Saturday 29 March 2014

[wanabidii] Wanajeshi JWTZ wanaendelea kuwapa mashaka wananchi wa Kimbiji, Dar-es-salaam


Wanajeshi JWTZ kuwanyang'anya Ardhi wananchi Kimbiji ! 
Wananchi wanaishi kwa mashaka kwa mda wa wiki mbili sasa!

Hali ya wasi wasi na maisha ya mashaka yanayosababishwa na 
uvunjwaji wa haki za binadamu unaofanywa na kikosi kimoja cha
jeshi la wananchi JWTZ unazidi kuwapa kero wananchi wa maeneo
ya Kimbiji,wilayani Temeke,Dar-es-salaam.
Kutokana na kuvamiwa na wanajeshi katika makazi na maeneo yao
ya ardhi,ambapo wanajeshi wanawalazimisha wananchi waondoke
bila ya ridhaa yao, wala kufuata misingi na taratibu za sheria za
ardhi.
Baadhi ya wanajeshi wamekuwa wakiweka mahema nje ya makazi 
ya raia hao na kuwapa usumbufu familia za raia hao wakiwemo
akina mama na watoto.
Pamoja na wananchi wa Kimbiji kulalamika mara nyingi katika
vyombo vya habari ,pia katika vyombo serikali kuhusu majanga
haya, cha kusikitisha hakuna jibu lolote walilo pewa !
Wananchi wa Kimbiji wanasikitishwa sana na usumbufu wanao upata
kutoka kwa wanajeshi JWTZ ambao wanadhamana ya kulinda nchi
sio kuwanyanyasa wananchi bila ya kufuata misingi ya sheria za miliki
ardhi,wakati serekali nayo haijatoa tamko lolote kuhusu unyanyaswaji huo.

Wananchi wa Kimbiji wanamiliki maeneo yao ya asili na hawajawai 
kushiriki katika kikako chochote kile kinachohusu kugawa maeneo
au kupisha mradi wowote ule wa maendeleo na Jeshi JWTZ.
Wananchi wa Kimbiji wamedai kuwa wanajeshi wana lengo la kuwapora
Ardhi kwa kutumia vitisho vya kofia na nembo ya JWTZ.
wananchi wanaiomba serikali pamoja tahasisi za mbali mbali 
kuingilia kati na kulitafutia ufumbuzi tatizo hili linalo wanyima usingizi 
wananchi wa Kimbiji.
kwa maelezo zaidi wasiliana na uongozi wa kimbiji 
Simu: 0713768082 Diwani au 0713846688 Mwenyekiti


0 comments:

Post a Comment