Huu ni ujinga! Wakati wewe unajaribu kupotosha hoja ya MCC, msikilize Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Augustine Mahiga anavyosema:
"Kitendo hiki ni kibaya. Unamuumiza mtu pale panapouma katika suala la maendeleo. Kitendo hicho kinafuta imani na uelewano kati yetu (Marekani na Tanzania) kwa sababu suala la nishati ni nyenzo ya maendeleo. Fedha hizo zingesaidia miradi ya umeme vijijini, kwa hiyo, watoto wetu wangesoma, wangepata elimu bora na zingeboresha huduma za afya. Walitutamanisha kuwa watatupa hizo fedha, lakini lakini wanafuta pale ambapo maendeleo yetu yamejikita.
SWALI: Unataka kusema kwamba Balozi Mahiga ni mwana UKAWA? Ametumwa na UKAWA kusema hayo? Kama hujajipanga vema, acha propaganda. Zitakuaibisha. UKAWA hawalili misaada ya nje. Wanasisitiza kuwa jeuri ya watawala ndiyo imesababisha hayo. Rais Magufuli alisema ya Zanzibar hayamhusu. Ona sasa kinachotokea. Kinaathiri Tanzania nzima. Tulipiga kelele dhidi ya Sheria ya Makosa ya Mtandaoni kwamba ni ya kikatili, ni dhalimu, ni ya kikoloni. Watawala wakafunika nyuso zao kwa viganja kama nyani. Wakaficha vichwa mchangani kama mbuni,, kumbe mwili mzima upo nje nje. Fedha hizi zilikuwa zinaelekezwa katika kuboresha huduma kwa wanyonge. Atahri zitawapata wanyonge, si Magufuli na wenzake.
Ansbert Ngurumo
Managing Editor
Managing Editor
Free Media
P.O. Box 15261
P.O. Box 15261
Dar es Salaam
Tanzania
Mobile +255 767 172 665
Tanzania
Mobile +255 767 172 665
www.freemedia.co.tz
On Wednesday, March 30, 2016 10:35 AM, 'lang'itomoni lokomoi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Magufuli na wanyonge vs UKAWA na wahisani
Hatimaye UKAWA wamejipambanua katika rangi yao halisi ya kutaka kuuza uhuru kamili wa nchi...kwa kuwalilia na kuwashabikia wazungu!!
Reference iko humu humu jamvini.
Ni ukweli usio na shaka kwamba UKAWA walipambana sana hata kabla ya matokeo ya uchaguzi wa Rais Nov 2015...
Ukawa walipambana vilivyo kuwaonesha wazungu kuwa Tanzania hakuna amani...
Ukawa kwa mara ya kwanza Tanzania walihakikisha kuwa vyombo vya habari vya kimagharibi vinaonesha Tanzania kuna tension kiasi cha amani kutoweka....
Ila kwa weledi mkubwa na uzalendo uliokithiri vyombo vyetu vya kiuongozi na kiusalama vikashinda jaribio hilo ovu la UKAWA na wananchi wa Tanzania wakamaliza uchaguzi kwa amani na ustaarabu kama ikivyo desturi yetu.
UKAWA waliandaa maandamano UK na USA na sio Manzese,Magomeni au Tandahimba ili kuonesha kuwa nchi hii haina demokrasia kisa CCM ilikuwa imeshinda na inaendelea kushinda...huku wakisahau kuwa ndani ya vyama vyao wanacheza tikitaka na kugeuza gia za angani ili tu viongozi wao wawe wa kudumu yaani wanahubiri demokrasia ambayo ndani ya vyama vyao haipo.
UKAWA wako tayari kuomba majeshi nje ili tukupambana na CCM(REFERENCE: Vijana wa IT na mabodyguard kutoka nje ya nchi)
UKAWA inaendelea kujidhihirisha kwa sera zake za utegemezi kwa mataifa ya nje...yaani UKAWA inaachana na dhana ya kutumia resource nyingi tulizonazo kukwamua wananchi kutoka kwenye matatizo na badala yake inajikita kwenye kuamini kuwa maendeleo yatakuja kwa msaada na hisani ya watu wa marekani.
UKAWA inatukumbusha vikundi vya miaka ile ya kudai uhuru ...vikundi tulivyoviita vibaraka wa wakoloni.
HII NI HULKA CHAFU YA UKAWA iliyotubadilishia gia angani!!
UKAWA hii ya sasa ni UKAWA inayonukia kinyesi cha UFISADI PAPA baada ya kukiokota na kujipaka yenyewe karibia na uchaguzi wa 2015.
Hii ni UKAWA iliyopoteza agenda muhimu za kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi,ukosefu wa ajira,ukosefu wa uadilifu,elimu duni na afya isiyoridhisha....UKAWA inahaha kutafuta Agenda ya kubakia kwenye ulingo wa siasa kwa gharama yoyote baada ya kuvurunda ...!
UKAWA inajitenga rasmi na hoja za wananchi na badala yake inachukua mrengo wa kunyenyekea wakoloni!
UKAWA inaanzisha mapambano upya ya sisi wazalendo dhidi ya Ukoloni wa kisasa na kwa nguvu zetu,adabu,uvumilivu na msimamo tutashinda tu...!
UKAWA haisikiki kwebye vita dhidi ya mauaji ya albino lakini inataka isikike kwenye msaada wa MCC...HUU NI UNAFIKI WA KUTUPWA!!
SHAME UPON UKAWA ILIYOAMINIWA NA KUJIGEUZIA GIA ANGANI...!
KWA MAGUFULI HAKIKA MTAISOMA NAMBA....KWANI AGENDA YETU NI KAZI TU KAZI TU KAZI TU!
iliwahi kusemwa kuwa 'NGUO YA KUAZIMA HAISITIRI.....Tufanye kazi na tulipe kodi!
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment