Ni zile ambazo serikal iligawia watu ambao inabomoa majumba yao????? Kama ni ndiyo siwezi kushangaa kuwa ni mali ya Sumaye.
--------------------------------------------
On Sat, 1/30/16, 'lang'itomoni lokomoi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Sumaye aiangukia Serikali wananchi kuvamia shamba lake la ekari 33 Mabwepande jijini Dar es salaam
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, January 30, 2016, 12:54 PM
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye,ameiangukia
serikali na kuomba
msaada baada ya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuvamia
eneo lake
la ekari 33 lililopo Mabwepande katika Manispaa ya Kinondoni
nje kidogo
ya jiji la Dar es salaam. Serikali imemuahikikishia Mhe.
Sumaye kuwa
haina mpango wa kumkandamiza mtu mnyonge wala tajiri hivyo
itahakikiha
inatoa haki kwa kila mmoja baada ya wiki mbili kwa kua
imesikiliza pande
zote mbili katika mgogoro huo.
Akizungumza katika kikao
cha
pamoja kati ya wananchi wa kitongoji cha Kimondo mtaa wa mji
mpya Kata
ya Mabwepande na Mhe.Sumaye Dar es Salaam leo asubuhi, Mkuu
waWilaya ya
Kinondoni Paul Makonda alisema ili kumaliza mgogoro huo
ambao Waziri
Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ameiomba serikali kuingilia
kati ni lazima
busara kutumika. Alizitaka pande hizo mbili kuiachia
serikali kwa wiki
mbili ili kutafuta njia bora ya kumaliza tatizo hilo huku
wananchi
wakitakiwa kuache kuendelea na ujenzi na kugaiana maeneo
katika shamba
hilo.
"Serikali ya Rais
Magufuli ni sikivu na ndio maana ilikuwa
tayari kumsikiliza Waziri Mkuu wetu Mstaafu Sumaye na
kusikiliza
wananchi ili kutenda haki tunatambua migogoro ya ardhi
ilivyokuwa na
athari kwa jamii hatuna mpango wa kumkandamiza tajiri wala
mnyonge,"alisema. Alisema katika eneo hilo anajua jinsi
wananchi
walivyotumia nguvu katika kuwekeza ujenzi na rasilimali zao
lakini kwa
sasa wasitishe shughuli hizo na kuendelea kugawana maeneo na
Sumaye pia
kuacha uwekezaji ili kutafuta suluhu.
Zipo njia nyingi
tutazitumia kumaliza mgogoro huu ikiwemo kufuata sheria kwa
kuangalia
iwapo mzee wetu alikiuka taratibu kweli za kumiliki ardhi
kama
ilivyodaiwa na wananchi hatua gani serikali
tuchukue,"alisema. Alisema
pia wanaweza kukaa na Sumaye na kuzungumza naye ili kukubali
hasara kwa
kutoa eneo kidogo na kuwapatia wananchi hao ambao hawana
makazi au
Manispaa kutafuta eneo mbadala na kuwauzia kwa bei
nafuu.
Alizitaka pande hizo mbili
kutambua umuhimu wa kulinda amani katika
mgogoro huo kwa changamoto zilizopo kutatuliwa bila kutumia
nguvu.Makonda pia aliagiza serikali ya kijiji kufanya
utambuzi wa
wananchi hao wenye makazi katika shamba la Sumaye. Awali
katika mkutano
huo Mhe. Sumaye alimueleza Mhe. Makonda jinsi serikali
ilivyo na kazi
ngumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi na kuomba kutumia
busara zake
kumpatia eneo hilo analomiliki kihalali.
"Mheshimiwa Mkuu wa
Wilaya kama nilivyokueleza awali serikali yetu inakazi ngumu
sana hasa
kutokana na viongozi wa chini kutokuwa wasikivu na wakweli
eneo hili
namiliki kihalali nina nyaraka zote na ninalipia kila mwaka
na nilikuwa
katika mpango wa kutafuta wafadhili ili kuliendeleza kwa
kujenga Chuo
Kikuu,"alisema. Alisema yeye na familia yake waliuziwa
eneo hilo toka
mwaka 1997 na anaamini serikali itatenda haki.
Diwani wa kata
hiyo Suzan Masawe alisema anauthibitisho kuwa eneo hilo
lilikuwa pori na
Sumaye alilitelekeza kwa muda mrefu na kusababisha uhalifu
ikiwemo
wanawake kubakwa,mali za wizi kufichwa na uhalifu
mbalimbali. Alisema
kutokana na hatua hiyo walimtafuta Sumaye lakini hakuwa na
ushirikiano
kwakuwa hata alipofanya uwekezaji kwa kuchimba kisima cha
maji alikataa
kuwapa wananchi .
Suzan alisema kutokana na hasira za
wananchi
hao kwa kukosa huduma za kijamii kwa muda mrefu ikiwemo eneo
hilo
kutokuwa na shule,Zahanati wala kituo cha polisi waliamua
kuvamia na
kujigaia maeneo. Mmoja wa wananchi hao Athuman Mnubi alikiri
kweli
hawana umiliki halali wa eneo hilo na katika hatua ya
kutafuta makazi
walivamia msitu huo uliotelekezwa na Sumaye.
Alisema wanaamini
kutokana na ahadi ya serikali ya Rais Magufuli katika kupora
maeneo
yaliyotelekezwa na wawekezaji watasaidiwa. WAKATI huo huo
Makonda
alisimamisha na kukamata baadhi ya malori ya kokoto na
mchanga,
wafanyakazi na Mwekezaji wa kigeni kutoka India Sules Waljan
wanaochimba
mchanga,kokoto na kifusi katika eneo la Mabwepande. Hatua
hiyo imekuja
baada ya kuona uharibifu mkubwa wa mazingira na alipowahoji
wafanyakazi
na Mwekezaji huyo kama wanavibali walisema hawana.
Makonda
amewafikisha watuhumiwa hao kituo cha polisi cha Wazo Hill
ili kutoa
maelezo ya kina na kusema kuwa serikali inatumia gharama
kubwa kwa
uhalibifu huo wa mazingira ambao pia unafanywa katika vyanzo
vya maji na
matengenezo ya madaraja yanayoharibiwa ni
makubwa.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment