TAMKO LA BALOZI JUMA V. MWAPACHU, KUREJEA UANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), Dar es Salaam, 16 Machi, 2016
Viongozi wa CCM, Mkoa, Wilaya na Kata ya Mikocheni;
Wana habari,
Ndugu zangu.
CCM OYEE! KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Awali ya yote naomba nitoe shurani zangu kwa uongozi wa CCM Kata ya Mikocheni kwa kuandaa shughuli hii maalumu kushuhudia tamko langu la kurejea katika Chama Cha Mapinduzi na kukabidhiwa kadi yangu upya.
Ahsanteni sana.
Wahenga wamenena kwamba, 'yaliyopita si ndwele, tugange yajayo'.
Kwa kiasi fulani, itikadi ya msemo huu ni kiini kimojawapo cha uamuzi ambao nimeuchukua hii leo wa kurejea katika chama changu; chama changu tangu mwaka 1967,
Ndugu zangu,
Yaliyotokea wakati wa harakati za kumpata mgombea urais ndani ya CCM na baadaye (wakati wa harakati) za kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa hakika kwangu, asilani, 'si ndwele'.
Ni maradhi ya kibinadamu yanayotibika kwa urahisi.
Hivyo, sioni haja au umuhimu wa kurejea mazingira hayo na hasa ikitambulika kwamba sikujiunga na chama chochote cha siasa.
Na kwa hakika, tangu Uchaguzi Mkuu umalizike, nimepitia kipindi kigumu cha kupima na kutafakari mustakabali wangu kisiasa.
Katika wiki zipatazo saba hivi sasa, nimekuwa na mawasiliano na ofisi hii ya Kata ya Mikocheni kuhusu vipi ningeweza kukubaliwa kurejea uanachama wa CCM. Ndugu Sudi Odemba wa Ofisi hii ni shahidi yangu.
Kipo kiini au msingi wa pili kwa nini narejea CCM. Ni vyema nitamke hili.
Msingi wenyewe unatokana na mafundisho na hekima za Rais (mstaafu) wa Awamu ya Pili, Mzee wetu Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
Mzee Mwinyi aliwahi kutamka kwamba, nanukuu; 'kila zama na kitabu chake.'
Alikuwa akifafanua utofauti wa misingi na mielekeo ya uongozi pale panapotokea mabadiliko ya viongozi kidemokrasia.
Maana yake ni kwamba viongozi wapya hupima hali ya mazingira halisi ya nchi, na hata yale ya vyama vyao vya siasa.
Wengi wao hufungua kurasa mpya zinazokidhi matarajio na matumaini ya watu.
Ndugu viongozi,
Imani yangu ni kwamba Tanzania hivi sasa imeingia katika 'zama' mpya na 'kitabu' kipya kimeandaliwa na kinazidi kufafanuliwa na Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Maamini pia zama hii mpya itaona uzinduzi wa kitabu kipya kuhusu uongozi ndani ya CCM.
Naamini kwa dhati kabisa kwamba Rais Magufuli atakaposhika hatamu za kuongoza CCM. Atakijenga chama hiki UPYA; ataimarisha CCM na kukirejesha katika misingi ya demokrasia na haki.
Na itabidi iwe hivyo kwa sababu ushindani wa kisiasa nchini umeimarika. CCM haina budi na italazimika kufungua milango upya ili kirejeshe hadhi yake kama chama cha wakulima na wafanyakazi.
Natoa shukrani zangu kwa uongozi wa CCM kwa kukubali kunipokea tena kama mwanachama.
Niko tayari katika ujenzi wa fikra mpya za kukiimarisha chama cheti.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
--Hata sisi CCM tungeweza kumpa uwaziri wa mambo ya nje, au waziri wa afrika mashariki; uwezo huo anao na haikuwa lazima kulitafuta hilo kutoka upinzani.
From: wanabidii@googlegroups.com <wanabidii@googlegroups.com> on behalf of Makaveli Markus <jikomboe@gmail.com>
Sent: Wednesday, March 16, 2016 4:01 PM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] HOTUBA YA BALOZI JUMA MWAPACHU KUTANGAZA KUREJEA CCMMakubwa hayo....
--
2016-03-16 17:43 GMT+03:00 Atu Mwangomale <acanemwango@gmail.com>:
Ni haki yake kufanya maamuzi aliyoyafanya Ila mtu mzima kusaliti chama kisa cheo anaonyosha ana uchu wa madaraka. si ajabu kusikia amehamia CUF
On 16 Mar 2016 17:34, "Yona Maro" <oldmoshi@gmail.com> wrote:--
--HOTUBA YA BALOZI JUMA MWAPACHU KUTANGAZA KUREJEA CCM
MIKOCHENI 16/03/2016Ndugu zangu,
Mtakumbuka kwamba mnamo tarehe 13 Oktoba 2015, nilitangaza kuihama CCM na kurejesha kadi yangu ya uanachama kwenye ofisi ya CCM Kata ya Mikocheni. Nilitoa maelezo kwanini niliamua kujiondoa CCM (maelezo hayo pia niliyabandika katika ukurasa wangu wa facebook). Nilieleza kwamba CCM imepoteza mwelekeo kwa kuamua kumnyima haki ya kugombea mcha mungu Edwad Lowasa. Nikasema Edwad Lowasa ndiye chaguo la wana-CCM na ndiye chaguo la Watanzania. Nikasema nitakuwa mnafiki nikiendelea kubaki CCM huku naamini Edwad Lowasa anafaa kuwa Rais kuliko John Pombe Magufuli.
Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowasa, nililewa ahadi ya Lowasa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowasa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.
Leo natangaza kurudi CCM kwasababu nimeona kazi nzuri ya Magufuli. Nimefanya kosa kubwa katika siasa ambalo nawasihi vijana kwenye siasa wasifanye. Nilihama kwa kwasababu ya mtu (Lowassa). Nimerudi kwasababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba CCM ikiweka mtu hovyo baada ya Magufuli, sitahama. Usemi wa CCM kwamba Chama Kwanza, Mtu Baadaye sasa ndio nauona maana yake. Niliwalaumu CCM kwa kumuacha Lowassa lakini sikujua kwamba CCM ina uwezo wa miujiza wa kuibua jembe bora linaloitwa Magufuli.
Naomba mnisamehe kwa kulifanya jambo langu la kujitoa CCM na kurudi CCM kuwa jambo la kitaifa ukizingatia kwamba sikuwa na nafasi yoyote ya uongozi wa CCM wakati nahama na pia sijawahi kuwa hata Mjumbe wa NEC ya CCM na nilikuwa nje ya ulingo wa siasa za CCM kwa miaka 20. Niliamua kulifanya jambo kubwa ili kumsaidia Lowassa. Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.
Naomba radhi kwa familia ya baba wa taifa Mwalimu Nyerere kwa kuitumia kisiasa siku aliyokufa (tar 14 Octoba) na kutumia msiba wake kutoa kauli za kisiasa zidi ya chama chake alichokiunda na ambacho hadi anakufa alikuwa mwanachama.
Wananchi wote tumuombee Magufuli na tumsaidie kwani tumepata nyerere mpya.
Mungu Ibariki Tanzania
mungu Ibariki Afrika
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:
Post a Comment