Wednesday 30 March 2016

Re: [wanabidii] Magufuli na wanyonge vs UKAWA na wahisani

Kaka Ansbert Ngurumo,

...Akizungumzia na gazeti hili jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk
Phillip Mpango alisema tangu Desemba mwaka jana walishasoma alama za
nyakati na hivyo kuamua kutozijumuisha fedha za MCC-2 katika
maandalizi ya Bajeti ya Serikali yanayoendelea kwa mwaka ujao wa
fedha.

"Tulisoma kwenye mitandao matamshi ya viongozi wa Mfuko huo ndio maana
tukaamua kutozijumuisha fedha za MCC kwenye bajeti ya mwaka ujao wa
fedha, hivyo Watanzania wasiwe na wasiwasi juu ya kusitishwa kwa
msaada huo," alisema Dk Mpango.

Hata hivyo, alisema Serikali itatoa tamko rasmi baada ya kupata barua
kutoka MCC ikiwaeleza wamesimamisha msaada huo hadi lini na nini
Tanzania inatakiwa kufanya ili kupata msaada huo. "Sisi tukipata hiyo
barua tutaitafakari na tutawajibu," aliongeza waziri. Alisema Serikali
bado inaamini uhusiano wa Tanzania na Marekani ni mzuri na wa muda
mrefu hivyo huko mbele kutakuwepo na maelewano na fedha hizo
zitatolewa.

"Sisi sio nchi ya kwanza kusimamishiwa msaada huo, Malawi waliwahi
kunyimwa lakini baadaye walipewa, na mimi bado naamini tutaelewana
huko mbele ya safari," alibainisha. Dk Mpango pia alitoa mwito kwa
Watanzania kuiunga mkono Serikali inapokusanya maduhuli kutoka vyanzo
visivyo vya kodi na wahakikishe wanalipa kodi inayostahili ili nchi
iondokane na utegemezi wa wahisani.

"Hili liwe fundisho kwetu kwamba nchi itapiga maendeleo kwa kutegemea
vyanzo vya ndani, hatuwezi kuwa tegemezi miaka yote ni lazima ifike
mahali tusimame kwa miguu yetu na tutafanikiwa tu iwapo tutalipa kodi
stahiki," alisema Dk Mpango......

"Tukiwa mbia mkubwa zaidi wa maendeleo kwa Tanzania, Marekani
itaendelea kufanya kazi pamoja na Tanzania katika kuboresha afya na
elimu, kukuza uchumi na kuimarisha usalama," alisema Balozi Childress.
Maoni ya wachumi Mkurugenzi wa Asasi ya Utafiti wa Kupunguza Umaskini
(REPOA), Profesa Samuel Wangwe alisema athari ya msaada wa MCC ni
ndogo kwa uchumi wa nchi kwa kuwa nusu ya fedha hizo zingerudi
Marekani kutokana na mfumo wa masharti hayo.

Alisema dawa ya kujitegemea ni kama ile aliyoitoa Rais John Magufuli
kutumia rasilimali za ndani kuendeshea shughuli za maendeleo badala ya
kutegemea misaada kutoka nje. Profesa Wangwe alihoji kama suala ni
kuminya demokrasia, vitendo ambavyo Marekani imefanya Irak na Libya
ndio kielelezo cha demokrasia?......

......Naye Mtaalamu wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Haji
Semboja alisema Marekani haina rafiki katika nchi maskini na haina
utamaduni wa kuzisaidia nchi maskini isipokuwa inasaidia pale
inapokuwa na ajenda zake na pale inapotokea wanabadili ajenda zao
lazima watoe sababu ya kusitisha msaada.

"Misaada ya kimarekani ni ya kipuuzi na hata watu wenye akili hawawezi
kuupigia bajeti kwa sababu wakati wowote taifa hilo linaweza kutoa
sababu za kipuuzi kukunyima msaada ambao imekuahidi na hiki ndicho
kilichotokea kwani suala la Zanzibar halihusiani na msaada huo,"
alisema Dk Semboja. Alisema kisingizio cha Zanzibar na sheria ya
mitandao kilichotumiwa na Marekani havina maana na hiyo inatokana na
taifa hilo kutokuwa na historia ya kuzisaidia nchi maskini kwa sababu.

Alisema msaada wa MCC ulitokana na urafiki uliokuwepo kati Rais George
Bush na Rais Kikwete na sio kati ya Serikali ya Tanzania na Marekani.
"Serikali haikupaswa kuweka fedha za msaada wa Marekani kwenye bajeti,
wenzetu wa Kenya walishafanya hivyo kwa sababu ya ubabaishaji wa
Marekani, lakini sisi kwa kuwa ni masikini wa akili tunaweka bajeti
kwa kutegemea mfuko wa mtu mwingine na madhara yake ndo haya," alisema
Dk Semboja......


....Naye Mkuu wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk
Ulingeta Mbamba alisema ni kweli kufutwa kwa msaada huo kutakuwa na
athari kwa uchumi ila akaeleza kuwa kama nchi ni lazima ijenge misingi
ya kujitegemea. "Sijalisoma hilo tamko lao, ila najua hizo fedha
ilikuwa ziende kwenye umeme, hili liwe funzo kwetu kwamba msaada sio
suluhu ya maendeleo ya nchi yetu, kujitegemea ni kuzuri zaidi,"
alisema Profesa Mbamba......

Chanzo; [wanabidii] Serikali yaipuuza Marekani, 'lang'itomoni
lokomoi', Tue, Mar 29, 2016 at 11:34 PM

NB; Sijui imetoka gazeti gani.

--
*"Anyone who conducts an argument by appealing to authority is not using
his intelligence; he is just using his memory." Leonardo daa Vinci
*

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment