Wednesday, 9 March 2016

Re: [wanabidii] Hakika Chadema ya sasa siyo ile

Kichwa cha habari kinahakisi ukweli wa mambo au labda kimepita pembeni mwa ukweli.
Ni muhimi kuanzia mbali mahala fulani.
Twaweza kuanzia kuiangalia CHADEMA kabla ya michakato ya uchaguzi.
Jinsi ilivyokuwa ikipambana na ufisadi.
Tukaifuatilia CHADEMA wakati wa uchaguzi na hasa mchakato wa kumpata mgombea urais.
Hapo tukaona jinsi CHADEMA ilipomtosa mtu aliyetarajiwa na wengi kugombea urais na kumzoa a;liyekuwa anatuhumiwa kuongoza ufisadi. Hapo kuna daraja ambalo CHADEMA ua ng'ambo ile siyo CHADEMA ya ng'ambo hii.
Tunaweza kufuatilia maneno ambayo yalinenwa juu ya Mbowe. Kuwa kuna mabilioni ya pesa aliyapokea kama mwenye kiti au mwenye chadema na hayakujulikana yalokokwenda. Lakini mbaya zaidi hakuweza kuyakanusha bali alikazana kusema hayaongelei yuko bize na uchaguzi.
Tulimsihi kuwa kuyaongelea ni sehemu ya uchaguzi maana CHADEMA ikipakwa matope basi matokeo yatajitokeza kwenye kura za rais. hakuwahi kukana na hana mpango wa kukana na kwa bahati nzuri anafikiri waTz wamesahau.

Uchaguzi umemalizika Serikali imeingia madarakani. Nguvu ya kupinga matokeo ilikuwa ndogo. Sijui kama anajua kwa nini ni ndogo. 2010 kila kona matokeo ya uchaguzi ya Rais yalinung'unikiwa. Kwa sasa siyo. Wenye akili walielewa.
Baada ya hapo Serikali imeingia madarakani. Bila kujadili kilichofanywa na serikali bali watu wanasemaje ndani na nje ya nchi kila mtu anaona. Tuangalie link hii (https://www.facebook.com/eugeneanthony.mwakapugi/videos/971705296246530/).
Sasa hebu tuangalie CHADEMA ile kabla ya kukatisha daraja na hii au tukampime mwenyekiti wake.
Mbowe ni mfanya biashara. waathirika wkubwa wa uongozi wa Magufuli ni wakwepa kulipa kodi. Na wakwepaji wakubwa ni wafanya biashara. Je mbowe ni muathirika wa utawala wa Magufuli au ni muathirika mtarajiwa? Tunahitaji kulijua hilo kwa sababu kuhakikisha kuwa makonteina yaliyobanwa hakukuwa na yake 500 hakuna anayeweza kujua.
Kama ndivyo tukianzia CHADEMA YA toka kukatisha daraja na kauli za mbowe tunajiuliza swali: Toka kukatisha daraja nililolieleza tunaiona CHADEMA au tunamuona Mbowe? Huenda chadema iliisha kabla ya uteuzi wa mgombea urais na sasa tunashughulika na Mbowe. Au labda CHADEMA haikuwahi kuwapo siku zote tulikuwa na Mbowe.
Nakumbuka tulivyomshabulia Zitto. Huenda alikuwa ameona (wakati ule) tunachokiona (sasa).
naihurumia Tanzania.
--------------------------------------------
On Wed, 3/9/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Hakika Chadema ya sasa siyo ile
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, March 9, 2016, 12:30 PM

WIKI
iliyopita, gazeti moja la
kila siku lilimkariri Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe, akilalamikia kampeni inayofanywa na Serikali ya Awamu
ya Tano ya
kusimamisha na kufukuza watumishi wa umma wanaotuhumiwa
kuhusika katika
ubadhirifu, wizi, uzembe na njama za kuhujumu
mapato.
Katika
habari hiyo, nilisoma hadi mwisho nikagundua mambo mawili
anayoelezea
Mbowe kuhusu kampeni hiyo iliyopewa jina la utumbuaji
majipu. Mosi, ni
madai kwamba ufukuzaji wa watumishi wa umma unafanywa bila
kufuata
utaratibu na pili; kama alinukuliwa sawasawa, ni madai
kwamba watendaji
hao wa serikali 'wanatumbuliwa' bila makosa yao kuwekwa
hadharani! Mbowe
ambaye aliyasema hayo katika ibada maalumu ya uzinduzi wa
ukarabati wa
Kanisa la Kiinjili la Kiliutheri Tanzania (KKKT), Usharika
wa Nshara
wilayani Hai, aliwataka viongozi wa dini kukemea mwenendo
huo.

Katika
habari hiyo, Mbowe pia alizungumzia mgogoro wa Zanzibar
ambao si
maudhui ya makala haya, lakini katika kipengele hicho cha
kukemea
utumbuaji majipu, kiliniacha nikiwa na maswali mengi. Mbali
na maswali
niliyojiuliza, nilianza kuthibitisha kile ambacho kimekuwa
kikidaiwa na
baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kwamba hii ya
sasa si Chadema
ya zama zile. Nitafafanua.
Swali la
kwanza nililojiuliza ni kama
kweli utumbuaji unafanyika kinyume cha sheria na taratibu
kama
alivyodai Mbowe. Kwa uelewa wangu ni kwamba wengi wa hawa
wanaokumbwa na
kampeni hii inayoungwa mkono na Watanzania wengi wakiwemo
wanachama wa
Chadema, ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho mkoani
Rukwa, Zeno
Nkoswe, wanasimamishwa kazi kupisha uchunguzi.
Ni kwa mantiki
hiyo, baada ya uchunguzi, mwajiri ambaye ni serikali,
ataamua,
kuwarudisha kazini kama hawana makosa, kuwafukuza kazi au
kuwafikisha
kortini. Ninachoelewa pia ni kwamba wale wanaofikishwa
mahakamani moja
kwa moja ni ambao tuhuma zao ziko wazi na ushahidi mwingi
upo.
Halikadhalika, sijasikia mtendaji yeyote wa sekta ya umma
ambaye
amesimamishwa, kufukuzwa au kufikishwa mahakamani bila
tuhuma zake
kuwekwa hadharani.
Nikirudi kwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani
Rukwa, Nkoswe, aliwahi kukaririwa na gazeti hili akisema:
"Serikali hii
ya Awamu ya Tano, binafsi nimefurahishwa nayo sana kwa
sababu uozo
katika sekta ya umma ambao tumekuwa tukiupigia kelele, sio
viongozi wa
upinzani pekee, bali hata wananchi wa kawaida, sasa tunaona
dhahiri
ukifanyiwa kazi."
Akaendelea kusema: "Hakika Rais John Magufuli
akifanikiwa vyema, nchi yetu itakuwa ya heshima kubwa
duniani na sisi
wananchi tutaona manufaa makubwa." Na huu ndio ukweli
dhahiri ambao
ninaamini hata Mbowe anao moyoni mwake. Chadema niliyoijua
Kabla hata
sijasoma habari yenyewe, nilijiuliza maswali mengi
sana.
Je, Mbowe
anayetajwa hapa ni yuleyule Mbowe wa Chadema iliyokuwa
inalalamikia sana
kukithiri kwa 'majipu' huku nyuma hadi siku chache
kabla ya nchi kuanza
harakati za uchaguzi mkuu mwaka jana?
Kila nilipokuwa nabahatika
kushiriki vikao vya Bunge, sehemu kubwa ya michango ya
wabunge wa
Chadema ilikuwa ni kulalamikia namna nchi yetu inavyoporwa
na watu
wanaotumia madaraka kwa maslahi binafsi. Ingawa kuna wakati
wasemaji wa
Chadema walikuwa wakilalamika kwa hisia tu, wakati mwingine
walikuwa
wakija na hoja zenye mashiko. Chadema 'ile' haikuwa
inahimiza hatua
kuchukuliwa kwa wabadhirifu na mafisadi wa fedha za umma
pekee, bali pia
ilihimiza uwajibikaji na watendaji katika sekta ya umma
kuacha kufanya
kazi kwa mazoea.
Ili kuunga
mkono hoja zangu, napenda kutumia
maneno ya mwana-Chadema mmoja tu, Halima Mdee, Mwenyekiti wa
Baraza la
Wanawake wa Chadema (Bawacha). Ipo video yake moja unaweza
kuisikiliza
katika youtube (www.youtube.
com/watch?v=8tkj) ambapo Halima 'anatumbua' majipu,
kinyume kabisa na
kauli hizi za Mbowe.
Baadhi ya
maneno ya Mwenyekiti huyo wa Bawacha
alipokuwa anachangia katika moja ya bajeti zilizopita ni
haya: "Tokea
tumekuja bungeni kwa mara ya kwanza, linapokuja suala la
matumizi ya
fedha za umma, linapokuja sula la mikataba ni wizi
mtupu."
Katika
video hiyo Mdee analalamikia pia hasara iliyosababisha
Tanzania kudaiwa
dola za Marekani milioni 50, sawa na Sh bilioni 90
zilizotokana na
mkataba mbovu wa Shirika la Ndege ATCL baada ya kutumia
ndege kwa muda
wa miezi sita tu. Anasema fedha hizo ni sawa na bajeti ya
maendeleo ya
miaka miwili ya wizara ya kilimo, sekta inayoajiri
Watanzania wengi.

Lakini
kubwa analolilalamikia ni serikali kuongelea hoja hiyo kwa
lugha
nyepesi bila kuonesha kuwawajibisha walioipa serikali
hasara kubwa kama
hiyo. Hapo nimechukua mfano wa msemaji mmoja tu wa Chadema
'ile'
niliyokuwa ninaijua, ambayo takribani wasemaji wake wengi
akiwemo Mbowe
mwenyewe walikuwa ni kulalamikia tu namna serikali
isivyochukua hatua
kali, za haraka na madhubuti kwa watumishi wa umma ambao ni
wabadhirifu,
wezi na wazembe.
Ndio maana
napata shida kuamini kama haya ya
wakati huo yalikuwa maigizo au nini? Ninavyoamini mimi,
baadhi ya hatua
zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano sasa ni
kufanyia kazi
ushauri wa muda mrefu uliokuwa unatolewa na upinzani,
hususan Chadema,
kuhusu tatizo la 'majipu' katika sekta ya umma. Na
pengine, hata takwimu
walizokuwa wanazitoa au ushahidi wao sasa unafanyiwa
kazi.
Kwa
mantiki hiyo, wengi tulitazamia kuona chama hicho
kinachoongozwa na
Mbowe, kikipongeza baadhi ya mambo kama alivyosema
Mwenyekiti wake wa
Rukwa, Nkoswe. Chadema ilipoamua kumchukua Waziri Mkuu
aliyejiuzulu kwa
tuhuma za kushiriki 'dili' chafu la kuleta kampuni ya
kitapeli ya kufua
umeme wa dharura ya Richmond, Edward Lowassa, wengi
walitabiri kwamba
mwisho wake wa kupambana na maovu katika sekta ya umma
umefika kikomo.

Ufuatiliaji
wa kampeni za chama hicho wakati nchi inaelekea kwenye
uchaguzi mkuu nao ulionesha kwamba Chadema ilikuwa imekosa
kabisa uwezo
(moral authority) wa kuzungumzia ufisadi. Huku kukiwa na
madai kwamba
sasa chama hicho ndicho kimbilio la wafanyabiashara ambao
wana 'walakini
nyingi' katika biashara zao ikiwemo kukwepa kodi, haya
aliyoyasema
Mbowe yanazidi kutusadikisha sisi wengine ambao tulitaka
tusiamini,
kwamba hii ya sasa siyo Chadema ile ya akina Zitto Kabwe,
Hayati Chacha
Wangwe na Dk Wilbrod Slaa.
Kazi ya
upinzani ni kupinga tu? Mimi
ninaamini kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inakubali
kukosolewa kwani
inaongozwa na wanadamu, si malaika. Kama ndivyo wanaweza
kufanya makosa.
Kwa mantiki hiyo, watu kama Mbowe wana nafasi kubwa ya
kuikosoa lakini
kwa njia na lugha za kiungwana. Kosa ambalo limekuwa
likifanywa na
wapinzani siku zote, na hilo kuna siku nitaliandikia makala
kwa urefu,
ni kutojua namna nzuri ya kumkosoa kiongozi.
Mafundisho
ya Dini
ya Kiislamu yanasema kwamba kiongozi yeyote wa nchi,
haombewi dua mbaya,
bali nzuri, ili Mwenyezi Mungu ampe uwezo na moyo wa huruma
kwa
wananchi wake. Kadhalika, mafundisho yanasema kiongozi wa
umma, hata
kama ni dhalimu (fisadi), hakosolewi kwa njia ya dharau na
kuvunjiwa
heshima. Ukitaka kumkosoa kiongozi wa umma, unampa heshima
yake kwanza
kisha unatafuta mazuri yake na kuyasifia na kisha
unazungumzia mambo
ambayo unadhani anapaswa kuyafanyia kazi huku ukitumia lugha
ya
kiungwana.
Tuyaache
hayo. Mpaka sasa, watumishi zaidi ya 160 wa
sekta ya umma wamesimamishwa kazi au kufukuzwa huku baadhi
yao
wakifikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi na uwajibakaji
mbovu, ule
uliokuwa ukilalamikiwa na Chadema. Kwa mafundisho hayo ya
dini na kwa
akili tu ya kawaida, nilitegemea Mbowe angeanza kusifia
mazuri
yaliyofanywa katika kipindi kifupi sana cha uongozi wa
Serikali ya Awamu
ya Tano, ambayo ni mengi, kama alivyosema Nkoswe.
Kisha, kama
yapo ya kukosoa, angeyasema ingawa si hayo ya utumbuaji
majipu kwa
sababu si kweli alichokisema labda kama ni tukio moja au
mawili kati ya
majipu mengi yaliyotumbuliwa na yanayoendelea kutumbuliwa.
Je, ni kweli,
hata hatua ya kutoa elimu bure Mbowe haoni? Kubana matumizi

kunakofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, kuongeza mapato
ya serikali
yanayokusanywa na mengine lukuki hayaingii kwenye akili ya
Mbowe?



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment