Saturday 17 September 2016

[wanabidii] Michango kwa kuijenga kagera upya.

Wandugu,

Ni faraja kubwa sana kuona Watanzania wenzetu na raia wa nje ya nchi wanavyoshirikiana bega kwa bega kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi la september 10. kwakweli inafariji, inatia moyo ni ishara ya umoja wetu.

Kagera imepigwa, kagera imeharibiwa watu wameathirika kijamii, kiuchumi nk. Nyumba ziko chini,vifo, magonjwa na ulemavu. wanakagera wana hali mbaya sana.

Hili ni pigo la tatu tangu nchi yetu ipate uhuru. ilianza vita ya kagera, ikaja janga la ukimwi, na sasa tetemeko la ardhi. japo kuwa kuna kuzama kwa meli, mafuriko hasa ya elnino na vimbunga/ukame

Kagera ina wakati mgumu sana aisee. inatia huruma kuzungukia maeneo ya mkoa huu. zilipokuwa nyumba ni vifusi, mabati yaliyokuwa yameezeka majumba sasa yamepigiliwa misumari na kuwa ndio makazi yao. hali ni mbaya.

Faraja kubwa ni kwa wanaochangia walichonacho. Shurani kwenu

--
J L Kamala

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment