Thursday 1 September 2016

[wanabidii] DHANA YA UPINZANI NA MCHANGO WAKE KATIKA MAENDELEO NA USALAMA WA TAIFA LETU:

Bahati mbaya sana neno lenyewe ''Upinzani'' halionekani kuwa neno la kistaarabu kama lile la kiingereza linavyoonekana- Opposition.
Lakini dhana yenyewe inalenga kuwapa wanaochagua kuchagua kati ya mambo mawili au zaidi yaliyowekwa mbele yao, na baada ya kuchagua kufurahia au kujutia uchaguzi wao mpaka wakati mwingine wa uchaguzi.
Waingereza hivi karibuni walilazimika kuchagua kati ya kuendelea kubaki umoja wa Ulaya au kujitoa. Mchuano ulikwa mkali. Wazee wakitaka kujitoa na vijana wakitaka kubaki. Wazee wakawapiku vijana kutokana na vijana kutopiga kura. Kwa sasa waingereza wote kwa pamoja wanajadiliana namna ya kujitoa Umoja wa Ulaya. Mtu akijitokeza na kuanza kusema tusijitoe watamshangaa.
Wamarekani mwaka huu wataamua kati ya Sera za Clinton na Trump. Mchuano ni mkali. Matusi yznarushwa bila shida. Kila aina ya jina wanaitana hao ambao kwa kipindi kifupi wataitwa ''mahasimu''. Baada ya uchaguzi hakuna atakayeona ni muujiza kukuta wanasalimiana. Wala magazeti hayawezi kuandika kitu hicho.
Ni kweli kuwa mataifa hayo mawili niliyoyataja hapo juu yanabishania agenda. Baada ya watu kuchagua moja kati ya mawili, wote wanaheshimu na kutumikia maamuzi ya wananchi wao. Lakini wanaheshimu na maamuzi yanayotolewa na kiongozi wao. Kutokana na Marekani kuwa na agenda ndiyo maana miaka miwili iliyopita Rais Mstaafu Bush na Rais Obama walikutana hapa Tanzania na kushiriki shughuli fulani. Yapo mambo ya msingi ambayo pamoja na agenda ya taifa hutegemea kiongozi aliyepo. Kama wamarekani watamchagua Trump, watakuwa wamechagua kujenga ukuta kati yake na Mexico. Wanaweza kuwa hawapendi hilo lakini kwa kuwa anayo mengi wanayoyataka basi wakawa tayari kuvumilia ujenzi wa ukuta huo wasioutaka. Wasiotaka watakaa kimya au watakuwa wananong'ona tu.

Nikirudi kidogo hapa kwetu naona kuna mwanya mkubwa wa kujifunza kwa wenzetu kwa makusudi ya kujenga taifa letu.

Kuna wakati Tanzania iliingia mtafaruku na Rwanda. Rais wetu kwa kuzingatia mazingira inayokumbana nayo wakimbizi wanapojitokeza iliishauri Rwanda kuongea na makundi hasimu. Jambo hili lilikuwa chukizo na mabadilishano ya maneno makali yakatokea. Watanzania wazalendo wote waliungana sambamba na rais wetu, kama ambavyo wanyaRwanda wazalendo waliungana na Rais wao. Nami kama mtanzania, niliungana na rais wangu japo kipindi hicho nilikuwa simfurahii. Cha kushangaza baadhi ya vyama vya upinzani vilijitokeza kupinga. Hii ilifanya tuulize hata sera za nje za vyama hivyo na havikutoa majibu. Lakini katika mijadala ilikuwa wazi kuwa vyama hivyo vinapinga kwa sababu ya kutaka kupinga msimamo wa serikali. Huu nao ni ukosefu wa elimu nami natafuta neno sahihi. Kipindi hicho kulikuwa na mambo mengi ya kupinga na wananchi tulikuwa upande wa vyama hivyo. Ufisadi, ubadhilifu, Ukwepaji kodi, hujuma nyingine kama kuchakachua mawazo ya wananchi mchakato wa katiba; kulitawala na wakati wote wananchi tulikubaliana na mikakati ya kufanya mabadiliko.

Tumeingia uchaguzi mwaka jana na uchaguzi ukafanyika. Kwa kadri upepo ulivyokuwa mabadiliko Tanzania yalikuwa hayaepukiki. Ndicho kilichotokea.
Baada ya uchaguzi inatarajiwa watu na taasisi zote kuungana kutekeleza mabadiliko hayo. Lazima kila mtu/taasisi itashiriki kwa nafasi yake. Haitarajiwi vyama vya upinzani vivumilie makosa hata kama ni madogo, kama isivyotarajiwa watawala kujikosoa hadharani. Haitarajiwi pia taasisi au mtu kupinga kila kitu.


Mambo matatu yamejitokeza:
1) Kama ilivyotarajiwa uongozi mpya umejikita kuyashughulikia matatizo yaliyowakwaza wananchi kwa myaka mingi. Ukusanyaji kodi umeimarishwa; Matumizi yasiyo na tija yamedhibitiwa. Nidhamu ya watumishi imeimarika na inakaribia kurudi. Watumishi wanaoshukiwa wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa mfumo uliopo ambao ulikuwa hautumiki. Kuwahamasisha wananchi kuchangia madawati. Kama kuna jambo lilitia aibu ni Tanzania yenye miti ya mbao kukosa madawati. Yapo yanayofanyika kuandaa misingi ya kufanya mambo muhimu. Mfano huwezi kushirikiana na watu wanaodhaniwa ni wezi au mafisadi kuweka mifumo ya kudhibiti wizi. Lakini kuna yanayofanyika kwa sababu muda wa kuyafanya ulishapita na bila sababu, mfano kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma.

2) La pili lililojitokeza ni wananchi na viongozi wa nchi za nje kuuona uongozi wa Tanzania ni wa kuigwa. Wakati wa uchaguzi wa Uganda kuna wagombea waliojitangaza kama wao ni ''Magufuli'' wa Uganda. Wakenya walimshauri Rais wao kuiga wa Tanzania na kadhalika. Nchi nyingi zilitamka na bado zinatamka matamshi ya kutia moyo watanzania kuwa na matumaini ya kujikomboa kutoka kwenye dimbwi la umaskini.

3) La tatu lililojitokeza ni baaadhi ya vyama vya siasa kubeza na kupinga kila kitu. Pale waliposhindwa kupinga wakakaa kimya. Hii inauumiza upinzani wenyewe kwani machoni pa watu wenye akili wanaonekana (wapinzani) hawaoni kinachoonwa na wengine. Wapinzani wamebeza mpaka juhudi za kuondoa tatizo la madawati na kusema wangeanza kuongeza mishahara ya walimu (japo mishahara haiwezi kulipwa kwa fedha za michango). Wamebeza na kuhamia Dodoma na sijui nini watasema kama serikali itahamia huko.

Matunda ya mambo hayo ni mtafaruku uliojitokeza. Nao ukaja na mambo makubwa haya:
1) Serikali kuamua kuonyesha uwezo wake kuwadhibiti wapinzani. Polisi wamezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa kutumia kpengere cha kuombwa ulinzi wakati wa mikutano. Rais kuzuia mikutano ya uanaharakati hadi kipindi cha kampeni.
2) Vyama vya upinzani vikaamua kutangaza mgogoro na serikali na kutangaza maandamano na mikutano ambayo haiendi kwa sheria. Tuiite civil disobedience. Wanatarajia wananchi wawe upande wao kama ilivyokuwa myaka ile. Kinyume chake ni kifo cha aibu cha vyama hivyo.
3) Serikali ikaamua kuonyesha vyombo vyake inavyovitumia kulinda demokrasia. Polisi wakaonyesha ujuzi wao. Majeshi yakajiandaa kuadhimisha kuanzishwa kwake.
4) Mtafaruku ukaongezeka. Waandamanaji wakapungua. Kwa bahati haitadhihirika. Hiyo itasaidia kila upande kushinda huko tuendako. Bila shaka anayeshinda na anayeshindwa anaanza kutafuta pa kutokea.
5) Bahati nzuri wakzjitokeza viongozi wa Taasisi mbalimbali kutaka 'kusuruhisha'. Serikali ikatoa msimamo wake. Haioni cha kujadili katika usuruhisi. Vyama vikaamua kupumulia hapo. Vimetangaza kusitisha maandamano kupisha usuruhishi. Humu twaweza kupata muafaka. Ingekuwaje bila usuruhishi? Lakini pia itakuwaje katika usuruhishi? La kuwaambia wabunge waliosusia bunge kuwa peleka mashtaka kwa Spika? Hili linasubiriwa wabunge wetu waambiwe na Masheikh na wachungaji. Kuelezwa kuwa matendo yanayotendwa na serikali ya awamu ya tano yanasifiwa na wengi msiyapinge. Ndiyo. Maaskofu watawaeleza.
Ninapenda kumalizia makala kwa kutoa wito. Ni muhimu kuelekeza upinzani wetu kuchangia usalama na maendeleo ya nchi zetu. Labda serikali hii kabla ya kumaliza mhula wake wa pili ihakikishe Tanzania ina agenda. Agenda ambayo vyama vyote vitaitumikia. Kitakachoipinga kiitwe mhaini na kushtakiwa kwa kosa hilo. Vyama vitumike kulinda agenda ya maendeleo na usalama wa Taifa letu. Wanyarwanda waliungana wakati wa mtafaruku na Tanzania, Tanzania tukapingana. Hii iitwe uhaini. Huwezi kuifanta Marekani FBI ikakuacha ukatembea hatua mbili. Tunaona watu wanabeza juhudi za kulikomboa taifa kutoka ufisadi wa namna zote. Hii ifike mahala iitwe uhaini. Hayo yatahitajika kuingizwa kwenye katiba mpya.. Kinyume chake upinzani huu tunaouona unaweza kutupeleka kwingine tusikotaka. Mtu akikataa kuuvumilia unashindwa umzuieje.
Elisa Muhingo
0767 187 507


Sent from my iPad



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment