Monday, 9 July 2012

[wanabidii] TAARIFA KUHUSU MADAKTARI WALIO KATIKA MAFUNZO KWA VITENDO

TAARIFA KUHUSU MADAKTARI WALIO KATIKA MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNS)

Wizara imepokea malalamiko kuwa kati ya tarehe 23 juni, 2012 hadi
tarehe 29 juni, 2012, Madaktari walio katika mafunzo kwa vitendo 372
kati ya 763 katika hospitali mbalimbali nchini, waligoma kutoa huduma
kwa wagonjwa ikiwa ni wajibu wao kama madaktari.Kitendo hicho sio tu
kilihatarisha usalama wa wagonjwa waliohitaji huduma za matibabu
katika hospitali hizo, bali kilikuwa ni ukiukwaji wa maadili ya
taaluma.

Madaktari hao waliogoma walirejeshwa Wizarani kwa barua kutoka kwenye
mamlaka za hospitali walikokuwa wakifanyia mafunzo kwa vitendo.

Kwa kuwa Wizara ndio yenye dhamana ya usimamizi wa huduma za afya
nchini, na kwa kuwa madaktari hao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari
Tanganyika, hivyo Wizara imewasilisha malalamiko haya huko ili Baraza
liwachunguze na kuamua hatma yao kitaaluma.

Kwa hivi sasa madaktari hao hawako maeneo yao ya kazi, na suala hili
limepelekwa Baraza la Madaktari kwa uchunguzi kuhusu kitendo
walichokifanya, hivyo Wizara inasitisha posho zao kuanzia Tarehe 1
Julai, 2012 hadi hapo itakapopata taarifa ya uchunguzi wa Baraza la
Madaktari.

Madaktari wengine waliogoma, taratibu za kiutumishi zitachukuliwa na
mamlaka ya ajira zao kwa mujibu wa sheria na taratibu husika.

Regina L. Kikuli
KAIMU KATIBU MKUU
09.10.2012


On Jul 9, 5:22 pm, cathy sungura <cathysung...@yahoo.com> wrote:
>  INTERNS-taarifa kkm.doc
> 66KViewDownload

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment