Saturday, 5 March 2016

Re: [wanabidii] DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUFUNGWA CHUMBA CHA UPASUAJI CHA HOSPITALI YA SANITAS YA MIKOCHENI

Yes Kim-Zamani hata kama dawa hospitali hakuna anakwambia doctor au nurse nenda hapa au pale ukanunue dawa aliyokuandikia lete hapa hakuna au zimekwisha. Mgonjwa anatibiwa na unakuta kila mgongwa ana bahasha lake la dawa alilonunua nurse kaliweka separate na mengine. Hakuna pampas unakwenda dukani nje unanunua unapeleka kwani private hospital huwezi gharama zake ambako pamsai utazilipia ktk bili yako ya gharama za juu. Unaridhika unampa kadogo kitu doctor wa GVT hospital kama asante.

Sasa hii fukuza na funga hapa na pale, fukuza nurse, daktari waliobaki-watakuangalia pale unakufa- Msubiri Mangufuli na Kingwalala waje!! Cheza na mbongo wewe!

Narudia-usifunge Duka la Dawa nje ya zahanati au huduma ya afya yoyote kabla hujafungua lako ndani ya huduma hiyo na kuhakikisha Health Kit ya huduma husika ina dawa za kutosha. Wakitoka nje wanakuta dawa ghali kuliko duka la ndani ya facility hiyo ya GVT hawanunui nje bali ndani. Daktari atafanya uwekezaji upi kama sio ktk sekta yake aliyosomea?_Duka la Dawa. kama hana hilo-ataondoka hapo mapema kwenda kutoa huduma private hospital ili agange njaa. Foleni ndefu yupo daktari mmoja tu wengine wamesepa kuongeza mshahara.

Kama maduka ya dawa yamezingatia sheria na kupata leseni na wananunua dawa kiuhalali hata liwe la daktari liache!. Daktari ya hospitali, health Centre, Dispensary anajua ni magonjwa gani yapo highly prevalent hapo na muda gani yanatokea. Hivyo ananunua dawa anazoona zitahitajika eneo hilo. Health Kit ya Zahanati kwa mfano inategemea kaya ngapi zimenunua Health Card ya SHS 10,000 kwa mwaka familia ya watu sita na health Card ya mwanafunzi shule watoto 5 wanaweza kujumuishwa shs elfu 2 kila mmoja matibabu ya mwaka kwa kadi moja ya elfu 10.

Binafsi-nimejitolea sana kutibu wanafunzi kwa pesa zangu kila nipitapo vijijini kwa research na ninaposimamia miradi ya maendeleo vijijini ambayo huhusisha pia school health. Dawa nyingine za minyoo iliyomfanya mtoto awe na matezi nilizinunua DSM kwa ajili ya mwanafunzi aliyepo Milola kilometa 60 kutoka Lindi mjini. Haikupatikana Lindi. Kuzisafirisha vijijini kwa bus la abiria. Vifaa vya zahanati kuvinunua Dar maduka ya medical equipment authorized by the Ministry na kusafirisha Zahanati ninakosimamia mradi husika unaogopa vikipitisha Wilayani vinaweza visifike vinakotakiwa lakini unamuarifu DMO kuwa umepeleka hiki na kile kama mlivyokubaliana wakavikague vimeshafika. Hiyo ni Health Centre au Zahanati ya Serikali.

Mzazi anashindwa hata kumpa mtoto hela akatibiwe zahanati lakini anakunywa pombe daily hanunui health card. Kama kaya ni elfu 2 waliolippia kadi ya afya ni kaya asilimia 2 unafikiri Health Kit ya Zahanati itapatikana vipi? Wakati mwingine inakwenda sio kit husika kwa eneo hilo. Mpaka irudishwe inayohusika hapo na madawa hitajika ifike-hawajafa tu kama hakuna duka la dawa la binafasi? Hii funga funga mimi inanikera labda kwa mtu ambae hana uelewa na sekta hii ataona ile ingia funga na toka nje funga maduka ya dawa ni kitu chema. Hata vyuo vya elimu ya juu wameruhusu restaurants za watu binafsi na wanauza chakula sio bure tena kama tuposoma sisi cafeteria unapata nusu kuku unakula na kutupa. Sasa lipia kula ule utupe kwa matakwa yako. Huwezi ukafunga tu biashara hapo campus au nje ya shule wakati huduma ya serikali ya chuo kwa sasa inaendeshwa na mkandarasi sio dezo tena. Tujiangalie na maamuzi ya Hapa Kazi tu yanavyofasiriwa vibaya bila ya kuzingatia principles of good democratic governance, effective manpower management and effective institutional management.

Kama Kawa

--------------------------------------------
On Fri, 4/3/16, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUFUNGWA CHUMBA CHA UPASUAJI CHA HOSPITALI YA SANITAS YA MIKOCHENI
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, 4 March, 2016, 22:51

MAMA Kiwasila ametoa
mwangaza,

serikali isishie kuwa wakali kwa watumishi wa afya haswa
huduma za afya, tuangalie takwimu za vifo na huduma
nyinginezo katika hospitali zetu!! 

Ndio namna ya kugundua kama tunasonga mbele, zikizidi
tunarudi kurekebisha jambo, zikipungua tunashukuru
tumeweza!!  Ila kugawa mambo ya msingi kama dawa n.k. ni
jukumu la serikali.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment