Watu 21 wamefariki dunia katika ajali mbaya iliyotokea jana saa mbili usiku katika Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani ikihusisha magari 3 na wengine 11 kujeruhiwa.
Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei, alisema ajali hiyo imetokea katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam-Lindi, eneo la Ikwiriri, wilayani humo.
Awali ajali hiyo ilihusisha magari mawili, Toyota Hiace (T 948 CUX), iliyokuwa ikitokea Ikwiriri kuelekea
Rufiji ambalo lilikwenda kukwaruzana na lori (T 132 AFJ) kwa nyuma, ambalo lilikuwa limeharibika na kusimama barabarani.
Alisema baada ya kulikwaruza lori hilo, mlango wa Hiace uling'oka na kubaki kwenye roli ambapo gari hiyo lilipoteza mwelekeo na kwenda kugongana uso kwa uso na gari nyingine aina ya Canter (T 774 CJW) na kupinduka.
"Katika ajali hii, watu 14 walifariki dunia papo hapo, wakati polisi na baadhi ya wananchi wakiendelea kuwaokoa majeruhi ili wakimbizwe hospitali, likatokea basi la kampuni ya Mining (President) (T 242 BXA), kuwakanyaga watu waliokuwa wakitoa msaada na kuwaua ndio maana idadi ya waliokufa imefikia 21.
"Basi hili lilikuwa linatoka Lindi kuelekea Dar es Salaam... polisi walifanya jitihada za kulisimamisha lakini dereva wake alikataa kusimama na kwenda kukanyaga watu lakini tayari tumemkamata. Majeruhi mmoja amehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam,"
alisema Kamanda Matei.
Kamanda Matei alisema, basi hilo linashikiliwa polisi ambapo uchunguzi ukikamilika, dereva wake atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka.
Aliwataja waliokufa ni Sixtus Ally Mtanga (32) na Nassoro Mohamed Kajani (20) wakazi wa Ikwiriri, Juma Said Kitambulilo (30), Salum Goma Makonde (50), Ustaadhi Kalilambwe (34), Shafil Kip (30), Wasabi Sabil (45), Ramadhani Ally (23) wote wakazi wa Mbagala.
Shabani Bakari (30) Kondakta wa Hiace, mkazi wa Kibiti, Masud Abulal (27), mkazi wa Mkuranga, Ammi Mpemba (30) na Madadi Hassan Mangasongo (45) wakazi wa Jaribu na Japhet Ponsian (24), mkazi wa Dar es Salaam.
Pia yupo Said Ally China (21) mkazi wa Kimanzichana, Jaribu, Abdalahaman Yusuph Kihemke (45), mkazi wa Kongowe na Fikiri Said Sauze, mkazi wa Vikindu.
Wengine ni Nywari Mshigani mkazi wa Dar es Salaam, Hassan Wasabi (18), mkazi wa Kibiti na Seleman Mcharazi (47) na mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Mustafa, wote wakazi wa Mbagala. Pia ipo maiti ya mwanamke haijafahamika jina lake.
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Frank Sixmundi (31), dereva wa gari la Maliasili Kibiti ambaye alifika eneo ili kutoa msaada kwa majeruhi ambaye ameumia kichwani, Mohamed Salehe (49) na Charles Rogasani (23), wote wakazi wa Kibiti na Mohamed Mengine (42), mkazi wa Dar es Salaam.
Wengine ni Mniko Magige Mango (54) na Abdalah Issa (25) wakazi wa Mkuranga, Khalid Salum (32), mkazi wa Dar es Salaam, Ahmad Yusuph (23), mkazi wa Kigamboni na Shomari Yusuph (42), mkazi wa Mburahati.
Majeruhi wamelazwa katika hospitali za Ikwiriri, Misheni ya Mchukwi na wengine hospitali ya Taifa Muhimbili.
via blog ya Imma Matukio
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment