Wednesday, 16 March 2016

Re: [wanabidii] HOTUBA YA BALOZI JUMA MWAPACHU KUTANGAZA KUREJEA CCM

Mwapachu alihama. Hatukujua kuwa alikuwa anafuata Cheo CHADEMA. Sasa amerudi CCM.
Tunajifunza mambo mengi hapa.
1) Chadema inahitaji kujua kuwa kama Lowasa angeshinda Serikali yake ingekuwa inaundwa na CCM. Kama msimamizi wa sera za nje wa Serikali ya CDM angetoka CCM. hatujui waziri wa uchumi, kilimo elimu na nyingine alikuwa hatoki CCM, basi CDM ijue kuwa serikali hiyo ingekuwa ya CCM.

2) Watanzania wajue kuwa wangekosea kufikiri wanaongozwa na CHADEMA kumbe wanaongozwa na CCM kwa jina la CDM. Taifa lingeyumba na linaweza kuyumba 2020 kama wakifanya kosa walilokwepa 2015.

3) Mwapachu alipohama tulimjadili. Tulisema ameonyesha kuwa hana maana. Sasa si kwamba amedhihirisha kuwa hana maana bali ameziki kupunguza na maana kidogo aliyokuwa amebakiza. Kumbe anayumbishwa na Mtu. Kwanza alienda CDM kumfuata Lowasa. Sasa anarudi CCM kumfuata Magufuli. Hatujajua kama magufuli amemuahidi au hapana. Tusubiri. Eti anatoa ushauri vijana wasihame tena. Anaiahidi CCM ikitaka iweke mtu wa hovyo maana hawezi tena kuhama. Alihama kwa sababu hakuweza kutambua kuwa magufuli hakuwa mtu wa Hovyo. Watu wote ambao mpaka tarehe 13 October 2015 walikuwa hawajajua kuwa magufuli ni mtu makini watu hao ni wa hovyo.. Haya ni maneno ya kujadili.

Mimi CCM ikiweka mtu wa hovyo nitaihama. Wakati ule ilipoelekea kuweka mtu wa hovyo nilikuwa nasema wazi kuwa sitampigia kura ya urais. Wakati huo nilikuwa namuona mtu wa hovyo anaelekea kukiyumbisha chama cha mapinduzi. Na nilikuwa naona mtu makini ndani ya CDM ambaye alikuwa ameshiriki kuijenga CDM na ikapendeza na kuwa chama mbadala. Mtu makini akatimka CDM na CCM ikaweka mtu makini na watu wa hovyo wakaimbia CCM. Kampeni za uchaguzi zikaanza. Mtu makini akaonekana wazi katika kampeni. Hotuba zake ziliguza matatizo ya watanzania. Mtu wa hovyo akaonekana pia. Mikutanoni hasemi chochote. watu makini wakawa wameona. Lakini Mwapachu tadi 13 October alikuwa hajajua kuwa Magufuli si mtu wa hovyo. Akahama kwa maneno yaliyotushangaza na nakumbuka kuandika kuwa kwa nini hakuyasema wakati CCM ikiwa hovyo na sasa inarekebika anaikimbia.
Ni kwa sababu ya hayo nashindwa kumuamini Mwapachu na nawashangaa watakaomuamini.
Nimeyaandika mimi Elisa Muhingo
--------------------------------------------
On Wed, 3/16/16, Makaveli Markus <jikomboe@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] HOTUBA YA BALOZI JUMA MWAPACHU KUTANGAZA KUREJEA CCM
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, March 16, 2016, 6:01 PM

Makubwa hayo....

2016-03-16 17:43
GMT+03:00 Atu Mwangomale <acanemwango@gmail.com>:
Ni haki yake kufanya maamuzi aliyoyafanya Ila mtu
mzima kusaliti chama kisa cheo anaonyosha ana uchu wa
madaraka.  si ajabu kusikia amehamia CUF
On 16 Mar 2016 17:34,
"Yona Maro" <oldmoshi@gmail.com>
wrote:
HOTUBA YA
BALOZI JUMA MWAPACHU KUTANGAZA KUREJEA CCM 
MIKOCHENI 16/03/2016Ndugu
zangu,Mtakumbuka kwamba mnamo tarehe
13 Oktoba 2015, nilitangaza kuihama CCM na kurejesha kadi
yangu ya uanachama kwenye ofisi ya CCM Kata ya Mikocheni.
Nilitoa maelezo kwanini niliamua kujiondoa CCM (maelezo hayo
pia niliyabandika katika ukurasa wangu wa facebook).
Nilieleza kwamba CCM imepoteza mwelekeo kwa kuamua kumnyima
haki ya kugombea mcha mungu Edwad Lowasa. Nikasema Edwad
Lowasa ndiye chaguo la wana-CCM na ndiye chaguo la
Watanzania. Nikasema nitakuwa mnafiki nikiendelea kubaki CCM
huku naamini Edwad Lowasa anafaa kuwa Rais kuliko John Pombe
Magufuli.Baada ya miezi
miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana.
Nililewa mahaba ya Lowasa, nililewa ahadi ya Lowasa kunipa
uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowasa ambayo
yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na
wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi
kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi
wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana
vyeo.Leo natangaza kurudi CCM
kwasababu nimeona kazi nzuri ya Magufuli. Nimefanya kosa
kubwa katika siasa ambalo nawasihi vijana kwenye siasa
wasifanye. Nilihama kwa kwasababu ya mtu (Lowassa). Nimerudi
kwasababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba CCM
ikiweka mtu hovyo baada ya Magufuli, sitahama. Usemi wa CCM
kwamba Chama Kwanza, Mtu Baadaye sasa ndio nauona maana
yake. Niliwalaumu CCM kwa kumuacha Lowassa lakini sikujua
kwamba CCM ina uwezo wa miujiza wa kuibua jembe bora
linaloitwa Magufuli.Naomba
mnisamehe kwa kulifanya jambo langu la kujitoa CCM na kurudi
CCM kuwa jambo la kitaifa ukizingatia kwamba sikuwa na
nafasi yoyote ya uongozi wa CCM wakati nahama na pia
sijawahi kuwa hata Mjumbe wa NEC ya CCM na nilikuwa nje ya
ulingo wa siasa za CCM kwa miaka 20. Niliamua kulifanya
jambo kubwa ili kumsaidia Lowassa. Na sasa nimeamua
kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye
kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu
zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua
kumsaidia swahiba wangu.Naomba radhi kwa familia ya baba wa taifa Mwalimu
Nyerere kwa kuitumia kisiasa siku aliyokufa (tar 14 Octoba)
na kutumia msiba wake kutoa kauli za kisiasa zidi ya chama
chake alichokiunda na ambacho hadi anakufa alikuwa
mwanachama.Wananchi wote
tumuombee Magufuli na tumsaidie kwani tumepata nyerere
mpya.Mungu Ibariki
Tanzania 
mungu Ibariki AfrikaBalozi
Juma Mwapachu

--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment