Ardhi ya hiyo ya Mh Sumaye hapana shaka aliichukua wakati akiwa PMO akaweka mifugo miaka ile ya yeye kuwa mkubwa wa nchi. Tukiwasikia watu wakisema wakimsindikiza shamba huko kwenye mifugo yake-akifika huko alikuwa hasikii harufu mbaya ya kinyesi! Yeye ni ndani ya sisi la ng'ombe kinyesi kukikanyaga na boots zimebeba mzigo wa tope la kinyesi akifurahia kuziangalia ng'ombe zake kwa tabasamu na kukaa harufu kwake manukato! Sasa yamegeuka tena. Ardhi zao wameuza wanaitaka hiyo?
Kisheria, Kijiji kinaruhusiwa kutoa mwisho ekari 50. Hao wananchi wavamizi wanatumia udhaifu wa serikali kuvamia mashamba ya watu. Kuna wananchi walikuwa na customatry land sio vijijini tu hata vijiji vya mjini dar na miji mingine mikubwa na midogo TZ. Hawa wameuza. Msewe, Goba, Changanyikeni, Tabata, salasala, mkuranga, Mbezi, Kimara, Kimara Bonyokwa, Tegeta, Bunju etc. Wameuza na sasa baadhi wanakaa mashimo ya kokoto na mchanga wamevamia na kutesa watoto. Wamevamia Wazo hill kiwanda kikaingia matatizo ikaamua kuwapa maeneo na watafanya tena land survey kufuta mipaka ya ukoloni. Lakini waliojenga vibanda kwa kuvamia-wameuza. wamevamia maeneo ya kuchimba kokoto JKT na JWTZ Tegeta Mbuyuni-Kunduchi. Subiri tingatinga la JWTZ litakapotembea na kubomoa majumba mazuri. Taarifa za kuhama ni za karne hawajahama wala kubomoa. Maeneo ya kijiji cha Salasala ya kujenga Ofisi ya Kijiji na Shule, zahanati viongozi wameuza kuna yard ya magari etc. Ofisi za Kata Mzee Aziz mwanzilishi mmojawapo wa Chama cha TANU kawapa ofisi ya Kata. Ofisi ta Mtaa-imejengwa kwa uvamiazi wa eneo la Benaco ambako kumevamiwa na kujengwa kote mpaka majumba na shule ya Msingi. Account ay Kijiji cha salasala-haijulikani imeishiaje baada ya Vijiji kuwa Mtaa. Maeneo ya kuchimba mawe na kokoto kabla hayajafanyiwa quarry recovery cama sheria inavyotaka-yameshavamiwa na watu kujenga na maduka mpaka maghorofa yanazidi kuongezeka. Waliouza mashamba Salasala-wamejenga mashimoni kunacojaa maji. Maekari mengi ya customary land wameuza na walichofanyia hela-ni cha kuuliza. Waliojenga kando ya mto Tegeta daima majumba/vibanda kuporomoka. Ndio hawa eti wa kima cha chini ambao wanauza ardhi kwa ammilioni na kuishia ndani ya mashimo wanayochimba kokoto. wakivamia shamba la Sumae au wazo hill na kumegewa vipande wajenge-Wanauza tena!
Kuna haja hata Katiba ya Nchi kubadilika kuondoa ule usemi kwamba mtu anaruhusiwa kwenad kokote kule atakako (Bila ya kuvunja sheria). Sheria inavunjwa mara zote. hata waliopewa mashamba ya katani, pamba etc ya mamlaka mbali mbali kumegewa ekari 400+ wameuza kuna lodges, bar kila kona vijijini wapo wapo barabarani kwenye way-leave. Katiba iseme unaruhusiwa kwenda popote mradi tu uwe na right of occupancy ya customary au statutory land rights. Haraka Waziri wa ardhi afanikishe Land Use Planning na kutoa Hati Miliki (Isiyohamishika mpaka kwa kibali cha Waziri) kwa kila owner. Hii itapunguza-uuzaji ardhi hovyo, uvamizi ardhi, uhamaji hamaji unaoathiri maendeleo, afya na elimu kwa watoto na kuathiri uchumi wa kaya na nchi; itasaidia uwekezaji-wawekezaji hawatoogopa kuja bongoland kwa kuogopa kuvamiwa mara kwa mara ktk maeneo yao na kuharimiwa mali zao kwa kubomolewa, kuchomwa moto na uharibifu mwingine. Itakomesha uvamizi wa vyanzo vya maji, barabara, misitu hifadhi na mbuga za wanyamapori. Marufuku pia kutoa leseni za mbao, mikaa bila ya muhusika ,kuonyesha kuwa-ana pori la miti alilopanda kufanya biashara za mazao ya miti.
Bila ya utekelezaji wa sheria kali-mtanzania atauza ardhi daima na kuhamahama kisha kulaumu serikali na wawekezaji hasa wa nchi za nje na kuvamia ardhi ambao baadhi wameipata kihalali pamoja na kuwa ni kubwa. Mtu anatoka Manyara, Monduli anahamia na mifugo maelfu Ramsar Site ya Kilombero halafu anasema-anaonewa na Ramsar! Toka lini ardhi chepechepe kwa Mpogoro kulikuwa na maelfu ya mifugo kama sio samaki Kitoga, kambale mitoni na mfugo mkuu ni KUKU?! Ubwabwa ukiitwa UGALI na ugali wameujua juzi tu? Nyama ikiliwa ni ya ng'ombe mwitu/Mbogoi, Kibogo, Ngiri!! Mtu akiona mbogo mate yanamtoka. Bora apigwe pembe na mbogo kuliko kukosa nyama yake. Leo mifugo ndani na mabonde kibao, kulishia mashamba, uvamizi mbuga za hifadhi kisha-Ramsar inaonea wafugaji? Tuyaangalie vema haya kama hatujatetea uharibifu wa mazingira yetu tukajimaliza. Serikali iangalie pia na kulazimisha kilimo na ufugaji endelevu. iwe marufuku mtu kuwa na ng'ombe 1000 (livestock units) katika ekari 5 ambapo alitakiwa awe na ekari 5,000 kama yupo semi-arid area. Huyo ni mmoja bado kijiji kizima kwa kaya zote. Hii husababisha uharibifu wa mazingira na watu kuhamahama kutesa wenzao huko wanakokwenda-source ya vita kuu ijayo kuliko vita ambayo watu tunaona itatokana na tofauti za kisiasa-No. Vita itatokana na tatizo la uvamizi wa ardhi, uharibifu wa mazao kati ya wakulima na wafugaji. Hii italeta mapigano na mauaji ya mpaka kikabila. Ya Kisiasa-mbona majeshi yanaweza kuwabeba wa upinzani na chama tawala wakawapa mkong'oto safi wakawasepesha. Wananchi hawatapigana ila watawadharau kuona kuwa-wanapata posho, kula hela zetu na kutuletea upuuzi-"Wapigwe Tu!!" Ila haya ya kuvamia shamba la mtu-kupigwa; kuingiza mifugo kulisha mazao maekari, kuharibu vyanzo vya maji kujaza kinyesi na uchafu mwingine na kupiga wamiliki bakora, mapanga, mikuki, kukata miguu mifugo-hii ni vita mbaya ambayo italeta sio tu economic but triobal/ethnic conflicts ambayo ni another Rwanda genocide!! ambapo itakuwa TZ genocide!!
Babu zetu sisi wengine walimiliki ardhi kubwa ambayo ni sawa na ukubwa wa kijiji au kitongoji fulani kwa sasa. Wazee hawa baadhi walitoa maekari kuvipa vijiji vijenge huduma za jamii. Wakatubakizia nyingi tu. Sisi kiukoo tumeuza na sasa hatuna ardhi kabisa!
Wakifuatiliwa hao waliovamia shamba la Sumaye-ni opportunists tu, madalali, wameuza maeneo yao Bunju etc, anavamia anajenga kajibanda-atauza na kwenda kuvamia kwingine. Sitetei wakubwa kujichukulia mashamba/ardhi wakiwa na madaraka kwa manufaa binafsi, lakini wapo wabongo wanaouza maeneo yao kiupumbavu halafu kuvamia ya wenzao na ya serikali. Tusitetee ujinga huu.
Na sasa ni vunja vunja kila eneo lililopimwa DSM na miji mingine ambapo wakazi na wamiliki plots wameziba barabara (feeder roads), viwanja vya michezo au public open spaces; mitoni, baharini, kujenga viosk nje ya ukuta ambavyo vinapunguza nafasi ya barabara/mapito. Beba magari yote unayoyakuwa wamepaki juu ya barabara ya mapito kwa mguu, juu ya concrete slides za stormwater drainage system na kuzibomoa; beba mbao na malori wanayopark kando ya barabara kuuza biashara ya mbao na beba miavuri yote inayoziba footpaths kando ya barabara kuzuia watu wasipite. Tumia JWTZ kuwazoazoa ili kujenga nidhamu kwani mgambo wa jiji hawawezi. hawa wanaishi na jamii ambayo inawalipizia kisasi. Sasa-hapa kazi tu na jeshi ili tujenge nidhamu inayotakiwa na sheria za nchi.
Kama kawa
--------------------------------------------
On Sat, 30/1/16, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Sumaye aiangukia Serikali wananchi kuvamia shamba lake la ekari 33 Mabwepande jijini Dar es salaam
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, 30 January, 2016, 22:41
Ni zile ambazo serikal iligawia watu
ambao inabomoa majumba yao????? Kama ni ndiyo siwezi
kushangaa kuwa ni mali ya Sumaye.
--------------------------------------------
On Sat, 1/30/16, 'lang'itomoni lokomoi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Subject: [wanabidii] Sumaye aiangukia Serikali wananchi
kuvamia shamba lake la ekari 33 Mabwepande jijini Dar es
salaam
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, January 30, 2016, 12:54 PM
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye,ameiangukia
serikali na kuomba
msaada baada ya wananchi kuchukua sheria mkononi na
kuvamia
eneo lake
la ekari 33 lililopo Mabwepande katika Manispaa ya
Kinondoni
nje kidogo
ya jiji la Dar es salaam. Serikali imemuahikikishia Mhe.
Sumaye kuwa
haina mpango wa kumkandamiza mtu mnyonge wala tajiri hivyo
itahakikiha
inatoa haki kwa kila mmoja baada ya wiki mbili kwa kua
imesikiliza pande
zote mbili katika mgogoro huo.
Akizungumza katika kikao
cha
pamoja kati ya wananchi wa kitongoji cha Kimondo mtaa wa
mji
mpya Kata
ya Mabwepande na Mhe.Sumaye Dar es Salaam leo asubuhi,
Mkuu
waWilaya ya
Kinondoni Paul Makonda alisema ili kumaliza mgogoro huo
ambao Waziri
Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ameiomba serikali kuingilia
kati ni lazima
busara kutumika. Alizitaka pande hizo mbili kuiachia
serikali kwa wiki
mbili ili kutafuta njia bora ya kumaliza tatizo hilo huku
wananchi
wakitakiwa kuache kuendelea na ujenzi na kugaiana maeneo
katika shamba
hilo.
"Serikali ya Rais
Magufuli ni sikivu na ndio maana ilikuwa
tayari kumsikiliza Waziri Mkuu wetu Mstaafu Sumaye na
kusikiliza
wananchi ili kutenda haki tunatambua migogoro ya ardhi
ilivyokuwa na
athari kwa jamii hatuna mpango wa kumkandamiza tajiri wala
mnyonge,"alisema. Alisema katika eneo hilo anajua jinsi
wananchi
walivyotumia nguvu katika kuwekeza ujenzi na rasilimali
zao
lakini kwa
sasa wasitishe shughuli hizo na kuendelea kugawana maeneo
na
Sumaye pia
kuacha uwekezaji ili kutafuta suluhu.
Zipo njia nyingi
tutazitumia kumaliza mgogoro huu ikiwemo kufuata sheria
kwa
kuangalia
iwapo mzee wetu alikiuka taratibu kweli za kumiliki ardhi
kama
ilivyodaiwa na wananchi hatua gani serikali
tuchukue,"alisema. Alisema
pia wanaweza kukaa na Sumaye na kuzungumza naye ili
kukubali
hasara kwa
kutoa eneo kidogo na kuwapatia wananchi hao ambao hawana
makazi au
Manispaa kutafuta eneo mbadala na kuwauzia kwa bei
nafuu.
Alizitaka pande hizo mbili
kutambua umuhimu wa kulinda amani katika
mgogoro huo kwa changamoto zilizopo kutatuliwa bila kutumia
nguvu.Makonda pia aliagiza serikali ya kijiji kufanya
utambuzi wa
wananchi hao wenye makazi katika shamba la Sumaye. Awali
katika mkutano
huo Mhe. Sumaye alimueleza Mhe. Makonda jinsi serikali
ilivyo na kazi
ngumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi na kuomba kutumia
busara zake
kumpatia eneo hilo analomiliki kihalali.
"Mheshimiwa Mkuu wa
Wilaya kama nilivyokueleza awali serikali yetu inakazi
ngumu
sana hasa
kutokana na viongozi wa chini kutokuwa wasikivu na wakweli
eneo hili
namiliki kihalali nina nyaraka zote na ninalipia kila
mwaka
na nilikuwa
katika mpango wa kutafuta wafadhili ili kuliendeleza kwa
kujenga Chuo
Kikuu,"alisema. Alisema yeye na familia yake waliuziwa
eneo hilo toka
mwaka 1997 na anaamini serikali itatenda haki.
Diwani wa kata
hiyo Suzan Masawe alisema anauthibitisho kuwa eneo hilo
lilikuwa pori na
Sumaye alilitelekeza kwa muda mrefu na kusababisha
uhalifu
ikiwemo
wanawake kubakwa,mali za wizi kufichwa na uhalifu
mbalimbali. Alisema
kutokana na hatua hiyo walimtafuta Sumaye lakini hakuwa na
ushirikiano
kwakuwa hata alipofanya uwekezaji kwa kuchimba kisima cha
maji alikataa
kuwapa wananchi .
Suzan alisema kutokana na hasira za
wananchi
hao kwa kukosa huduma za kijamii kwa muda mrefu ikiwemo
eneo
hilo
kutokuwa na shule,Zahanati wala kituo cha polisi waliamua
kuvamia na
kujigaia maeneo. Mmoja wa wananchi hao Athuman Mnubi
alikiri
kweli
hawana umiliki halali wa eneo hilo na katika hatua ya
kutafuta makazi
walivamia msitu huo uliotelekezwa na Sumaye.
Alisema wanaamini
kutokana na ahadi ya serikali ya Rais Magufuli katika
kupora
maeneo
yaliyotelekezwa na wawekezaji watasaidiwa. WAKATI huo huo
Makonda
alisimamisha na kukamata baadhi ya malori ya kokoto na
mchanga,
wafanyakazi na Mwekezaji wa kigeni kutoka India Sules
Waljan
wanaochimba
mchanga,kokoto na kifusi katika eneo la Mabwepande.
Hatua
hiyo imekuja
baada ya kuona uharibifu mkubwa wa mazingira na
alipowahoji
wafanyakazi
na Mwekezaji huyo kama wanavibali walisema hawana.
Makonda
amewafikisha watuhumiwa hao kituo cha polisi cha Wazo Hill
ili kutoa
maelezo ya kina na kusema kuwa serikali inatumia gharama
kubwa kwa
uhalibifu huo wa mazingira ambao pia unafanywa katika
vyanzo
vya maji na
matengenezo ya madaraja yanayoharibiwa ni
makubwa.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment