rais Magufuli.
Aidha,
Rais Magufuli alisema serikali yake imeamua kuchukua hatua
kudhibiti nidhamu serikalini, kwa kuhakikisha inawachukulia
hatua
watumishi wa umma wanaolisababishia taifa upotevu mkubwa wa
fedha, na
ameahidi kuwa hatua hizo maarufu kwa jina la "kutumbua
majipu"
zitaendelea kuchukuliwa hadi tatizo hilo likomeshwe.
Dk
Magufuli pia alikumbusha viongozi wote wakiwemo Wakuu wa
Mikoa,
Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala na Wakurugenzi, kutekeleza
wajibu wao
ipasavyo na ameweka bayana kuwa mahali popote ambapo
hapatakuwa na
ufanisi, kiongozi husika atakuwa amedhihirisha kuwa hatoshi
kuendelea na
wadhifa aliopewa.
Rais
Magufuli aliwapongeza walimu kote nchini kwa kufanya kazi
nzuri
ya kufundisha, licha ya changamoto ya ongezeko kubwa la
wanafunzi
waliojiunga darasa la kwanza mwaka huu, lakini ametaka
wazazi na kamati
za shule kushirikiana na walimu kuwasimamia wanafunzi ili
wafanye vizuri
katika masomo yao.
"Naziomba kamati za shule zote
Tanzania nzima, kama haziwezi
kusimamia
nidhamu ya wanafunzi shuleni, zile kamati za shule
zijiuzulu.
Lakini pia kama wewe ni Mwalimu Mkuu, shule yako kila siku
inatoa
divisheni ziro nyingi kila mwaka, sioni sababu ya wewe
kuendelea kuwa
Mwalimu Mkuu," alisisitiza Dk
Magufuli.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment