Sunday 30 March 2014

Re: [wanabidii] CCM NDIO CHAMA TAWALA NI LAZIMA KIONGOZE KATIBA MPYA

Hivi tunaweza tizama financial linkage ya hizi pesa? Hawa waheshimiwa wakishalipwa wanafanyia nini? Wanajenga bar na gest? Wanajenga makazi binafsi? Wananunua magari? Wanaweka bank kwa matumizi ya badae? Au wanatumia katika shughuli za kijamii? Hii inaweza kuwa mbinu nzuri ya kuwawezesha wananchi kiuchumi kwani kupitia kwao kumetengenezwa ajira zaidi zikiwemo za madereva, mafundi washi, na wahudumu mbalimbali.

Ila tatizo kuu ni ''economic diversity'' yaani ukuaji wa uchumi usiotarajiwa usiendana na huduma za jamii.

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, March 30, 2014 12:14:42 PM GMT-0700
Subject: [wanabidii] CCM NDIO CHAMA TAWALA NI LAZIMA KIONGOZE KATIBA MPYA



CCM NDIO CHAMA TAWALA NI LAZIMA KIONGOZE KATIBA MPYA.

Hatimaye mpaka leo Tarehe 30/3/2014 Bunge la Katiba Dodoma sasa limetimiza
siku 40 toka lianze rasmi Tarehe 18/2/2014, na katika muda wote kwa
mahesabu ya haraka haraka Taifa letu limekwisha tumia Shillingi Bilioni
85.6 kwa ajili ya marekebisho ya Katiba kwa ujumla. Shillingi Billioni 70
zilitumika na Kamati ya Tume ya Rasimu ya Warioba, Shillingi Billioni 8.2
zilitumika kukarabati bunge la sasa na Shillingi Billioni 7.6 zimeshatumika
mpaka sasa kwa ajili ya posho tu za Wabunge hao 640 wa bunge hilo huko
Dodoma mahesabu ambayo hayajumlishi matumizi mengine ya kiofisi ya bunge
hilo. Pesa zote hizo zilozkwisha tumika ni sawa na Dola za Kimarekani
Millioni 540 na ukweli bado upo pale pale kwamba wananchi wengi haturidhiki
na matokeo tunayoyaona huko Bungeni Dodoma, ambako bunge jipya limetawaliwa
na malumbano ya kitoto na yasiyo na tija kabisa kwa Wananchi wala Taifa
kinyume na wananchi wengi tulivyotegemea baada ya kuongozwa kwa Miaka 52 na
Katiba ambayo kimsingi ilitengenezwa kukidhi matakwa ya utawala wa Serikali
ya chama kimoja tu CCM. Pesa zilkizokwisha tumika mpaka sasa ambapo Taifa
limeambulia kujionea uwezo mdogo wa kufikiri wa Wabunge wengi wa Bunge
hilo, zingeweza kuimaliza kabisa barabara mpya ya Iringa mpaka Dodoma ya
Kilmoita 260, ambayo inahita dola 140 tu za Kimarekani toka mwanzo wake
mpaka mwisho na bado zingeweza kubaki za kutosha Bajeti nzima ya Wizara ya
Uchukuzi kwa Mwaka huu ambayo ni jumla ya Dola za Kimarekani 153 na bado
zingeweza kubaki hela za kutosha kutengeneza barabara zote za Tanzania ili
ziweze kufikia viwango vya kisasa Mwaka 2025 ambapo zinahitajika jumla ya
Dola za Kimarekani Millioni 222 tu ambapo kwa ujumla wake hapa zingetumika
jumla ya Dola za Kimarekani 514 Millioni, na bado ukabaki na chenji ya Dola
Millioni 26 kwa hela zilizotumika mpaka sasa na Katiba mpya ambayo bado
haipo hata dalili ya theluthi moja tu! Tume ya Rasimu ya Katiba imezichoma
wee pesa za wananchi Billioni 70 na kuishia kutupatia Rasimu ambayo imekuwa
ni utata mtupu kutokana na Tume hiyo kujiingiza kwenye kutenengeza maoni ya
Rasimu badala ya kusikiliza tu na kukusanya maoni ya wananchi kama
ilivyotakiwa na Jamhuri. Zikaja tena zikatumika Billioni 8.2 kukarabati
bunge liweze kuwahudumu Wabunge wote 640, na sasa Billioni 7.6 tayari
zimeshachomwa kwa ajili ya posho za Wabunge hao kwa siku 40 ambapo kila
siku Wabunge hao hulipwa jumla ya Shillingi 300,000.Wanachi wengi
tunajiuliza maswali mengi makubwa na mazito kuliko majibu kwamba kulikoni
huko Dodoma na suala zima la marekebisho ya Katiba?

Wananchi wengi tulitegemea kwamba Wabunge wetu wanakwenda Dodoma wakiwa
wanajua mapema wanachokitaka na wasichokitaka kuhusiana na mapungufu ya
Katiba yetu ambayo imekuwa ikililiwa kwa miaka nenda rudi na Wanasiasa wetu
wa pande zote mbili, yaani Chama tawala na Wapinzani na hasa wananchi wengi
wasomi wa Taifa hili ambao wanawakilishwa vizuri sana na kundi la wajumbe
wapya 201 walioteuliwa na Rais kutokana na mapendekezo ya Taasisi mbali
mbali za Taifa letu. Badala yake tunajionea vituko vya ajabu kila kukicha
ndani ya bunge hilo, kwa siku 10 mfululizo bunge hilo limelumbana kushoto
na kulia kwa hoja moja ndogo sana ya namna ya kupiga kura kama iwe ya siri
au ya wazi. Na hata pale Kamati maalum ya maridhiano ya bunge ilipotoa hoja
ya namna ya kupiga kura hizo, bado Wabunge wetu wameendeleza malumbano ya
kitoto na ya aibu sana yasiyo na tija kabisa kwa Wananchi na Taifa kwa
ujumla.Wabunge tuliowategemea waturekebishie Katiba sasa wamefikia mahali
pa wananchi wengi kujiuliza kujiuliza Taifa letu limekubwa na nani cha
ajabu maana sio siri wanaotuwakilisha huko Dodoma ndio sisi wenyewe
Wananchi wa Tanzania hii ya sasa. Kila siku Wabunge hawa na hasa wasiokuwa
wa CCM wanapochangia hoja za Bunge hilo kuna neno moja wengi wao
wanalirudia rudia kila wakati wakiwashambulia Wabunge wa CCM na wale wote
wanaounga mkono hoja za msimamo wa chama hicho kwamba wasijione kwa vile ni
wengi basi wakadhani kwamba watapitisha mambo yao wanavyotaka, wengine
wameeenda mbali hata kutishia kuondoka Bungeni hapo iwapo hoja zinazoungwa
mkono na CCM zitalazimishwa kupitishwa bila ridhaa zao. Hoja hizi na
zingine za namna hii zimerudiwa bungeni mara kwa mara na hata kuwahoji
Wabunge wa CCM wanaotaka kura za wazi kwamba wanaogopa nini kupiga kura za
siri kama wao wanajiamini ni wengi? Halafu kuna Wabunge ambao kazi yao ni
kuzomea zomea wengine wasiokubaliana na mawazo kama yao, haya yote
yamelifanya Bunge kutonyesha sura halisi ya Taifa letu kwamba bado tuna
kazi kubwa sana ya kubadilika kimawazo kwa vile sio siri kwamba bado tupo
katika usingizi mzito sana kutoelewa maana ya matumizi ya muda, na hasa
mazingira ya kisiasa tuliyomo sasa hivi ambayo ndio hoja yangu hasa ya
msingi ya waraka wangu huu wa leo.

Mataifa yote yalioyendelea Duniani utakuta wananchi wake wana msemo mmoja
mzito wa "Muda ni Pesa", ikiwa na maana kwamba ni makosa makubwa sana kwa
Binadam kuchezea muda kwa sababu historia ya maisha Duniani ipo wazi kwamba
mchezea muda siku zote huwa anazichezea Pesa ambazo aidha angezitengeneza
kwa kutumia muda aliouchezea au kupoteza pesa ambazo tayari anazo lakini
kwa kuchezea muda anaishia kutoongeza zaidi.Kwa mfano, umekata tiketi ya
ndege ya kuondoka Saa Tisa wewe ukafika Saa tisa na dakika mbili maana yake
ni kwamba hutaondoka kwa sababu ndege zote zinafunga milango saa ile ile
uliyoambiwa kwenye tiketi sasa kwa sababu umechelewa ili uitumie tena ile
tiketi basi ni lazima utalazimika kuongeza pesa ili uweze kuitumia
kusafiria ama sivyo ile tiketi itakuwa haina kazi tena.Kwa hiyo utakuwa
umepoteza muda na pesa kama msemo huu unavyosema na sio siri kwamba dhana
zote hizo mbili zimefanyika na Mchakato mzima wa hii Katiba sio tu na hili
bunge tu bali ni kuanzia mwanzo wa Tume hii ya Rasimu mpaka hapo ulipofikia
sasa hivi Taifa hili tumepoteza muda mwingi sana wa Taifa na pia tumepoteza
pesa nyingi za Taifa.

Halafu ni dhana muhimu na ya msingi haswa wa waraka wangu huu wa leo nayo
ni nafasi ya chama tawala CCM katika mchakato huu mzima wa kurekebisha
Katiba, Wabunge wengi wasiokuwa wa CCM wanaonekana kutoelewa kabisa umuhimu
wao ndani ya suala hili. Ni muhimu sana tukawekana sawa kwenye hili tena
kuambiana ukweli usio mzuri sana lakini ni ukweli wa mambo wa mazingira ya
kisiasa tuliona Taifa hili la Tanzania, ni kwamba Chama Cha Mapinduzi ndio
chama chenye ridhaa ya wananchi wa Tanzania kutawala kutokana na kura
walizowapa kwenye chaguzi karibu zote kuanzia Kata, Wilaya, Mikoa mpaka
Taifa. Chama hicho ndicho chenye Viongozi wengi waliochaguliwa na wananchi
kwenye kila kona za chaguzi za Taifa hili kwa hiyo kama Sheria inavyosema
wao ndio wenye nafasi kubwa ya kufanya maamuzi mengi sana ndani ya mchakato
huu kwa sababu nyingi sana mojawapo ikiwa ni pamoja na wingi wao ndani ya
bunge hili la Katiba kwa mujibu wa Sheria. Sheria ya Bunge la Jamhuri ipo
wazi kwamba ni Theluthi mbili kwa Tatu ndio inayotawala ndani ya jengo hilo
la Taifa, kwa maana ya kwamba wengi ndio wenye nafasi kubwa ya kushinda
maamuzi mengi kutokana na dhana muhimu sana ya wengi ndio wenye hoja ndani
ya Demokrasia yoyote Duniani. Na ni ukweli usiopingika kuwa ni Serikali ya
chama hicho hicho Tawala iliyoamua kuruhusu mchakato huu kwa hiyo,
haiwekzekani kwamba Chama hicho hakikujua kwamba kwenye mbio hizi za
mchakato kungetokea ambayo yanatokea sasa hivi, halafu baada ya kutawala
miwa miaka 52 mfululizo chama hicho sasa hivi ndio chama pekee kikongwe
kilichomo kwenye madaraka katika Afrika nzima ni kwa sababu kimepitia
madharuba mengi sana ndio kipo hapo kilipo yaani bado kwenye madaraka. Wale
wabunge wote wasiotaka kuelewa ukweli ni kwamba CCM ndio wengi ndani ya
Bunge sio kwa bahati mbaya ila kwa mujibu wa sheria kwa hiyo ni lazima
Wabunge hao waelewe hilo katika kazi zao zote humo Bungeni.

Demokrasia ipo wazi katika Dunia nzima inapotumika kwamba siku zote wengi
wape, kwa hiyo CCM ndio wanaotakiwa kuwa na mkono wa juu katika maamuzi
mengi na wala hawana sababu ya kuogopa au kujisikia vibaya au kuanza siasa
za huruma. Kwa wale wasiotaka kuelewa hilo ni muhimu wakajitoa huko Bungeni
sasa hivi kuliko kupoteza muda bure wa Taifa kubishania hoja zisizo na
mashiko za kuilaumu CCM kwa wingi wao bungeni ni ujuha wa hali ya juu sana
ambao usingetegemea kuonekana Bunge la Taifa. Wabunge wakubali ukweli
kwamba wananchi wengi wa Tanzania wanaridhika na CCM na ndio maana wapo
madarakani kwa miaka 52 toka tupate Uhuru mpaka leo, huu ni ukweli
usiopingika kwamba hata wanayoyasimamia ndio yanayoungwa mkono na wananchi
wengi wa Taifa hili. Sasa tunakubali kwamba kutakuwa na misuguano ndani ya
mchakato huu ni muhimu sana wabunge wasio wa CCM wakalielewa na kulikubali
hili kwamba CCM ndio wenye mkono mrefu kutokana na wingi wao unaotokana na
kukubalika zaidi na wananchi wengi wa Taifa hili. Kwenye waraka wa leo
nimeshindwa kwa makusudi kabisa kutumia mifano ya Demokrasia zingine ni kwa
sababu ya kuelewa sana kwamba katika suala la mchakato kama huu huwezi
kutumia mifano ya mataifa mengine kwa sababu mazingira ya kila Taifa
lililohusika na michakato ya namna hii hayafanani kabisa.

Kwa kumaliza ninapenda kuwakumbusha Wabunge wa bunge hili la Katiba kwamba
wafike mahali wajiridhishe na ukweli wa mazingira ya kisiasa tuliyonayo
kwamba CCM ndio chama Tawala na ndio kwa mujibu wa Sheria na kwamba pamoja
na Demokrasia kuwapa nafasi ya kushiriki kwa kutoa mawazo yao, bado
inapofikia mahali pa kushindana sana basi zitapigwa kura za wanaotaka na
wasiotaka na sio siri kwamba kwenye kura za namna hiyo CCM watakuwa ndio
wenye mkono mrefu kuliko wengine. Wakubali kwamba uamuzi wa kufanyika
marekebisho ya Katiba umefanyika kutokana na kilio cha wananchi wengi wa
Taifa hili na ni kilio kilichosikilizwa na Chama Tawala CCM, tunategemea
wabunge wote wafanye kazi pamoja na kutuletea Katiba mpya yenye tija kwa
wananchi na Taifa. Wafike pahali waachane na malumbano ya kitoto yasiyo na
tija kabisa kama yalikuwa yakifanyika jana juzi Tarehe 27/3/2014, ilikuwa
ni moja ya siku ya aibu sana kwa Taifa hili na hasa watoto wetu na wajukuu
wetu, ninaomba kuwakumbusha wabunge wetu kwamba Taifa limekwisha tumia
Shiilingi Billioni 85.6 na mpaka leo siku ya 40 bado hatujaona la maana
walilokwisha lifanya kuelekea kutuaminisdha kwamba tutapata Katiba mpya na
bora kwa Taifa. Tumewasikia kwamba wengi wao ni wasemaji wazuri sana, wengi
wao ni wasemaji wazuri sana, lakini mwisho wa yote CCM ndio wengi ndani ya
bunge na ndio wenye nafasi ya kuamua maamuzi mengi iwapo kutatokea utata au
msuguano kwenye hoja, na wajaribu sana kuweka Tanzania kwanza.

MUNGU AIBARIKI TANZANIA

WILLIAM J. MALECELA +255 717 618 997
williammalecela.com/willymalec@gmail.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment