Thursday, 31 March 2016

[wanabidii] Uchaguzi Marekani ni demekrasia ya kiini macho

Kwa muda takribani miezi kadhaa sasa habari kutoka Marekani zikitawaliwa na kinyang'anyiro cha urais.

Wagombea wanaowania tiketi za vyama wamekuwa wakipambana huku nahuku na mashabiki wao nao wamekuwa wakitiana ngumi na kushikana mashati.

Mgombea mmoja anasema "ukinichafulia mkutano wangu name n'tamwaga mboga" ilimradi watazamaji wengi wamekuwa wakichukulia mchakato mzima kama burudani ya aina yake.

Kinachofanyika kwa sasa ni uchaguzi wa awali (primaries) utakaopelekea kufanyika uchaguzi wa rais Marekani tarehe 8 November 2016. Katiba yao imewka ukomo wa awamu mbili hivyo kupelekea Rais Obama kung'atuka na kumpisha mwingine atakayechaguliwa.

Utaratibu wao wa kuteua wagombea na hata kumchagua Rais ni tofauti na wa hapa kwetu. Kwa kweli sitashanga hata wamarekani wenyewe wasipoelewa.

Wao wanadai wanaongoza kwa demokrasia duniani. Lakini cha ajabu mgombea wao wa urais hateuliwa na wanachama, na rais hachaguliwi na wananchi moja kwa moja kama tunavyofanya sisi hapa kwetu.

Ndio maana wanapofanya uchaguzi ubalozi wao huita waandishi na kuwapa semina juu ya uchaguzi huo na baadaye huwapeleka marekani kushuhudia uchaguzi huo ili wakirudi nyumbani waandika makala motomoto za kuusifu mfumo huo

Huko Marekani wananchi huwachagua watu watakaomchagua rais kwa niaba yao. Watachagua kikundi cha wapiga kura (electoral college) amabao ndiowatakaopiga kura kumchagua rais.

Hivi sasa kinachofanyika ni mchakato wa kuwateua wagombea urais ulioanza tarehe 1february na kumalizika june 14mwaka huu. Uteuzi huo unahusu majimbo yote 50 nchini kote.

Watu watapiga kura kuwachagua wajumbe watakaohudhuria mkutano mkuu wa chama (nominating convention) ambao ndio utamchagua mgombea urais atakayepeperusha bendera ya ya chama.

Kwa mfano, chama cha Republican kitawachagua wajumbe, 2472 watakaohudhuria mkutano mkuu (convention) ambako mhombea wa urais anachaguliwa.

Lakini yote kwa yote kuhusu huu uchaguzi ni kiini macho kwa kuwa hakuna mgombea atakayezeka kushinda bila kukubaliwa na AIPC na hawezi kuupata urais wa Marekani kama atathubutu kuikosoa Israel.

Kuna asasi ya kizayuni inayoitwa AIPAC amabayo ndiyo inayohakikisha kuwa kila rais au mtarajiwa wake anatangaza utii kwa Israel. Ndio maana kabla Obama kuchaguliwa katika muhula wa pili aliiangukia AIPAC. Na ndivyo hivyo hivyo kwa kina Hillary Cliton na kina Trump, watakavyoiangukia AIPAC ili waruhusiwe kugombea urais.
 

0 comments:

Post a Comment