Ndugu Shoo, Ndugu Kassala,
Ninawashukuruni sana kwa maelezo yenu. Ukweli elimu kama hii inahitajika sana hasa kwa wanaomaliza chuo waweze kupata ufafanuzi kama huo wa kwenu.
Ni elimu ambayo wengi tumeikosa ninaomba muangalie uwezekano wa kuwa na makala kwenye magazeti na hata kwenye vyombo vya habari hasa vya dini muweze kuwafungua macho tulio wengi.
Ninaomba mnisaidie tena kidogo.
Hali ndiyo hiyo kama mnavyoiona na mnavyoelezea mnashauri nini kifanyike kwa mtu mmoja mmoja na kwa vikundi vya kijamii ili tuweze kubadilisha hii hali. Kwa maana kila mmoja anapiga kelele lakini akishafika pale (kwenye madaraka) anabadilika naye anakuwa kama wao anajisahau kuwa yeye alikuwa hakubaliana na mambo yalivyokuwa yanafanyika na anaendelea kuyafanya yale yale yaani ni kama mtu anapiga kelele kwa vile yeye hajapata mwanya wa kutafuna naye.
Vijana wengi wanamaliza vyuo vikuu hawana kazi na wakipata kazi wanataka weweze kuoa, kununua gari na kujenga kwa mwaka mmoja. Jamii ilivyo sasa anayetajirika kwa hali hiyo ndani ya mwaka mmoja anaonekana kuwa ndiyo anayefaa kwenye jamii na anasifiwa na kuwa ndiye msemaji wa jamii anayoishi si kwa vile ana uwezo wa kupambanua mambo ila ni kwa vile anauwezo wa kifedha na ameweza kutumia akili ya kupata utajiri wa haraka.
Waheshimiwa ninawaomba mnisaidie tufanye nini- a) Jamii iweze kuchukia watu wanajipatia fedha bila kutoka jasho
b) Nini kifanyike ili kama mtanzania tuweze kutambua fursa zilizopo ili waweze kujipatia kipato hasa kwa wale wanaomaliza Chuo Kikuu (Kuna kijana amemaliza Chuo Kikuu analipwa shs laki mbili kwa mwezi anafanya kazi kwa wahindi)
Mtanisamehe kwa maana nimechanganya mambo mengi kwa wakati mmoja
Asanteni na nawatakia wiki end njema.
--------------------------------------------
Erasto Ndeuka
Konrad Adenauer Stiftung (KAS)
Accountant
Isimani Street / Upanga
P.O. Box 6992 Dar es Salaam
Tanzania
phone +255 (0) 22 2153174
fax +255 (0) 22 2151990
erasto.ndeuka@kas.de
www.kas.de/tansania
Von: Gideon Shoo <drgshoo@gmail.com>
An: Camillus Kassala <cdnkassala2002@yahoo.co.uk>,
Kopie: Erasto Ndeuka <Erasto.Ndeuka@kas.de>, Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>, Charleskitima <charleskitima@yahoo.com>, Wanahakirasilimali <hakirasilimali@googlegroups.com>, Homotanzanianus <homotanzanianus@gmail.com>, Issa Shivji <issashivji@gmail.com>, John Mnyika <johnmnyika@gmail.com>, Juma Mwapachu <jvmwapachu@gmail.com>, Rodrick Kabangila <kajuna2010@gmail.com>, "Dr. A. Massawe" <massaweantipas@hotmail.com>, Ngowi Prosper <pngowi2002@yahoo.com>, Richard Shaba <richardshaba@hotmail.com>, Shaabani Nzori <snzori777@gmail.com>, Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>, "wanataaluma@googlegroups.com" <wanataaluma@googlegroups.com>, yahoogroups <wanazuoni@yahoogroups.com>
Datum: 11.03.2016 13:42
Betreff: Re: Antwort: Fw: [TPN] Mfugaji wa Ufisadi: MUSH!!!!!
Ndugu Erasto,
salaam.
Pengine swali lako la aina ya uchumi ambao Tanzania inaujenga au inaufuata linatakiwa kuangaliwa kwa macho mawili tofauti au tuseme majibu yanategemea anayetaka kulijibu anasimamia wapi.
Ukiwauliza wanaosimamia uchumi wanakuwa wepesi kuimba nyimbo za Bretton Woods. Kila ukiwauliza hawana majibu yoyote yale ya maana na badala yake wanakimbilia kuimba nyimbo walizofundishwa za kuhalalisha yale ambayo wanayafanya.
1. Tuliondolewa kutoka katika uchumi jamii anaouzungumzia Ndugu Kassala bila ya maandalizi yoyote.
2. Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo ni nguzo ya uchumi jamii ilitelekezwa kimya kimya kwa kuhofia kutokukubalika kwa uchumi wa soko holela/huria. Ukimya huo ni hadi leo.
3. Unyemela huo ndiyo uliosababisha wananchi kutokuandaliwa kwa uwazi kuelewa nini hasa uzuri na ubaya wa uchumi wa soko holela/huria.
4. Unyemela huo ndiyo uliotoa mwanya wa ubinafsishaji/uporaji wa mashirika ya umma pamoja na raslimali ardhi.
5. Unyemela huo ndiyo uliotoa mwanya kwa wachache waliokuwa kwenye madaraka kugeuza siasa kuwa ni kitega uchumi.
6. Ili siasa iwe kitega uchumi ilikuwa ni muhimu sana kuhakikisha kwamba mageuzi ya kiuchumi na kisiasa yanafanyika katika mazingira ya vurugu na ndiyo sababu asasi za usimamizi na uratibu ziliundwa kama wazo au fikra za baade baada ya wachache kupata fursa ya kupora na kujilimbikizia mali kwa njia haramu.
7. Sheria na kanuni za manunuzi ya umma zilitungwa kwa namna ambayo iliwatengenezea mazingira ya ulaji/rushwa kwa waliokuwa madarakani.
8. Uchumi wetu ni mkorogo wa vurugu za soko holela/huria pamoja na masalia ya uchumi jamii yaliyoachwa na siasa ya ujamaa na kujitegemea ambayo wakubwa wanaiogopa kama ukoma.
Ni mawazo yangu tu.
Wakatabahu
Gideon Shoo, Ph.D.
G&S Media Consultants
P.O.Box 32870 Kijitonyama
Kinondoni District
Dar es Salaam
Tanzania
East Africa
+255784222293
2016-03-10 19:06 GMT+03:00 Camillus Kassala <cdnkassala2002@yahoo.co.uk>:
Ndugu Ndeuka,
Kuna wanauchumi wa aina mbili: Kuna wale wanaoangalia takwimu za kiuchumi; na kuna wale wanaoangalia madhara ya uchumi unaoshamiri! Kwa bahati mbaya sayansi ya uchumi inayoshamiri sasa haitaki kupima madhara ya uchumi unaokua kwa binadamu! Tukitengeza mizinga ya vita 100,000 kwa ajili ya kwenda kuua, tutaambiwa pato la taifa limeongezeka, na uchumi umekuwa! Hatujiulizi, kukua kwa pato hilo la taifa kuna mdhara gani kwa binadamu watakaolengwa na hiyo mizinga?
CDNKassala
On Thursday, 10 March 2016, 18:28, Erasto Ndeuka <Erasto.Ndeuka@kas.de> wrote:
Ndugu Kassala,
Ninashukuru kwa elimu yake ya uchumi jamii.
Ni muhimu sana ili tutoke hapa tulipo kuwa na uchumi jamii. Kwa sasa hivi sijui mfumo unaotumika Tanzania ni upi ni Ubepari au Ujamaa na kujitegemea au ni ?. Dr Kassala ninaomba unisaidie hapo kwa sasa unaweka mfumo wetu tulio nao kama upo kwenye kundi lipi?
Mgonjwa anafurahia ugonjwa alionao na anaona kama akienda kwa Dr. nina maana viongozi wetu hawaoni mwelekeo wa nchi kuwa ni mmbaya wanazunguzia uchumi umeongezeka/umekuwa kwa 7% halafu wewe unasema ni mbaya. Kuna kiongozi mmoja wa ngazi ya juu alisema kama watu hawaoni maendeleo yaliyoletwa wanaupofu wa macho:)))))))
Ninakutakia jioni njema.
--------------------------------------------
Erasto Ndeuka
Konrad Adenauer Stiftung (KAS)
Accountant
Isimani Street / Upanga
P.O. Box 6992 Dar es Salaam
Tanzania
phone +255 (0) 22 2153174
fax +255 (0) 22 2151990
erasto.ndeuka@kas.de
www.kas.de/tansania
Von: Camillus Kassala <cdnkassala2002@yahoo.co.uk>
An: yahoogroups <wanazuoni@yahoogroups.com>, Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>, Issa Shivji <issashivji@gmail.com>, Juma Mwapachu <jvmwapachu@gmail.com>, Shaabani Nzori <snzori777@gmail.com>, "Dr. A. Massawe" <massaweantipas@hotmail.com>, "wanataaluma@googlegroups.com" <wanataaluma@googlegroups.com>, Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>, Wanahakirasilimali <hakirasilimali@googlegroups.com>, Ngowi Prosper <pngowi2002@yahoo.com>, Rodrick Kabangila <kajuna2010@gmail.com>, Gideon Shoo <drgshoo@gmail.com>, Homotanzanianus <homotanzanianus@gmail.com>, Charleskitima <charleskitima@yahoo.com>, John Mnyika <johnmnyika@gmail.com>, ":" <erasto.ndeuka@kas.de>, Richard Shaba <richardshaba@hotmail.com>,
Datum: 10.03.2016 18:05
Betreff: Fw: [TPN] Mfugaji wa Ufisadi: MUSH!!!!!
On Thursday, 10 March 2016, 17:57, Camillus Kassala <cdnkassala2002@yahoo.co.uk> wrote:
Ndugu Temu,
Nashukuru kwa kusoma maoni yangu. Kwa kuwa nimetumia msamiati wa kitabibu kwa kuuita ufisadi kuwa ni saratani katika mfumo wa uendeshaji uchumi wetu, nitatumia msamiati wa namna hiyo katika kujibu swali lako.
Kwanza: kama ilivyo kwa kila mgojwa anayetaka kupona, ni yeye mwenyewe huenda kwa daktari na kueleza shida yake ili daktari baada ya kuchunguza (diagnosis) anaweza kupendekeza mgonjwa apewe matibabu (prognosis) na uangalizi wa namna gani. Hivyo, sisi Watanzania kwanza lazima tutambue kuwa mfumo wa uongozi wetu unaumwa, na waliosababisha ugonjwa huu ni sisi wenyewe raia tulioendekeza na kunufaika na 'kuugua' kwa mfumo huu! Hivyo nasi tunawajibika kujitafiti na kuona ni wapi kila mmoja wetu ameshiriki na kunufaika na gonjwa hili la 'ufisadi'. Kama alivyosema Mheshimiwa Rais, wote waionufaika na ufisadi ni majipu, na watatumbuliwa tu! Ingawa njia hii ni ya mkato na ya muda mfupi, itasaidia kupunguza yale majipu ambayo yasipotumbuliwa yanaweza kuendelea kuambukia sehemu nyingine za 'mwili' wa mfumo wa uemdeshaji wa Serikali.
Pili: Kwa kuwa ufisadi ni 'saratani ya kimaadili katika jamii', itabidi jamii yenyewe ikubali kutumia dawa au matibabu ambayo daktari atakayoitoa. Daktari hapa ni wote wale ambao kwa nafasi zao katika jamii wana mamlaka (wazazi, waalimu, maafisa watendaji wa taasisi na mashirika na viongozi wa serikali), wana ushawishi (viongozi wa dini, viongozi wa asasi za kiraia, viongozi wa kisiasa, marafiki, majirani wema), na wana nguvu za kisheria (mahakimu, majaji, vyombo vya dola na vya usalama) ambao - kwanza wana huruma na uchungu na nchi yetu, na pili wako tayari kutoa maisha yao kwa ajili ya kutibu 'saratani' hii - ni waadilifu (na jamii inawatambua hivyo!) na wako tayari na wana ujasiri wa kutumia nafasi zao, mamlaka yao, ushawishi wao na nguvu zao kufundisha, kuonya, kuelimisha, kulaani na hata kuchukua hatua kali za kisheria.
Tatu: kwa kuwa sote Watanzania ni walengwa wa mfumo wa uongozi ambao 'umeoza' kwa sababu ya 'saratani ya ufisadi', tunawajibika pia kujitunza tusiambukizwe na hao wachache ambao wataeneza hiyo saratani ya ufisadi. Njia pekee ya kuweza kufanya hivyo ni kufanya yafuatayo:
1. Kutumia maadili ya jadi zetu, imani zetu na itikadi zetu za kidini kwa mawazo, kwa maneo na kwa matendo kila tunapojikuta ni lazima tufanye maamuzi kuhusu rasilimali, mali, fedha na huduma na kuyaelekeza maamuzi hayo kwa manufaa ya walio wengi.
2. Kujitawala katika matamanio yetu ya kupata zaidi ili tuwe watu wa kutosheka na kile tunachokipata kwa halali.
3. Tuondoe uwoga na tujenge ujasiri wa kupigania kile ni cha haki, halali na chema kwa ajili ya wengi.
4. Tupinge kabisa na kupiga kabisa jitihada zozote za kujitafutia utajiri wa haraka haraka.
5. Tujenge moyo wa ukarimu, huruma, kujali, ujirani mwema na kujitolea kwa ajili ya wanyonge, maskini, wasiokuwa na sauti na wanaoonewa katika haki na maslahi yao ya msingi ya maisha ya binadamu, hasa makazi, malazi, chakula, maji, ajira, elimu, burudani, matibabu, nishati na ajira.
6. Tuweke nia ya dhati ya kuwa wafuasi wa Mwalimu Nyerere katika kupigana na adui huyu ufisadi/rushwa kwa kuiskiliza au kusoma hotuba zake.
7. Tuweke nia ya dhati - na tufanye hivyo - ya kuishi maisha ya kawaida yasiyo na ubinafsi, ukuu, mbwembwe, ulafi, ufahari, kujiona, kutafuta umaarufu na kijicho.
8. Tuipende nchi yetu ya Tanzania na kuwa tayari kufa kwa ajili yake.
Mungu Ibariki Tanzani! Mungu Ibariki Afrika!
CDNKassala
On Thursday, 10 March 2016, 16:09, Apollo TEMU <atemu@calderberg.com> wrote:
Good analysis, good observation...
Sasa Mkuu, SARATANI ina stages and inaua kabisa...huyu mgonjwa wa hii diagnosis ya Saratani apewe treatment gani ili arudi fully healthy and productive member of society katika Soko Jamii linalofaa? Asiachwe afe tuu...ama ? -:)
Regards
---- ---- ----
Apollo TEMU
| Mobile +44 7855 581042 |
| Mobile +255 752 888 050 |
2016-03-08 9:05 GMT+00:00 Camillus Kassala <cdnkassala2002@yahoo.co.uk>:
Ukitaka kufuga rushwa, ufisadi, hongo, milungula, n.k. katika nchi changa za Afrika kama vile Tanzania, weka sera za mfumo wa uchumi wa soko huria (MUSH)! Mfumo wa uchumi wa soko huria haufai kabisa katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania, walau kwa sasa. Hii ni kwa sababu maofisa wengi wa serikali na Watanzania binafsi bado (labda hapo baadaye!) hawajajua mantiki yake kuu ni nini. Mantiki kuu ya Mfumo wa uchumi wa soko huria ni kuwa serikali isidhibiti hata kidogo nguvu za soko ambazo, waumini wa mfumo huo wanavyosema, zitarekebishwa na bei ya maelewano. Kwa bahati mbaya, Watanzania wengi hatuna ufahamu wa kutosha wa 'kudalili' (to bargain) ili tuweze kuuza na kununua bidhaa, huduma na hisa kwa namna ambayo italeta uwiano wa haki pande zote mbili. Siku zote nimekuwa nikijenga hoja kuwa kwa nchi za Afrika mfumo wa uchumi unaofaa ni ule wa 'soko-jamii', ambao unalinda maslahi ya kijamii na vile vile unawatuza wale wanaotumia ubunifu na ujasiria mali katika shughuli za kiuchumi. Mfumo wa namna hii unatilia maanani mambo ambayo hayawezi kuachiwa kwa sekta binafsi na kuwa bidhaa itakayouzwa au kununuliwa bila kujali athari zake, eti alimradi tu mtu katengeneza faida. Mambo hayo ya kijamii ni kama vile mazingira, ardhi na rasilimal zake juu yake na chini yake, maji, chakula, makazi, afya, elimu, kinga ya kijamii, nishati na usafirishaji. Ukiyaachia hayo yakaendeshwa kwa nguvu za soko huria, katika soko ambalo ni ushindani, wasiokuwa na uwezo wa kushindana (kama vile watoto, familia maskini, waajiriwa wa kipato cha chini, wanafunzi na wahitimu wasiokuwa na ajira) wataathirika sana hasa wakati wa majanga kama vile mafuriko, ukame, njaa, magonjwa ya mlipuko, ajali, ukimbizi, uzee bila pensheni inayokidhi, vifo, matetemeko, n.k. Hawa katika mfumo wa soko huria hawatakuwa na uwezo wa kukabiliana na majanga kama hayo! Lakini, mfumo wa uchumi wa soko jamii huhakikisha kuwa serikali iliyowekwa na wanajamii inazingatia maslahi ya kijamii kwanza kuliko maslahi ya watu binafsi ambao kwa sababu wanataka kupata faida kubwa hutumia njia ya kuwahonga wale wenye mamlaka na maamuzi kuhusu bidhaa, huduma na rasilimali za nchi. Na Tanzania yetu sasa naamini inapitia funzo hili! Ni mpaka hapo Rais Magufuli atakapotambua kuwa mfumo wa serikali na uongozi umezingirwa na mfumo wa uchumi wa soko huria uliokithiri mpaka umekuwa holela, ndipo atakapoweza kuubadilisha huo mfumo. Kutumbua majipu ni kuondoa matokeo ya mfumo ambao umekolea kiasi kuwa ume jikita katika 'nyama', 'misuli', 'neva' na 'mifupa' ya mfumo wa mwli wa serikali! Kwa neno moja: umekuwa 'saratani'!
CDNKassala
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanataaluma wa Tanzania" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanataaluma+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanataaluma wa Tanzania" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanataaluma+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment