Thursday, 10 March 2016

Re: [wanabidii] Hakika Chadema ya sasa siyo ile

Kuna wkati ukweli ulisemwa na kubezwa. Lakini kama mama mwenye mimba anajaribu kuificha kuna wakati unafika haifichiki. Bila mageuzi makini CDM inayoyoma. Nalo laweza kubezwa na kudharauliwa ila wakati ukifika ikaja tutakaa kimya kama tulivyonyamazia mengine. Huenda katika kuihakikishia uhai Mbowe anastahili kurudishwa nyuma. Au benchi kabisa
--------------------------------------------
On Thu, 3/10/16, 'Lesian' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Hakika Chadema ya sasa siyo ile
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, March 10, 2016, 5:43 PM

Dhuh
Tena
wanojaribu kujenga hoja dhaifu za kumpaka mbowe matope ni
mimamluki ya ccm lakin wameshindwa.
Cdm ndio
chama kinachokua kila siku na tunashukuru ccm imekopi sera
za cdm na sasa wanazitekeleza though bado itawachukua mda
mwingi kuweza kutekeleza bse sera si zao na ndio maana
wamegawanyika
Mbowe ni kiongozi na analeta
mabdiliko makubwa ya kisiasa despite challenges
tunazopitia,hv sasa tunapambana vita ya katiba mpya ianze
kwa kua tuliokua tunawategemea kutetea katiba ya warioba
washanunuliwa na warioba mwenyewe hivyo naamini kupitia cdm
tutaanza vita hiyo na tutapata tu kwa kua bila katiba mpya
kuiondoa ccm ni shida.
Kipengele cha
kuhojiwa matokeo mahakamani kama ya uganda ikiwekwa tutakua
sawa

emuganda@gmail.com wrote:

Ansbert,All I can say is
thanks. Mwenye kusikia na asikie na mwenye kubeza
aendelee.em

Sent from my iPhone
On Mar 10,
2016, at 2:50 AM, 'Ansbert Ngurumo' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

Ngoja
nijadili hoja hii kwa kifupi. Nakuhakikishia, Mbowe hana
muda wa kukasirikia maoni yako. Ameitwa majina mengi tangu
1992. Lakini ukweli unabaki kuwa Mbowe ndiye mwenyekiti
pekee wa chama cha siasa ambaye amejenga na kukuza chama
chake wakati vingine vinakufa. Kwa vigezo vyote, Chadema
ndicho chama pekee kinachokua kwa kasi Tanzania. Watu wengi
waliokaa mbali naye hawamjui vema, na wanamdharau kwa sababu
za kipropaganda, na kwa kuwa hajikwezi.
Waliokaa
naye karibu wanatambua kuwa Mbowe ni kiongozi ambaye
amewekeza katika kutengeneza na kutanguliza wanasiasa
wenzake. Vipaji vingi unavyoona na kujua katika Chadema
vimeibuliwa naye. Kwa asilimia kubwa, Chadema ya 2004 hadi
sasa ni zao la ubunifu na uchapakazi wa Mbowe.

Hana
makuu.Ni msikivu kupita wanasiasa wote niliowahi kukaa nao,
ukimwondoa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ni mbunifu. Ni
mwepesi wa kubadilika kulingana na mahitaji ya wakati. Ni
mfuatiliaji asiyechoka wa mambo anayotaka. Anajua kujenga
hoja kutetea anachoamini. Kwa Tanzania ya sasa na siasa
zake, nadiriki kusema kuwa Mbowe is the most influential
politician of current politics. Hata siasa zinazofanywa na
Magufuli sasa zinaegemea katika mtazamo uliojengwa na
Chadema kwa miaka 10 mfululizo. UKAWA unayoiona leo
imejengwa kwa kiasi kikubwa katika mgongo wa Mbowe.

Propagandists
wa CCM na usalama wa taifa wamefanya kazi kubwa kummaliza
Mbowe kisiasa, wameshindwa. Wametumia magazeti yao, hasa
HOJA na TAZAMA. Tangu 2004, gazeti la HOJA limempiga Mbowe
kila wiki. Limeshindwa kumbomoa. Limpiga Chadema limeshindwa
kukivunja. Wametumia mbinu zote walizotumia dhidi ya
Augustine Mrema wa NCCR-Mageuzi na Ibrahim Lipumba wa CUF;
hazikufua dafu kwa Mbowe.
Hata mwaka
jana, Chadema kilipompokea Edward Lowassa, walithubutu
kupandikiza sumu dhidi ya Mbowe na Chadema. Haikuwa na
makali. Walitumia kila mtu waliyedhani angeweza kusaidia
kubomoa Chadema. Hawakufaulu. Walijaribu kukosanisha
Chadema, Mbowe na umma; wananchi ndio wakafumuka zaidi
kuunga mkono Chadema, Mbowe na Lowassa.
Hata
waliomhusisha na ujio wa Lowassa, hawakujua kwamba si Mbowe
aliyemshawishi Lowassa kujiunga na Chadema. Lakini baada ya
yeye kushawishika kuhusu umuhimu wa Lowassa katika harakati
za mabadiliko, alisimama kidete kukamilisha kazi
iliyoanzishwa na wenzake kwa ufanisi mkubwa. Na kweli,
huwezi kupuuza nguvu ya waliomshawishi Lowassa, au Lowassa
mwenyewe au Mbowe katika harakati za kuinua upya upinzani
Tanzania.

Itabidi
wanaomchukia Mbowe watafute mbinu mpya. Hizi za miaka 12
mfululizo zimeshindikana. Mbowe anakipanga upya chama
akishirikiana na viongozi wenzake, wapya na wa zamani. Moto
utakaowaka nchi nzima baada ya wiki hii si wa kubeza.
Propaganda za mtandaoni zitaendelea. Matusi ya magazetini
yataendelea. Lakini hayatakomesha ubunifu na uchapakazi wa
Mbowe na timu yake. Nimefanya kazi naye kwa karibu. Najua
ninachosema. Sihitaji kuambiwa Mbowe ni nani.

Unataka
kumjua Mbowe? Tazama Chadema. Tafakari imepita katika
mabonde na milima ipi. Itazame Chadema ya Edwin Mtei na Bob
Makani. Ilinganishe na ya Mbowe. Ilinganishe na vyama
vingine vya siasa. Utaelewa kwa nini Mbowe anapigwa vita na
watawala na wapambe wao. Mbowe ni mti wenye matunda.
Atarushiwa mawe tu. Bahati nzuri, hana kawaida ya kujibizana
na wanaompinga. Wakati nyie mnahangaika kumtwanga
mitandaoni, yeye anachapa kazi.

 Ansbert Ngurumo

Mobile    +255 767 172
665www.freemedia.co.tzwww.voxmediatz.com
www.ngurumo.wordpress.com
www.ngurumo.blogspot.com

On Thursday, March
10, 2016 6:37 AM, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com>
wrote:

Ukiniuliza Who is Mbowe?
Jibu ni rahisi sana. DALALI BORA TANZANIA.
Anisamehe kama atakasirika.

;-)

--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment