Nimeyapenda sana maneno ya Tundu Lisu. Nimekumbuka mengi.
Nimekumbuka walivyokuwa wanachachamaa bungeni na wakitoka nje wanakuta wananchi tunawaubiri kuwashangilia. Tuliwashangilia kwa sababu serikali ilitelekeza matatizo ya wananchi na wao wakayabeba.
Nimegundua kitu hapo.
Tundu lisu alifikiri tulikuwa tunawashangilia wao. Aliendelea kuwa tutaendelea kuwashangilia hata kama wakipotoka.
Nimegundua pia mpaka anasema maneno hayo alikuwa hajajua kuwa sasa serikali iliyopo madarakani siyo ile iliyozoea kuwapa cha kushangiliwa.
Hii imewanyima na wao wakaamua kubwatuka na kufikiri tutaendelea kushangilia.
Ninaamini Sasa wamegundua.
Wamegundua kuwa watanzania wanajua wanachofanya. Ukiwakosea uwe serikali uwe chama cha upinzani watakukata. Sasa wataanza kufanya kazi waliyotumwa na wananchi kwa makini
--------------------------------------------
On Sat, 9/17/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Tulijua kina Lissu watamkumbuka Kikwete, na kwa hakika watamkumbuka Rais Magufuli pia
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, September 17, 2016, 6:08 PM
" NINAMKUMBUKA Kikwete. Ninaposema kwamba
ninamkumbuka Kikwete,
sikumbuki udhaifu wa serikali yake, namkumbuka yeye. Na
tumemsema sana.
Tulisema Rais huyu dhaifu na mimi nikamwandika kwenye
orodha ya
mafisadi.
" Kama kuna legancy (urith, alama ya ya kudumu) aliyoiacha
Kikwete
katika uongozi wake basi kikubwa ni kuhimiza uwajibikaji wa
serikali kwa
kutumia bunge, hakujaribu kuwanyima watanzania wasione
bunge likiivua
nguo serikali. Tulimpa shida kweli kweli lakini hakuthubutu
kuliingilia
bunge".
"Katika miaka kumi ya Kkikwete joto lilikuwa linapanda
kufikia kuchemka,
ikifikia hapo, anasema njooni tuzungumze (ikulu). Sasa
Rais akisema
njooni tuzungumze ukikataa kwenda wewe ndio shida,
mbaya"
Maneno hayo ni ya Tundu Lissu, mbunge wa Singida mashariki,
mwanasheria
mkuu wa chadema na mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni maneno
hayo ambayo
yalichapwa na gazeti moja la kila siku na kutoa ya moyoni
mwake, maneno
hayo kwa hakika yametuacha vinywa wazi kwa wengi wetu
tunaomfahamu Tundu
Lissu amabaye kwa mujibu wa maneno hayo, pengine angetamani
Rais huyo
na serikali yake wangerejee katika uongozi wa Tanzania ya
sasa siku
zijazo.
Kwa mbunge anayejua wajibu wake au mwanasiasa anayejua maana
ya siasa,
bunge na serikali, je; anaweza kujiona ni fahari na sifa
kuishughulikia
serikali? Kwa maana hiyo kazi ya bunge ni kuishughulikia
serikali na si
kuishauri serikali?
Na ni kweli kwa kuutumia vibaya uhuru waliopewa na serikali
ya awamu ya
nne kwa bunge, kina Tundu Lissu waliamua kuishughulikia
kweli serikali
badala ya kuishauri na matokeo yake tuliyaona. Serikali
ilivunjwa,
baraza la mawaziri jipya la mawaziri na kuunda lingine kwa
mara kadhaa,
mchezo huo wa kuishughulikia serikali ukawanogea kina Lissu
kuamua
kutumia vibaya uhuru huo na kuidhoofisha serikali ya ccm na
kuhakikisha
kila waziri wasiyemtaka na wanayemuona ni kikwazo kwao
wanamshughulikia
kwelikweli.
Kwa wanaofuatilia siasa za nchii hii hatutashangaa kwa kina
Tundu Lissu,
kumkumbuka mapaema hivi Kikwete kama mwenyewe alivyosema
walikuwa
wakiitwa ikulu wakati wa serikali ya wamu ya tano ya hapo
kazi tu
inawapuuza haitaki hata kuwaita ikulu kunywa chai na juice
amabayo
wamezimis sana.
LIssu kaamua kuweka wazi na kutoa kauli hiyo hadharani,
lakini ukweli ni
kwamba wanasiasa wengi mno kati ya wanasiasa wetu wa kambi
ya upinzani
hata kwa upande wa ccm, wanaomkumbuka Kikwete daima. Kina
Ttundu Lissu
wataachaje kumkumbnuka Kikwete katika siasa zao hizi,
amabazo leo
wanathubutu au kudiriki kumtaja hata Edward Lowassa kwa
kutumia neon
Muungwana?
Kwamba baada ya kina Freman Mbowe, John Mnyika, Peter
Msingwa na Saidi
Kubenea na wengine wengi tu ndani ya chadema kumtusi na
kumsema vibaya
Lowassa, leo wanamtaja kwa kumwita 'muungwana Lowassa'
haliyakuwa
walimwita fisadi na kutaka afungwe jela na wengine kufikia
kusema
ingekuwa China angeshanyongwa.
Wamesahau yote waliyomtendea hadi wakamtemesha uwaziri mkuu
wake, kwa
sababu ya kile walichokivalia njuga bungeni na kuzunguuka
nchi nzima
wakimwita fisadi mkuu kuhusiana na kashfa ya tata ya
Richimond, kashfa
ambayo pamoja na mbwembwe zote leo hii wanapomsafisha kwa
madodoki
lakini haitakaa imtoke pamoja na kumpaka mafuta kwa mgongo
wa chupa kwa
kumwita muungwana Lowassa.
Je jinsi Tundu Lissu walivyomyumbisha Kikwete katika uongozi
wake, na
kwa jinsi walivyoyumbisha bunge kiasi la kuligeuza kijwe cha
mipasho ya
'wahuni' wanastahilitena kupewa kupewa tena fursa na
uhuru huo?
Kwa kukumbushana tu, kila mtanzania anafahamu kuwa ili
tuendelee, tutoke
hapa tulipo kiuchumi tunahitaji, kijamii na kisiasa
tunahitaji mambo
manne, ambayo ni ardhi, siasa safi, na uongozi bora na wala
hatuitaji
demokrasia ya vyama vya siasa vinavyotaka kufanya mikutano
na
maandamano, tena yasiyokuwa na ukomo.
Tanazania ya sasa chini ya utawala wa Rais Magufuli imesheni
siasa safi,
na uongozi bora. Tangu kuingia madarakani kwa awamu ya tano
mambo yote
hayo yanakwenda kwa pamoja kwa mwendo wa mchakamchaka.
Hakuna urasimu
serikalini, hakuna utendaji wa ujanjaujanja wala wa kupiga
dili, kuanzia
ngazi ya wilaya mkoa hadi taifa.
Watanzania hatutaki kina Tundu Lissu wamcheleweshe Rais
Magufuli katika
uchumi wa kati na viwanda kwa kufanya mikutano na maandamano
yasiyo na
tija, Mwisho Rais Magufuli akaze kamba asiruhusu mazungumzo
ya kunywa
chai na juisi ikulu na hapo ndipo kina Kina Tundu Lissu
watakapomkumbuka miaka kumi ijayo Rais Magufuli, legency,
(alama ya yake
kuu ya kudumu) ibakie uwajibikaji kuwa nidhamu,
uwajibikaji kwa kila
mtanzania awe mtumishi wa umma, mkulima, mvuvi, mfugaji na
mkulima kwa
ajili ya maendeleo yake popote alipo.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment