Tuesday 13 September 2016

Re: [wanabidii] CHADEMA wanamaanisha au wanatania?

Huyu Mwanakijiji, haeleweki. Martin Luther, alikuwa na approach yake, Mahatma Ghandhi alikuwa na approach yake, Paulo Frere alikuwa na approach yake pia... Cha maana ni kuendelea kupambana katika kutafuta haki kwa kutumia njia ambayo inaweza kuwa more effective kutokana na mazingira ambayo wanaodai haki wamo. Hata ukiangalia manabii katika kufikisha ujumbe wa Mungu kwa wanadamu walikuwa na approaches tofauti. Mfano, approach ya Musa haikuwa sawa na ya Aaron, Isaiah, Amos, Yeremia, Mical etc. Yet, wote walikuwa na ujumbe mahsusi kwa addressees wao. Sasa anayosema Mwanakijiji ni nini? Kwanza si ni yeye pia aliyekuwa akiwashangaa Chadema kutangaza kufanya mikutano ya hadhara na kuandamana na sasa anawashangaa pia kuahirisha?

2016-09-13 2:15 GMT+03:00 'Lesian' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Mr muganda hawa si waandishi bana ni makanjanja, wanaokwepesha ukweli na kuasi professionalism......makala gani sasa hii
Makanjanja kama haya yanatumika kama anavyotumika mzee lipumba tu, wanakwepa ukweli, wana roho za usali, wanatumika, wanauza hata utu wao kwa vihela kuandika tu kufurahisha waliowatuma,'anyway, makanja wapo na watakuwepo ni kuacha tu kushabikia makala zao fake za kupika bhaaaaaassss

Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:

Endelea kumsoma ninao waandishi makala wa kutosha ninaoweza kutumia muda wangu kuwasoma.
em

2016-09-12 13:41 GMT-04:00 Joseph Ludovick <josephludovick@gmail.com>:

Tangu alipokataa kubadili gia angani. Ila Jana amemkosoa RAIS! Yule yuko objective sana!

On 12 Sep 2016 17:30, "Emmanuel Muganda" <emuganda@gmail.com> wrote:
Nimeacha kumsoma Mwanakijiji muda mrefu sana.
em

2016-09-12 4:15 GMT-04:00 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Na. M. M. Mwanakijiji

SIYO kila utani unachekesha; utani mwingine unaitwa utani mbaya kwani unaweza kumfanya mtu akasirike na wakati mwingine unaweza hata kusababisha ugomvi.

Ninachoogopa ni kuwa ndugu zetu wapinzani inawezekana wanapenda sana utani; tena ule utani mbaya. Kama hawatanii basi inawezekana wanamaanisha wanavyovisema na kama hawavimaanishi basi wanatutania na ni utani ambao haupaswi kuwepo kwani mambo tunayoyazungumzia ni makubwa sana na yana matokeo ya kudumu katika maisha ya mamilioni ya Watanzania.

Tuchukulie kwamba CHADEMA wanamaanisha wanayoyasema. Kwamba, kwa mfano wanamaanisha kabisa kuwa Magufuli ni "dikteta uchwara" na kuwa anasigina Katiba na kuwa anatawala bila kufuata sheria.

Kama madai haya ni ya kweli kabisa basi kuna baadhi ya mambo wasingeweza kuyaachilia hewani hasa kama wanajua wanasimamia walichoamini.

Baada ya kuliweka taifa katika hali ya wasiwasi ya mgongano viongozi wa CHADEMA waliamua kurudi na kuahirisha wakisema kuwa wameombwa na viongozi wa dini na watu wengine 'wazito' kuwa wasifanye maandamano yale ambayo yalikuwa yenye lengo la kuionesha dunia kuwa Magufuli ameleta utawala wa kidikteta.

Hili linanikumbusha jambo ambalo kiongozi wa wapigania haki za weusi wa Marekani Martin Luther King Jr alikutana nalo wakati wa harakati zake mwanzoni mwa miaka ya sitini.

Martin Luther King alikuwa akiongoza maandamano na kukaa chini katika kupinga vitendo mbalimbali vya kibaguzi katika mji wa Birmingham, Jimbo la Alabama.

Mikutano na maandamano hayo ambayo yalikuwa yanafanyika kila mahali yakasababisha mahakama kutoa zuio la maandamano hayo likipiga marufuku mikutano ya kila aina; hata kunyanyua bango kupinga ilizuiwa. King na wenzake waliamua kupuuzia amri hiyo ya mahakama akiamini kuwa kutii amri ovu ni kuendeleza uovu.

Kutokana na kukaidi amri hiyo King na wenzake kadhaa wakaswekwa ndani katika Jela ya Mji wa Birmingham. Akiwa jela, kundi la viongozi wa kidini – hasa weupe – wakimchukulia yeye kama mchungaji mwenzao waliandika barua kali ya kumkosoa mbinu zake na taratibu zake za kuupinga utawala muovu. Jambo hili lilimuuma na kumuudhi King na akaamua kuandika majibu ya hoja za wachungaji hao.

Kama kuna mwanaharakati yeyote ambaye hajawahi kusoma barua hii (unaweza kuipata kwa kuigoogle) nashauri watu wasome kwani ni kiongozi mzuri sana. Katika hili King anasema mojawapo ya mistari maarufu sana kuwa "dhulma mahali popote, ni dhulma mahali pote" (Injustice anywhere, is injustice everywhere).

Akijibu hoja kuwa maandamano waliyokuwa wanafanya kinyume na agizo la sheria ni uvunjaji mkubwa wa sheria King alijenga mojawapo ya hoja nzito sana zilizowasaidia kuwasimamisha wanaharakati wengi baada yake.

Alisema kuwa "naomba kuwakilisha kuwa mtu anayevunja sheria ambayo dhamira yake inamtuma kuamini ni ya kidhulma, na yuko tayari kukabiliana na adhabu ya kosa hilo ili kuamsha dhamira ya jumuiya juu dhulma yake, kiukweli kabisa anaonesha utii mkubwa zaidi wa sheria!"

Sasa ndugu zetu CHADEMA wamesema jambo kubwa sana; jambo lenye matokeo na jambo ambalo walitaka taifa zima liamini kuwa ni kweli – kwamba Tanzania inakabiliwa na udikteta na kuwa nikinukuu maneno yake ya juzi wakati wa kutangaza kuahirishwa kwa maandamano "Na wote tu-mashahidi wa jinsi ambavyo viongozi wa ngazi zote wa CHADEMA na wanachama wa kawaida wamekamatwa, kuteswa na kufunguliwa mashtaka ya uonevu kwa sababu tu ya kutetea au kutekeleza haki na uhuru wao kwa mujibu wa Katiba yetu.

Madai yote aliyoyatoa ni mazito. Sasa kutuambia kuwa wameombwa na viongozi sijui wa dini na watu gani wengine ndio wameona umuhimu wa kuahirisha maandamano ya UKUTA hawajitendei haki wao wenyewe na hawalitendei haki taifa.

Hawajitendei haki kwa sababu sasa hivi sijui ni jambo gani zito wanaloweza kumtuhumu Rais na serikali yake ambalo watu wataona kweli linawauma hasa tukizingatia kauli kali na maonyo ya mikwara ya kila namna kuelekea ile Septemba Mosi. Mara kadhaa walinukuliwa kuwa tarehe ile iko pale pale na hakuna kurudi nyuma.

Hawajalitendea haki taifa kwa sababu baada ya kuahirishwa UKUTA baadhi ya ndugu zetu hawa wameanza kuhoji "gharama" zilizotumika na vyombo vya dola na serikali kudhibiti UKUTA. Kwamba, hata kama maandamano hayakufanyika lakini Serikali imepata hasara na wametumia hela nyingi kwa wanajeshi na nyenzo mbalimbali.

Sasa kama lengo la UKUTA lilikuwa ni kuibebesha serikali na walipa kodi mzigo zaidi wa gharama basi lengo hili limefanikiwa. Lakini kama wanafurahia kuwa mpango wao umesababisha matumizi "makubwa" ya fedha nalo ni jambo la kuhoji kama wanamtakia mema Mtanzania wa kawaida.

Lakini kama wanachosema – na ipo mifano mingine mingi – siyo mambo ambayo wanaamini hasa bali wanachukulia kama utani; kama namna ya kujipatia au kujiongezea ujiko wa kisiasa (political clout) basi wananchi nao watawachukulia kiutani utani na mwisho itakuwa ni kama simulizi la yule mtoto aliyelia "mbwa mwitu" akitania kwa sababu tu hakutaka kuchunga na siku mbwa mwitu wa kweli alipokuja alipoita na kuita hakuna aliyejitokeza. Utani mwingine mbaya.

Lakini kama hii tarehe mpya ya Oktoba Mosi ni ya kweli na wanaamini kabisa kuwa wanamaanisha, nina ushauri mdogo sana lakini utaendana na dhima ya Martin Luther King Jr. Viongozi wa CHADEMA na viongozi wengine wa upinzani ambao wameamua kukabiliana na hicho wanachokiita "udikteta uchwara" basi maandamano yajayo yawe kwanza kabisa ya viongozi wa upinzani nchini.

Watangaze kuwa maanamdano hayo ni ya viongozi. Nina uhakika wakifanya hivyo, hata jeshi la polisi na vyombo vya usalama vitakuwa tayari kuwapa ulinzi viongozi hawa watakapoandamana kutetea kile wanachokiamini. Lakini kama wanatania…

Chanzo Rai
 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment