Mim ni mkazi wa Mbezi Makabe. naandika haya kwa uchungu sana jinsi barabara yetu ilivyo mbovu na hakuna mtu hata mmoja anaiangalia. Barabara ya kwenda Mbezi Makabe imekuwa mbovu mbovu. Haipitiki kabisa. Hii barabara inayoanzia Kituo cha zamani cha daladala Mbezi Mwisho kwenda Makabe-Msakuzi.wananchi wanataabika. Wanakaaa zaidi ya masaa 3 barabaran kusubiri daladala. Daladala zimekimbia kutokana na ubovu wa barabara. Magari ya watu binafsi nayo yanapata shida sana. Maji tunayonunua kwenye malori nayo yamepanda bei. Tunauziwa lita 1000 sh. 15 hadi elfu 20.
Mbunge tuliempa kura nyingi na madiwani wote hatuwaoni jimboniMh. Mnyika wananchi walikuchagua wanapata shida.
Tunakuomba angalau lipitishwe greda tuu. Wananchi wapo tayari kuchangia.
Hali ya barabara ni Mbaya ni Mbaya ni Mbaya.
Huduma za kijamii zimepanda. wananchi wamekata tamaaa.
Tafadhali Mh Mnyika. Hii la barabara na Maji Makabe ni jipu.
Rudi jimboni saidia wananchi
jf
0 comments:
Post a Comment