Thursday, 3 March 2016

Re: [wanabidii] ‘Magufuli anaua upinzani’

Hawei kuuua. anaweza kuudhoofisha tu. Lakini pia upinzani ukijipanga ukapata agenda utaimarika. Shida ni upinzani ufanyeje kuwapata walenga maendeleo na kuwaondoa walenga urais au ubunge nk.
--------------------------------------------
On Thu, 3/3/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] 'Magufuli anaua upinzani'
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, March 3, 2016, 1:09 PM


UTENDAJI wa Rais John Magufuli, umemkuna Mwenyekiti wa Bodi
ya Barabara
Tanzania, Dk. James Wanyancha, kiasi cha kumfananisha mkuu
huyo wa nchi
na sumu itakayoua nguvu ya vyama vya upinzani
nchini.
Dk.
Wanyancha aliyepata kuwa Mbunge wa Serengeti mkoani Mara na
Naibu Waziri
wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi katika Serikali ya Awamu ya
Nne ya Rais
Jakaya Kikwete, anatabiri kwamba kifo cha nguvu ya upinzani
kitatoa
fursa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kushika
madaraka ya nchi
hata kwa miaka 200 ijayo.
Anasema
kwamba aina ya utendaji
inayoonyeshwa na Rais Magufuli katika kukabili wezi na
wabadhirifu wa
mali ya umma na kutetea maslahi ya wanyonge, itaangamiza
nguvu ya
wapinzani kwa kuwakosesha cha kukichongea CCM kwa
wananchi.

"Lakini
kikubwa zaidi, Watanzania tunapaswa kumshukuru Mungu kwa
kumpata
Rais huyu, atalipeleka Taifa letu kwenye mafanikio makubwa,
watu
watakuja kushangaa," anasema Dk. Wanyancha katika
mahojiano maalum na
Raia Mwema wiki hii akitoa maoni yake kuhusu utendaji wa
Rais Magufuli.

Anajivunia
umakini wa chama chake cha CCM uliompatia Dk. Magufuli
baraka ya kugombea urais mwaka jana, akisema kitendo hicho
kimeudhihirishia umma wa Watanzania kwamba chama hicho
kikongwe
hakijafilisika watu waadilifu, waaminifu na wachapakazi
mahiri.

"CCM ni chama kikubwa, si kweli kwamba
wanachama wake wote ni mafisadi,
bado kina watu wengi waaminifu na waadilifu, inategemea
umemchagua nani…
tungechagua fisadi mambo yangekuwa mabaya, lakini
tunajivunia chaguo
letu la Dk. Magufuli, ni kiongozi safi na tumaini la
maendeleo ya kweli
ya nchi yetu," anasisitiza Dk. Wanyancha aliyepata pia
kuwa Mbunge wa
Bunge la Afrika.
Kuhusu mtazamo wa watu wachache wanaodhani kasi
ya utendaji aliyoanza nayo
Rais huyo wa Awamu ya Tano itaishia kuwa
nguvu ya soda, Dk. Wanyancha ambaye pia ni Mshauri wa
Kujitegemea wa
Uhifadhi wa Mazingira, anasema:
"Hao wanajidanganya, huyu Dk.
Magufuli mimi ninamfahamu vizuri, alikuwa bosi wangu kwenye
Wizara ya
Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, yeye yuko hivyo siku zote, ni
mchapakazi
hodari na ni mtu wa kujituma na kujitolea.
"Ninaweza kusema
kwamba Watanzania sasa tutarajie kuona nchi yetu inapata
mafanikio
makubwa zaidi kupitia uongozi wake, tutarajie kuona huduma
nzuri za
kijamii zinapatikana hapa nchini zikiwamo za afya, elimu,
maji,
barabara, umeme na mawasiliano.
"Ninasema hivyo kwa sababu Rais
Magufuli ameonyesha dhamira ya kweli ya kuboresha maisha ya
Watanzania
bila ubaguzi. Tukisimamia vizuri rasilimali zetu kama
anavyoonyesha
kiongozi wetu huyu, Tanzania itaweka historia ya kuwa
miongoni mwa nchi
tajiri sana duniani.

Nyangwine: Nchi iligeuzwa shamba la
bibiNaye mbunge wa zamani wa Tarime mkoani Mara,
Nyambari Nyangwine,
amesifu utendaji wa Rais Magufuli, huku akiibuka na hoja
kwamba kabla ya
kiongozi huyo kuingia Ikulu, nchi ilikuwa imekosa ulinzi
thabiti
mithili ya shamba la bibi.
"Ninaridhishwa na utendaji wa Rais
John Magufuli, kwa kweli ameonyesha utendaji uliotukuka,
ameimarisha
uongozi wa nchi yetu iliyokuwa imegeuzwa kuwa kama shamba la
bibi lisilo
na mlinzi," ameeleza Nyangwine.
Kada huyo wa CCM ambaye pia ni
Mwenyekiti wa kampuni za Nyambari Nyangwine zinazochapisha
na kusambaza
vitabu vya kiada na ziada katika shule za sekondari,
anamtazama Rais
Magufuli kama tumaini halisi la kuifikisha Tanzania kwenye
neema ya
uchumi imara na maendeleo ya kutolea mfano
mzuri.
"Tulikuwa
tunataka kiongozi kama huyu hapa Tanzania, kiongozi mwenye
uthubutu wa
kuchukua maamuzi magumu haraka, maana huko nyuma nchi yetu
iliyumba
kutokana na ukosefu wa maamuzi magumu yenye maslahi kwa umma
na Taifa
letu."
"Kwa kweli kinachonifurahisha zaidi kwa Rais
Magufuli ni
ujasiri wake wa kufanya maamuzi magumu papo kwa hapo badala
ya kusema
'ngoja tuunde tume tuchunguze', huyu ndiye Rais
tuliyekuwa tunamhitaji
kwa ajili ya kuimarisha uwajibikaji serikalini na maendeleo
ya kweli
nchini.
"Matumaini yangu ni kwamba mkuu huyu wa nchi
ataendelea
kuonyesha uongozi uliotukuka ikiwa ni pamoja na kuwezesha
wananchi
kiuchumi, tukiwa na uchumi imara, nchi yetu itapiga hatua
kubwa ya
maendeleo katika sekta mbalimbali," anasema
Nyangwine.
Pamoja na
hatua nyingine zenye mwelekeo wa kudhibiti wizi na
ubadhirifu wa mali ya
umma, matumizi mabaya ya madaraka serikalini, kwa nia ya
kuwezesha
unafuu wa maisha kwa wananchi wa hali ya chini, Rais
Magufuli
ameshawavua madaraka na kuwasimamisha kazi vigogo kadhaa
katika kipindi
kifupi kinachokaribia miezi minne sasa.
Tofauti na matarajio ya
baadhi ya watu kwamba kiongozi huyo angebanwa na chama
chake, CCM, kiasi
cha kukosa uthubutu wa kuwashughulikia vigogo wasiyo
waadilifu
serikalini, utendaji wake umewashangaza wengi, hasa kutokana
na msimamo
wake kuchukia ufisadi na rushwa, huku akiegemea zaidi kwa
wananchi wa
tabaka la chini.
Msukumo wa Rais Magufuli umeweka rekodi ya
kuongeza ukusanyaji wa mapato mara dufu na kudhibiti
matumizi yasiyo ya
lazima serikalini. Amefanikisha mambo mengi ya kitaifa kwa
muda huo
mfupi kwa kutumia kauli mbiu ya 'kutumbua majibu' katika
idara na
taasisi za umma.
Itakumbukwa kwamba siku chache baada ya
kuapishwa kushika madaraka ya nchi Novemba 6, mwaka jana,
Rais Magufuli
alifanya ziara zikiwamo za kushitukiza katika Hospitali ya
Taifa
Muhimbili (MNH), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka
ya Bandari
Tanzania (TPA), miongoni mwa idara nyingine, ambapo
alichukua hatua za
kinidhamu na kutoa maelekezo machungu yaliyowagusa baadhi ya
watumishi
wakiwamo wakiwamo makada wa CCM.
Lakini pia katika hali ambayo
ilidhaniwa na baadhi ya wananchi kwamba haitawezekana,
kiongozi huyo wa
nchi amefungua ukurasa mpya kwa kufanikisha utekelezaji wa
ahadi ya
chama chake ya utoaji wa elimu ya msingi hadi kidato cha nne
bure
kuanzia Januari mwaka huu.
Raia
Mwema



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment