Thursday 15 September 2016

[wanabidii] Pori Letu La Akiba La Selous: Swali Muhimu La Kujiuliza Kama Taifa


Ndugu zangu,

Nimesoma makala yaliyotoka http://mjengwablog.com/…/27763-barua-ya-wazi-kwa-mheshimiwa… magazeti kadhaa makubwa ya hapa nchini kuhusiana na pori letu la akiba la Selous kuwa hatarini kuondolewa kwenye orodha ya UNESCO kama moja ya urithi wa dunia.

Swali muhimu la kujiuliza Kama Taifa kwa sasa..
Je, kipi ni bora, kubaki na pori letu la akiba la Selous ambalo ni uchumi endelevu kwa vizazi na vizazi, au kuruhusu uchimbaji wa madini ya uranium ndani ya hifadhi na kutuingizia mapato kwa muda mfupi huku tukisababishiwa athari za kimazingira zitakazowaathiri viumbe wa nchi kavu na majini kwa muda mrefu?

Ndugu zangu,

Afrika ina mapori yake, lakini, pori kubwa kuliko yote Afrika liko Tanzania. Ni pori la Selous.

Ni ukweli, kuwa nchi yetu imejaliwa kuwa mapori mengi. Pori la akiba la Selous ni moja kati ya mapori mengi hapa nchini. Selous ina ukubwa kilomita za mraba 50.000 ikijumuisha maeneo ya ardhi oevu, misitu ya miombo, nyasi za kuvutia, maziwa na mito ya kuvutia kama Rufiji yenye kutiririsha maji yake bahari ya Hindi.

Ndio, ukubwa wa pori la Selous karibu ni sawa na ukubwa wa nchi za Rwanda na Burundi kwa pamoja. Rwanda (26,338 square kilometres) na Burundi (25,680 square kilometres).

Pori hili linapita katika mikoa ya Ruvuma, Lindi, Morogoro na Pwani. Lilianzishwa rasmi mwaka 1896 na Wajerumani likiwa pori la kwanza barani Afrika kutengwa kwa madhumuni ya kuwalinda wanyamapori. Ni la pili duniani baada ya lile la Marekani la Yellowstone National Park.

Kutokana na umuhimu wa pori hili la Selous, mwaka 1982, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya Utamaduni na Sayansi, UNESCO lililiorodhesha pori la Selous kama moja ya maeneo ya asili ya urithi wa dunia. Hiyo ni heshima kubwa kwa nchi yetu na ni jambo la kujivunia.

Ndugu zangu, 
Swali muhimu linabaki kwetu Watanzania;
Je, kipi ni bora, kubaki na pori letu la akiba la Selous ambalo ni uchumi endelevu kwa vizazi na vizazi, au kuruhusu uchimbaji wa madini ya uranium ndani ya hifadhi na kutuingizia mapato kwa muda mfupi huku tukisababishiwa athari za kimazingira zitakazowaathiri viumbe wa nchi kavu na majini kwa muda mrefu?

Maggid Mjengwa, 
Iringa, 
0754 678 252, 0688 37 36 52

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment