Saturday, 12 March 2016

RE: [wanabidii] Ngurumo aliyemkataa Lowassa enzi za JK na kumkubali miezi mitatu ya mwisho ya JK.

Mhariri wangu Ansbert Ngurumo.
Nakupongeza kwa dhamira yako njema katika kuitumikia nchi yetu.
Nakutia shime, songa mbele bila woga maana Tanzania itajengwa na watu wenye moyo, wasiokata tamaa, wenye ujasiri na uzalendo usiotiliwa shaka.
Wanafiki--wanaume na wanawake, ndio wamesababisha nchi yetu kuota majipu ya kutisha--ambayo yamesababisha watu wachache kuwa matajiri kufuru kwa wizi wa mali umma huku mamilioni ya Watanzania wakinuka ufukara.
Ninamshukuru Mungu maana angalau tumempata Rais--Rais Dr John Magufuli--Rais makini asiyekumbatia unafiki na wanafiki na anawajuwa wanahabari makini wasiojikomba bali wanaopenda kuona nchi yetu ikiwa na viongozi wenye nia ya dhati kutumikia wananchi bila wizi, siasa za kibaguzi, unafiki na ubinafsi.
Watu wa mfano wa Rais Dr John Magufuli,Ansbert, Nguruma na wengine wengi wenye sifa hizi njema---kujitoa kwa ajili ya nchi yako na watu wake---Mungu yupo upande wao kila uchao.

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Fri, 3/11/16, Neatness Msemo <nmuzeh@gmail.com> wrote:

Subject: RE: [wanabidii] Ngurumo aliyemkataa Lowassa enzi za JK na kumkubali miezi mitatu ya mwisho ya JK.
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, March 11, 2016, 8:44 PM

Umenifurahisha kaka yangu kwani kama
wajapan,wachina,waswedish ,wajerumani .nk wanaongea na
wakalimani wapo tuenzi lugha yetu wao wajifunze kiswahili
mbona tukienda kwao wanataka tuongee kikwao bigup
JPM.kiingereza sio lugha ya kwetu sio vibaya kuijua lakini
kila mvamba ngoma avutie kwake
On Mar 10, 2016 10:20 PM,
"Edgar Mbegu" <embegu@hotmail.com>
wrote:




Na kwa kweli siyo Rais
tu. Hata viongozi wetu wengine wakuu waongee Kiswahili
halafu watumie wakalimani. Huu ni uzalendo na ni kuheshimu
lugha yetu ya Taifa!
From: embegu@hotmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: RE: [wanabidii] Ngurumo aliyemkataa
Lowassa enzi za JK na kumkubali miezi mitatu ya mwisho ya
JK.
Date: Thu, 10 Mar 2016 19:14:19 +0000





Safi. Ni vizuri Rais wetu
akatumia Kiswahili.
Date: Thu, 10
Mar 2016 11:10:01 -0500
Subject: Re:
[wanabidii] Ngurumo aliyemkataa Lowassa enzi za JK na
kumkubali miezi mitatu ya mwisho ya JK.
From: emuganda@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Excellent!em
2016-03-10 10:08 GMT-05:00 'Ansbert
Ngurumo' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:


Nimekusoma ndugu
yangu. Kuna mambo 10 nataka niyaweke sawa, maana
umeyakosea.


1. Makala ya
Maswali Magumu haikuanza na Rais Jakaya
Kikwete. Ilianza na Rais Benjamin Mkapa mwaka 2002 katika
gazeti la Mwananchi
Wiki Hii.


2. Makala zangu
za
uchambuzi wa kukosoa serikali hazikuanza na utawala wa Rais
Kikwete. Nilizianzia
The African na baadaye Rai na Mtanzania
katika Habari Corporation ya Jenerali Ulimwengu, Salva
Rweyemamu, Gideon Shoo, Shaaban Kanuwa etc. Siku Rais Mkapa
alipomvua urais Jenerali
Ulimwengu (2000 au 2001) nami nilitumiwa ujumbe na watu wa
serikali kuwa nisipopunguza
makali katika kukosoa serikali nitakiona cha mtema kuni. Kwa
hiyo,
wanaonihukumu kwa kutazama makala zangu zinazochambua
serikali ya Rais John Magufuli
yawezekana ni watoto wadogo tu (kiumri au kiakili) ambao
enzi hizo walikuwa
hawajajua (au hawataki) kusoma, au ni watu wazima
waliobahatika kusoma makala
zangu katika kipindi cha miaka 10 tu iliyopita. Sikosoi
serikali kwa chuki bali
kama njia ya kuamsha waliolala, kunyosha yanayokosewa ili
yasahihishwe, wananchi
wapate huduma wanazostahili. Hiyo ni sehemu ya kazi ya
waandishi wa habari na
vyombo vya habari. Namwambia rais kupitia gazetini kwa kuwa
ndipo pangu, na kwa
kuwa wengi waliomzunguka wanaogopa kumwambia ukweli;
wanamsifu badala ya
kumwonesha kasoro ili asahihishe mambo. Yeyote atakayeingia
Ikulu, kama nipo nitafanya
kazi hiyo kwa uzalendo mkubwa, bila woga wala upendeleo,
nikihoji kuhusu
masuala muhimu ya taifa. Kama rais ameamua kujiita mtumbua
majipu, lazima
wawepo wengine wanaoweza kutumbua majipu yake kila
yanapoiva. Mimi nimejipa
kazi ya kutumbua majipu ya Ikulu – iwe ya Magufuli,
Ngurumo. Lowassa, Abdallah
au Juma!


3. Sijawahi kuwa
shabiki wa mgombea yeyote wa CCM, kama mwandishi anavyodai.
Lakini kama
mwandishi wa habari, nimefanya kazi na wanasiasa wote bila
kujali itikadi. Kwa
hiyo, nisingeweza kuwa shabiki wa Mzee John Malecela, kama
inavyodaiwa. Mwaka
2005 nilitafutwa sana, niliombwa sana na watu wa timu ya
Kikwete niwaunge mkono,
nikakataa. Nilikuwa na sababu mbili. Kwanza, niliamini kwa
dhati kwamba Jakaya
Kikwete hakuwa mgombea bora katika wenzake 10 katika kundi
lao la wagombea 11
ndani ya CCM. Niliona kama kuna wagombea wanamzidi uwezo,
upeo, ujasiri,
uthabiti, umakini, uadilifu na kadhalika. Msimamow angu huo
haujabadilika hata
baada ya miaka 10 ya utawala wake. Niliwaeleza
walionishawishi kuwa urais una
hadhi na viwango vyake. Sikuona kama Kikwete alikuwa
anakidhi viwango hivyo, nilipomlinganisha
na wenzake 10. Pili, sikuwa tayari kuunga mkono mgombea wa
CCM, kwa kuwa sikutamani
kuwa na rais kutoka CCM tena. Niliamini katika mabadiliko
ambayo yanaambatana
na kuondoa mfumo mkongwe na kuweka mpya. Kuunga mkono
mgombea yeyote wa CCM
kungekuwa kinyume cha ukweli na msukumo huo. Hata hivyo,
nilikuwa na mgombea
wangu kupitia Chadema - Freeman Mbowe. Nisingeweza kufanya
kazi ya kubeba CCM
wakati nina mgombea wangu.


Kilichootokea ni
kwamba, nikiwa mhariri wa Tanzania Daima Jumapili,
nilishirikiana na wenzangu
kusaka exclusive interviews na
wagombea urais. Mimi nilipangiwa kumpata na kumhoji Mzee
John Malecela. Naye
hakuwa tayari kuzungumza na waandishi kwa sababu alidhani
Kikwete anawatumia
kumchimba, kama alivyokuwa amewatumia "kumuumiza" huko
nyuma. Baada ya kunikwepa
mara kadhaa, baadaye aliridhia kuzungumza na mimi. Maswali
niliyomuuliza
yaliandaliwa kwa ushirika kati yangu na wahariri wenzangu.
Kitaaluma, hata kama
hukubaliani na msimamo au  hoja za mtu
unayemhoji, unachopaswa kufanya ni kumtendea haki.
Unamsikiliza. Unaandika
alichosema. Huongezi maoni yako popote.


Hata Mzee
Malecela
hakuamini kama ningeweza kumtendea haki, hadi aliposoma
mahojiano yake gazetini.
Nilimnukuu neno kwa neno. Sikujadili kauli zake. Msomaji
mmoja alinipigia simu
kuuliza, "mbona sioni wewe unasemaje kuhusu Mzee
Malecela?" Nikasema,
"kitaaluma, sina sababu ya kuweka maoni yangu katika
stori ninayoandika.
Huo ni msimamo wake, ni maoni yake. Nikitaka kuandika maoni
yangu nitaandika
mahali pa maoni, si katika stori
yake."


Wasiojua msimamo
huu,
hasa waliokuwa washindani wake, walitaka nimshughulikie
katika habari hiyo, au
nisimhoji kabisa. Baadhi yao wakadhani mimi ni mtu wa Mzee
Malecela. Walikosea.
Baadaye nilisikia mahali Fulani, Kikwete, Rostam Azizi na
Edward Lowassa wakisema,
"Ngurumo ni mtu wa Dk. Salim." Nao hawakuwa
sahihi. Sikuwa na mtu
katika CCM.

Walipokwenda
Dodoma
kuchukua fomu za urais katika chama chao, walinikuta. Wote
11 walijieleza na
kujibu maswali yetu. Ajabu, niliguswa na maelezo ya Mzee Idd
Simba. Kwangu, ndiye
alionekana anajua kwanini anataka kuwa rais. Aliniridhisha.
Lakini alikuwa
anapoteza muda, kwa kuwa hakuwa chaguo la chama chake.
Hakuwa na mtandao.
Alishapigwa na kuchafuliwa ili asipite. Kama wengine wote
waliokuwa
wameshachafuliwa na kambi ya Kikwete – Frederick Sumaye,
Mark Mwandosya, Dk.
Salim Ahmed Salim, Mzee Malecela - naye aliishia hapo.



4. Katika makala
zangu kati ya 2006 na 2015, kama umenisoma vema, nimewahi
kumshambulia Lowassa
mara moja au mbili hivi. Nakumbuka mara ya kwanza nilimsema
alipotaka kutumia
mabavu kufungia gazeti la Tanzania Daima lilipomkosoa.
Nilikuja juu, nikasema
anatumia vibaya madaraka yake. Mara ya pili nilimwandama
Lowasa na Rostam kwa
kosa moja kubwa - kutuletea Kikwete. Nilisema Tanzania
haitawasamehe wasipotubu
dhambi hiyo, wakaachana na Kikwete; maana kama si wao,
Kikwete asingekuwa rais.
Baadaye nilipopata fursa ya kuzungumza nao, walikiri kosa
hilo, na sasa hivi wanajuta.
Tena wanashangaa mimi nilimjuaje kuliko wao; maana wakati
namkosoa, nao
waliniona mbaya.

4. Lowassa
alipojiuzulu uwaziri mkuu, nilimpongeza. Kwanini?
Nilibahatika kujua undani wa
sakata la Richmond kutoka kwa wahusika waliomsulubisha
bungeni. Nilijua kilichongunduliwa
na ripoti, ambacho hakikuandikwa; na kwanini Kikwete
hakuingizwa kwenye ripoti.
Nilijua kuwa Richmond haikuwa mali ya Lowassa. Nilijua
ushiriki wake katika mchakato
wa kuipa tenda. Nilijua hatua alizotaka kuchukua kuvunja
mkataba, rais
akakataa. Nilijua jinsi alivyokutana na rais Ikulu Chamwino,
mmoja akamdanganya
mwenzake, Lowassa akajiuzulu. Nilijua nguvu iliyotumiwa na
kamati ya wabunge wa
CCM kumshawishi rais aachane na Lowassa. Nilijua jitihada za
watu wa usalama wa
taifa kuhusu sakata hilo. Nilijua ufa uliojengeka kati ya
Lowassa na Kikwete
tangu siku hiyo. Nilijua kuwa Lowassa alikua na siri nyingi
alizomtunzia rais
wake, wakati rais anasmhughulikia kichini chini.



Niliandika baadhi
ya
mambo hayo, si kwa kumsakama Lowassa, bali kuwa kumtaka
atoboe siri. Nilitaka
ajue kuwa anamwamini sana Kikwete, lakini Kikwete haaminiki.
Katika makala
moja, niliandik hivi: "Hongera Lowassa, bado
Kikwete." Wakati nafanya
hayo yote, Lowassa alikuwa haoni umuhimu wa kauli zangu.
Alikuwa miongoni mwa
watawala walionichukia. Alikuwa bado nan damu ya CCM.
Alikuwa amefumbwa macho,
haoni tunachokiona sisi. Lakini nilijua,, na niliandika,
wakati mwingine kwa uwazi
au kwa mzunguko, kuwa siri ya Richmond iko kwa Kikwete, na
kwamba Lowassa aliwajibika
kisiasa kutokana na madaraka yake. Alipaswa kuwajibika kwani
alihusika.

Hata wakati
anawania
kuteuliwa na CCM agombee urais, baadhi yetu tulijua kuwa
angekatwa tu. Wakati
huo, hakusikia ushauri wowote wa kumtenga na CCM. Wakati
wake wa kufunuliwa
ulikuwa haujafika. Ulipowadia, akaumizwa kwelikweli, ndipo
alijua kwamba yumo
katika kundi lisilo lake. Akawa na ujasiri usiotarajiwa,
akaondoka CCM, akajiunga
na Chadema. Si jambo la kawaida kwa mtu aliyewahi kuwa
waziri mkuu, katika
siasa chafu za Tanzania, tena aliyetangazwa kuwa fisadi na
kuhusishwa na uchafu
mwingi, kuhama chama tawala – na akawaambia "kama mna
ushahidi wa tuhuma zangu,
nipeleke mahakamani!" Si rahisi.


5. Ni kweli.
"Laana"
ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere imekuwa inamwandama
Lowassa. Ni ukweli
wa kihistoria kwamba kama si Mwalimu Nyerere kumzuia 1995,
Lowassa ndiye
angekuwa rais. Ni kweli kwamba tangu pale, ndani ya CCM
yamejengeka makundi
dhidi ya Lowassa kwa sababu ya kile kinachoitwa
"kukataliwa na
Nyerere." Ni kweli kwamba Kikwete alimteua Lowassa
katika mazingira hayo,
na hata alipomteua, kuna mbunge mmoja kijana alitaka
kulianzisha kwa kuomba
wazee wamsaidie kujenga hoja ya kumkataa ili asiidhinishwe
na Bunge. Ni kweli
kwamba mbunge huyo alikwenda hadi kwa Mzee Malecela,
akamwambia "Mzee na
wewe umeondolewa kwenye urais kwa sababu Nyerere alikukataa.
Kwanini tusimkatae
na huyu Lowassa kwa sababu hizo hizo?" Mzee Malecela
alimweleza mbunge
huyo kuwa asingemuunga mkono katika hilo kwa sababu mbili.
Kwanza, asingeweza
kuzuia uteuzi wa rais kwa kuwa wanamtandao walikuwa
wameshika serikali. Sana
sana ilikuwa ni kutafuta ugomvi na serikali mpya, ugomvo
ambao mbunge huyo
asingeushinda, na ungemsababishia wakati mgumu kwa miaka
mitano. Pili,
alimwambia kuwa yeye anamjua Lowassa, kwani alipoteuliwa kwa
mara ya kwanza
kuwa waziri, alipelekwa ofisi ya waziri mkuu, wakati huo
Malecela akiwa waziri
mkuu. Alisema kwamba licha ya maneno yanayosemwa dhidi ya
Lowassa, ana kasoro
zake kama binadamu, lakini kama ni uchapakazi, Lowassa
akisema jambo fulani
litafanyika, haweki mguu chini hadi
lifanyike.


6. Ni kweli kuwa
Lowassa aliteuliwa uwaziri mkuu katika mazingira magumu,
ambamo Kikwete alikuwa
pia amemwahidi Samwel Sitta nafasi hiyo wakati wa kampeni.
Kwa sababu hizi za
kihistoria, Sitta aliamini kwamba Lowassa asingeteuliwa.
Alishangazwa na
ushauri aliokuja kupewa na Kikwete baada ya kuapishwa,
kwamba "Bunge
linahitaji Spika makini kuliko Pius Msekwa, hivyo tunaona
ugombee uspika."
Baadaye ilipoletwa bahasha yenye jina la waziri mkuu
bungeni, akakuta ni
Lowassa. Lowassa na Sitta wakawa wanatunishiana misuli ya
madaraka – huyu wa
serikali, huyu wa bunge. Bifu lililoibuka tangu hapo kati ya
Sitta na Lowassa,
huku Sitta akisaidiana na akina Harrison Mwakyembe na Lucas
Selelii kusumbua
Lowassa na Kikwete halijaisha hadi sasa. Hata sakata la
Richmond lilichipuka
katika mkondo wa Sitta na Mwakyembe kutaka kumwondoa Lowassa
kwenye uwaziri
mkuu. Sitta ndiye aliingiza Richmond nchini akiwa Mkurugenzi
Mkuu wa TIC.
Aliijua vema, lakini alifanikiwa kumshughulikia Lowassa kwa
sababu waliona
"mkono wake katika Richmond." Ndiyo maana baada ya
Lowassa kijiuzulu,
Sitta hakutaka bunge lihoji tena sakata hilo, na akafunga
mjadala bila hata
serikali kutimiza maazimio ya bunge kuhusu Richmond. Maelezo
ni marefu. Yapo
mengi ambayo jamii haiyajui kuhusu Richmond, na mimi
nakumbuka vema kwamba haya
ninayoandika hapa nimewahi kuwaandika kwa kirefu katika
makala zangu. Katika
maandishi yangu nilimkosoa sana Kikwete, na kumsuta Lowassa
na wenzake. Nilieleza
nilichojua. Kumbukumbu zipo. Siwezi kulishwa
maneno.


7. Mimi kufanya
kazi
na Dk. Willibrod Slaa lilikuwa jukumu nililopewa na chama.
Nilikuwa naye kabla
ya uchaguzi, wakati wa kampeni na baada ya kampeni.
Sikufanya naye kazi
kirafiki au kwa kujikomba. Nilifanya nilichopaswa kufanya
naye kwa ajili ya
jamii pana ya Watanzania. Kimsingi, nilifurahia utumishi
wangu huo. Kwa kazi
tuliyofanya kwa kushirikiana na Dk. Slaa na wengine wengi,
habari zilifika kila
kona, na kwa sababu ya kipaji na haiba yake binafsi,
alikubalika kwa wananchi.
Hadi Julai 2015, alipokuwa akisimama majukwaani, wananchi
walikuwa wakimuita "rais
wa mioyo wa Watanzania." Leo hana anuani hiyo tena. Sababu
zinajulikana. Dk.
Slaa hayupo Chadema tena. Alifanya kazi nzuri kama ya Musa
tunayemsoma katika
Biblia. Musa aliamriwa na Mungu aongoze Wanaisraeli kutoka
Misri hadi Kanaani.
Walikaa jangwani kwa miaka 40. Hatimaye walifika kwao,
lakini Musa hakufika.
Tulimwandaa Dk. Slaa agombee, naye alijiandaa agombee tena
urais 2015. Lakini
hakugombea. Kilichotokea ama mnakijua au mnakikwepa.
Yaliyomkuta Dk. Slaa
hayawezi kuondoa kazi nzuri aliyofanya akiwa mwanachama na
kiongozi wa Chadema.


8. Lakini kama
Dk.
Slaa si mwanachama tena wa Chadema, na hagombei tena urais,
haina maana kwamba
tuendelee kumfuata huko alikokimbilia. Kwamba Lowassa
alikuwa mwana CCM, tena
tuliwahi kumsema akiwa huko, haina maana kwamba hana haki ya
kuhama na kujiunga
nasi. Na wengi unaowaona leo katika vyama vya upinzani -
hata kwa Dk. Slaa
ilikuwa hivyo - walitoka CCM. Tena wengi wao waliingia
upinzani baada ya
kukatwa majina au kufukuzwa na CCM. Lowassa amezungumzwa
sana kwa sababu ya
ukubwa wa jina lake. Hakuwa mwanachama wa kawaida katika
CCM. Hakuwa kiongozi
mdogokatika serikali. Lowassa alijijenga akawa taasisi ndani
ya CCM. Taasisi
hiyo ilipohamia Chadema, isingeweza kutua bila kishindo. Na
hawezi kuungwa
mkono na kila mtu. Kuna watu hadi sasa hawamwelewi; wengine
(wachache) hawamkubali.
Ndivyo siasa ilivyo. Katika hali ya kawaida, sitarajii
mwanachama au mfuasi wa
Chadema, aunge mkono Dk. Slaa aliyeondoka eti kwa kuwa huko
nyuma alifanya kazi
naye;  amwache Lowassa aliyeingia na
kukabidhiwa jukumu jipya la kitaifa.


9. Unazungumzia
taswira
ya Lowassa kama fisadi? Kwamba hakupaswa kupokelewa Chadema?
Tujadili. Mimi ni
Mkristo Mkatoliki. Nimebahatika kusoma historia ya Kanisa.
Najua mchango wa
Mfalme Constantine ambaye alikuwa mpagani katika kukuza
Kanisa, kulipa uhuru wa
kuabudu hata kabla mwenyewe hajaongoka. Kama Himaya ya
Kirumi isingekuwa na mtu
kama Constantine, ingechukua miaka mingi sana kwa ukristo
kushamiri kwa sababu
ulikuwa unapigwa vita na serikali yake. Mchango wake ndio
uliwezesha wakristo
kusali hadharani, kujenga makanisa, kuhibiri kwa uwazi; na
alipoongoka mfalme
kila mtu akataka kuingia katika dini mpya ya Mfalme. Wewe
endelea kujadili
upagani wa Constantine.


Nimesoma pia
historia
ya maisha binafsi ya Mt. Augustine wa Hippo. Vile vile
nimesoma kitabu
"Confessions of St Augustine." Anasema wazi kuwa
hakuna uchafu ambao
hajawahi kufanya akiwa kijana. Alipoongoka akabatizwa,
amekuwa mkristo hodari kuliko
hata aliowakuta; hadi akawa askofu. Leo historia inatambua
kama mmoja wa walimu
na mababa wa kanisa.

Nimesoma Biblia
nikaona jinsi Sauli alivyokuwa anatesa Wakristo. Aliwafunga.
Aliwapiga. Aliwaua.
Aliongoka akiwa njiani anakwenda kutesa Wakristo. Akabatizwa
jina Paulo.
Mwanzoni, Wakristo walimwogopa, hawakuamini kama ana nia
njema nao. Alipojitambulisha
kwa mitume, kwa kauli ya Mtume Petro, wakampokea, akawa
mwenzao.



Kwamba aliwahi
kutesa
nan kuua wakristo kwa amri za utawala mbovu uliokuwapo,
haikumzuia kuhubiri
injili kwa kauli na maandishi. Soma  nyaraka
zake kwa Wakorinto, Wakolosai, Wagalatia,
Wafilipi, Wahebrania, Waefeso; kwa Tito, kwa Timotheo, na
kadhalika. Paulo
ambaye hakuishi na Yesu, Paulo aliyetesa wafuasi wa Yesu,
ndiye alikuwa mhubiri
mkuu na mwandishi wa nyaraka nyingi kuliko wanafunzi 12 wa
Yesu. Hatujadili tena
mateso aliyosababisha kwa Wakristo. Hayo ni maisha ya
kale!


10. Kwa miaka
ipatayo
20 sasa, nimejipambanua kwa maandishi bila unafiki. Nakosoa,
natafakari,
nafikirisha. Shabaha yangu ni kusaidia walio madarakani
wajirudi. Siandiki kwa
chuki. Ni uzalendo unaojitokeza katika kutazama upungufu wa
watawala na kupiga
kelele. Kelele hizi zinaposikilizwa, zinanyoosha mengi.



Kwa mfano,
Jumatatu
Machi 7, 2016 niliandika uchambuzi katika safu ya Gumzo la
Wiki katika gazeti
la MwanaHALISI, nikasema jinsi Rais John Magufuli
alivyofedheheka kwa kuchomeka
Kiingereza kibovu katika hotuba ya Kiswahili mbele ya
viongozi wenzake Jumjuiya
ya wa Afrika Mashariki na wageni waalikwa. Nilishauri atumie
Kiswahili katika
hotuba zake ndani na nje ya nchi, kwa kuwa hana kipawa na
kuzungumza Kiingereza
fasaha, na kwa kuwa Kiswahili ni lugha yetu ya taifa, yenye
hadhi ya kimataifa.


Kuna watu
walinishambulia.
Wakadiriki hata kupotosha mada yangu, eti nashabikia
Kiingereza. Eti nimwache
azungumze Kiingereza kibovu. Sikuahangaikia nao, kwani watu
wa jinsi hii
wanajikomba kwa wakubwa, na ndio wanalea kasoro za
wakubwa.

Bahati nzuri,
rais
mwenyewe amezingatia ushauri wangu. Jumatano, siku mbili
baadaye, alimpokea
mgeni wake, Rais wa Vietnam, Ikulu, Dar es Salaam. Katika
mazungumzo na
waandishi wa habari, Rais Magufuli alitumia Kiswahili.
Nilimpongeza kwa usikivu
huu. Nilifurahi kwamba alisikia ushauri. Na hii ndiyo kazi
ambayo baadhi yetu
tumejipa.

Mashabiki wa
makosa ya
wakubwa ndio wanaonishambulia ninapoyagusa. Sijui wanafaidi
nini tusipowakosoa.


Nawasilisha!







Ansbert Ngurumo

Mobile    +255 767 172 665www.freemedia.co.tzwww.voxmediatz.com
www.ngurumo.wordpress.com
www.ngurumo.blogspot.com



On Thursday, March
10, 2016 12:19 PM, 'lang'itomoni lokomoi' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:




ANSBERT
NGURUMO, kwa takribani miaka yote kumi ya utawala wa wa
Kikwete, alitumia
kalamu yako kumuuliza Rais Kikwete alichokuwa akikita
maswali magumu, aliuliza
maswali hayo bila kuchoka kwa muda wote huo hakuna
kumbukumbu kama aliwahi
kujibiwa.


Mwaka 2005,
katika mchakato wa uteuzi wa CCM wa kumtafuta mteule wake
ambapo Kikwete
aliibuka kidedea, Ngurumo alikuwa katika kambi ya Malecela,
waziri mkuu na
makamu wa kwanza wa rais mstaafu.


Kwa bahati
mbaya jina la Malecela lilitupwa mwanzoni kabisa katika
mchakato huo kitendo
hicho hakikumfurahisha Ngurumo ndipo akaamua kuwa mpinzani
wa CCM


Mwaka 2010,
Chadema ilipomsimamisha Dk. Wilboard Slaa ambaye kwa kidogo
alikuwa mgombea
urais kutoka upinzani mwenye muonekano wa uzalendo wa
uadilifu wa kweli.
Hapo
ndipo Ngurumo akapata pa kupumulia, akaingia front kumuunga
mkono Dk. Slaa
kabla ya kupata bahati ya kuwa miongoni mwa watu watano
muhimu wa kubeba mikoba
ya mgombea huyo wa urais katika kipindi chote hicho
akifanywa kuwa mratibu na
mshauri.


Kila
Mtanzania mwenye kuitakia afya njema nchi yake angeweza
kuungana na Dk. Slaa
kutokana kilele cha ufisadi ambacho nchi ilikuwa imefikia
chini ya uongoiizi wa
Rais Kikwete, mafisadi wakitamba kifua mbele bila ya kuguswa
wakati walikuwa
wakifahamika na vitendo vyao vikijulikana


Binafsi
nawachukia mafisadi na vitendo vyao kwa nchi hii kama
ambavyo niliamini  Kama Ngurumo na Dk. Slaa
wanavyowachukia
mafisadi  pamoja na vitendo vyao vya
kifisadi.


Mwaka 2010
niliamini asalimia zote kwamba ndoa ya Ans Ngurumo na Dk
Slaa ilitokana na
msimamo wa kuwachukia mafisadi wananchi hii pamoja na
vitendo vya kifisadi,
hivyo basi iliwahitaji wanyonge hao waunganishe nguvu zao
pamoja na wanyonge
wengine dhidi ya nguvu ya mafisadi.


Kumbe
nilikosea kuamini hivyo kwa Ans Ngurumo ila kwa Dk Slaa
nilikuwa sahihi.
Kilichowaunganisha mwaka 2010 haukuwa ukombozi wa nchi dhidi
ya mafisadi, kumbe
Ans Ngurumo  alikuwa anatazama mbali
zaidi, maslahi binfsi zaidi ya kiuchumi na
kisasa.


Kwa nini
nilikosea,
Baadhi ya maswali ya Ngurumo kwa Kikwete yalihusu, kwa nini
kiongozi huyo
alikiuka miiko nya mwalimu Nyerere kwa kumteua Lowassa kuwa
waziri mkuu wake?


Na hata
mwaka 2008 Rais Kikwete alipolazimika kuvunja baraza la
mawaziri na kumfukuza
Lowassa kutokana na kashfa ya ufisadi wa richimond, Bado
Ngurumo liendelea
kusisitiza kwa rais kikwete enzi hizo kwamba mzimu wa Mwl.
Nyerere hautamuacha
salama kwa kuendelea kumkumbatia fisadi Lowassa ndani ya
chama chake cha CCM.


Kwa msimamo
huo wa wa  Ngurumo wengi wetu tulidhania
baada ya Dk.Slaa kusutwa na nafsi yake hivyo kufanya uamuzi
mzito wa kuachana
na Chadema, baada ya uongozi kufanya kosa kubwa la kiufundi
la kukabidhi chama
kwa lowassa na kumfanya kuwa mgombea urais, Ngurumo naye
angeonyesha uzalendo
wake wa kuunga mkono hatua hiyo ya Dk. Slaa.


Leo hii kwa
neema za Mungu, ndani ya CCM amepatikana DK. Magufuli
aliyedhamiria kupambana
na uchafu wake wote ndani ya serikali na taasisi zake, Kina
Ngurumo  hawa wa kumdhikhaki na kumkejeli?



 Eti
anadiriki kusema hana dhamira hiyo na wala
hakuwa chaguo la watanzania, bali Lowassa ambaye yeye
NGurumo alikuwa
akimsakama Kikwete usiku na mchana akimtaka kumfunga jela
kwa ufisadi ndio huyo
huyo leo anasema kuwa ndio chaguo la
watanzania?


Huyu Ngurumo
hakuwahi kumwamini Kikwete kama kama president material na
sasa anandika upuuzi
ule ule kama hamuamini Dk. Magufuli kama president material.



Yeye
alimuamini Mwalimu NYerere akamuamini Malecela na akamwamini
Lowassa wakati
Mwalimu aliwakataa wote Malecela na Lowasa, tena miaka
takribani kumi akitumia
kalamu yake kutuaminisha kuwa fisadi leo anatwambia Lowassa
ndiye president
material na alikuwa chagua la watanzania na angekuwa rais
bora kuliko Dk.
Magufuli?





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.








--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.







--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment