Monday 31 March 2014

Re: [wanabidii] CCM NDIO CHAMA TAWALA NI LAZIMA KIONGOZE KATIBA MPYA

Na hisi kichwa cha habari kimekosewa au? Kama kiko sawa basi u chama tawala wa Maccm umeshindwa kuongoza kuelekea kwenye kuundwa kwa katiba mpya. Ndo maana sasa wanachochea jeshi liingilie kati kuitawala inchi.

On 30 Mar 2014 19:14, "Abdalah Hamis" <hamisznz@gmail.com> wrote:

CCM NDIO CHAMA TAWALA NI LAZIMA KIONGOZE KATIBA MPYA.

Hatimaye mpaka leo Tarehe 30/3/2014 Bunge la Katiba Dodoma sasa limetimiza siku 40 toka lianze rasmi Tarehe 18/2/2014, na katika muda wote kwa mahesabu ya haraka haraka Taifa letu limekwisha tumia Shillingi Bilioni 85.6 kwa ajili ya marekebisho ya Katiba kwa ujumla. Shillingi Billioni 70 zilitumika na Kamati ya Tume ya Rasimu ya Warioba, Shillingi Billioni 8.2 zilitumika kukarabati bunge la sasa na Shillingi Billioni 7.6 zimeshatumika mpaka sasa kwa ajili ya posho tu za Wabunge hao 640 wa bunge hilo huko Dodoma mahesabu ambayo hayajumlishi matumizi mengine ya kiofisi ya bunge hilo. Pesa zote hizo zilozkwisha tumika ni sawa na Dola za Kimarekani Millioni 540 na ukweli bado upo pale pale kwamba wananchi wengi haturidhiki na matokeo tunayoyaona huko Bungeni Dodoma, ambako bunge jipya limetawaliwa na malumbano ya kitoto na yasiyo na tija kabisa kwa Wananchi wala Taifa kinyume na wananchi wengi tulivyotegemea baada ya kuongozwa kwa Miaka 52 na Katiba ambayo kimsingi ilitengenezwa kukidhi matakwa ya utawala wa Serikali ya chama kimoja tu CCM. Pesa zilkizokwisha tumika mpaka sasa ambapo Taifa limeambulia kujionea uwezo mdogo wa kufikiri wa Wabunge wengi wa Bunge hilo, zingeweza kuimaliza kabisa barabara mpya ya Iringa mpaka Dodoma ya Kilmoita 260, ambayo inahita dola 140 tu za Kimarekani toka mwanzo wake mpaka mwisho na bado zingeweza kubaki za kutosha Bajeti nzima ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka huu ambayo ni jumla ya Dola za Kimarekani 153 na bado zingeweza kubaki hela za kutosha kutengeneza barabara zote za Tanzania ili ziweze kufikia viwango vya kisasa Mwaka 2025 ambapo zinahitajika jumla ya Dola za Kimarekani Millioni 222 tu ambapo kwa ujumla wake hapa zingetumika jumla ya Dola za Kimarekani 514 Millioni, na bado ukabaki na chenji ya Dola Millioni 26 kwa hela zilizotumika mpaka sasa na Katiba mpya ambayo bado haipo hata dalili ya theluthi moja tu! Tume ya Rasimu ya Katiba imezichoma wee pesa za wananchi Billioni 70 na kuishia kutupatia Rasimu ambayo imekuwa ni utata mtupu kutokana na Tume hiyo kujiingiza kwenye kutenengeza maoni ya Rasimu badala ya kusikiliza tu na kukusanya maoni ya wananchi kama ilivyotakiwa na Jamhuri. Zikaja tena zikatumika Billioni 8.2 kukarabati bunge liweze kuwahudumu Wabunge wote 640, na sasa Billioni 7.6 tayari zimeshachomwa kwa ajili ya posho za Wabunge hao kwa siku 40 ambapo kila siku Wabunge hao hulipwa jumla ya Shillingi 300,000.Wanachi wengi tunajiuliza maswali mengi makubwa na mazito kuliko majibu kwamba kulikoni huko Dodoma na suala zima la marekebisho ya Katiba?

Wananchi wengi tulitegemea kwamba Wabunge wetu wanakwenda Dodoma wakiwa wanajua mapema wanachokitaka na wasichokitaka kuhusiana na mapungufu ya Katiba yetu ambayo imekuwa ikililiwa kwa miaka nenda rudi na Wanasiasa wetu wa pande zote mbili, yaani Chama tawala na Wapinzani na hasa wananchi wengi wasomi wa Taifa hili ambao wanawakilishwa vizuri sana na kundi la wajumbe wapya 201 walioteuliwa na Rais kutokana na mapendekezo ya Taasisi mbali mbali za Taifa letu. Badala yake tunajionea vituko vya ajabu kila kukicha ndani ya bunge hilo, kwa siku 10 mfululizo bunge hilo limelumbana kushoto na kulia kwa hoja moja ndogo sana ya namna ya kupiga kura kama iwe ya siri au ya wazi. Na hata pale Kamati maalum ya maridhiano ya bunge ilipotoa hoja ya namna ya kupiga kura hizo, bado Wabunge wetu wameendeleza malumbano ya kitoto na ya aibu sana yasiyo na tija kabisa kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla.Wabunge tuliowategemea waturekebishie Katiba sasa wamefikia mahali pa wananchi wengi kujiuliza kujiuliza Taifa letu limekubwa na nani cha ajabu maana sio siri wanaotuwakilisha huko Dodoma ndio sisi wenyewe Wananchi wa Tanzania hii ya sasa. Kila siku Wabunge hawa na hasa wasiokuwa wa CCM wanapochangia hoja za Bunge hilo kuna neno moja wengi wao wanalirudia rudia kila wakati wakiwashambulia Wabunge wa CCM na wale wote wanaounga mkono hoja za msimamo wa chama hicho kwamba wasijione kwa vile ni wengi basi wakadhani kwamba watapitisha mambo yao wanavyotaka, wengine wameeenda mbali hata kutishia kuondoka Bungeni hapo iwapo hoja zinazoungwa mkono na CCM zitalazimishwa kupitishwa bila ridhaa zao. Hoja hizi na zingine za namna hii zimerudiwa bungeni mara kwa mara na hata kuwahoji Wabunge wa CCM wanaotaka kura za wazi kwamba wanaogopa nini kupiga kura za siri kama wao wanajiamini ni wengi? Halafu kuna Wabunge ambao kazi yao ni kuzomea zomea wengine wasiokubaliana na mawazo kama yao, haya yote yamelifanya Bunge kutonyesha sura halisi ya Taifa letu kwamba bado tuna kazi kubwa sana ya kubadilika kimawazo kwa vile sio siri kwamba bado tupo katika usingizi mzito sana kutoelewa maana ya matumizi ya muda, na hasa mazingira ya kisiasa tuliyomo sasa hivi ambayo ndio hoja yangu hasa ya msingi ya waraka wangu huu wa leo.

Mataifa yote yalioyendelea Duniani utakuta wananchi wake wana msemo mmoja mzito wa "Muda ni Pesa", ikiwa na maana kwamba ni makosa makubwa sana kwa Binadam kuchezea muda kwa sababu historia ya maisha Duniani ipo wazi kwamba mchezea muda siku zote huwa anazichezea Pesa ambazo aidha angezitengeneza kwa kutumia muda aliouchezea au kupoteza pesa ambazo tayari anazo lakini kwa kuchezea muda anaishia kutoongeza zaidi.Kwa mfano, umekata tiketi ya ndege ya kuondoka Saa Tisa wewe ukafika Saa tisa na dakika mbili maana yake ni kwamba hutaondoka kwa sababu ndege zote zinafunga milango saa ile ile uliyoambiwa kwenye tiketi sasa kwa sababu umechelewa ili uitumie tena ile tiketi basi ni lazima utalazimika kuongeza pesa ili uweze kuitumia kusafiria ama sivyo ile tiketi itakuwa haina kazi tena.Kwa hiyo utakuwa umepoteza muda na pesa kama msemo huu unavyosema na sio siri kwamba dhana zote hizo mbili zimefanyika na Mchakato mzima wa hii Katiba sio tu na hili bunge tu bali ni kuanzia mwanzo wa Tume hii ya Rasimu mpaka hapo ulipofikia sasa hivi Taifa hili tumepoteza muda mwingi sana wa Taifa na pia tumepoteza pesa nyingi za Taifa.

Halafu ni dhana muhimu na ya msingi haswa wa waraka wangu huu wa leo nayo ni nafasi ya chama tawala CCM katika mchakato huu mzima wa kurekebisha Katiba, Wabunge wengi wasiokuwa wa CCM wanaonekana kutoelewa kabisa umuhimu wao ndani ya suala hili. Ni muhimu sana tukawekana sawa kwenye hili tena kuambiana ukweli usio mzuri sana lakini ni ukweli wa mambo wa mazingira ya kisiasa tuliona Taifa hili la Tanzania, ni kwamba Chama Cha Mapinduzi ndio chama chenye ridhaa ya wananchi wa Tanzania kutawala kutokana na kura walizowapa kwenye chaguzi karibu zote kuanzia Kata, Wilaya, Mikoa mpaka Taifa. Chama hicho ndicho chenye Viongozi wengi waliochaguliwa na wananchi kwenye kila kona za chaguzi za Taifa hili kwa hiyo kama Sheria inavyosema wao ndio wenye nafasi kubwa ya kufanya maamuzi mengi sana ndani ya mchakato huu kwa sababu nyingi sana mojawapo ikiwa ni pamoja na wingi wao ndani ya bunge hili la Katiba kwa mujibu wa Sheria. Sheria ya Bunge la Jamhuri ipo wazi kwamba ni Theluthi mbili kwa Tatu ndio inayotawala ndani ya jengo hilo la Taifa, kwa maana ya kwamba wengi ndio wenye nafasi kubwa ya kushinda maamuzi mengi kutokana na dhana muhimu sana ya wengi ndio wenye hoja ndani ya Demokrasia yoyote Duniani. Na ni ukweli usiopingika kuwa ni Serikali ya chama hicho hicho Tawala iliyoamua kuruhusu mchakato huu kwa hiyo, haiwekzekani kwamba Chama hicho hakikujua kwamba kwenye mbio hizi za mchakato kungetokea ambayo yanatokea sasa hivi, halafu baada ya kutawala miwa miaka 52 mfululizo chama hicho sasa hivi ndio chama pekee kikongwe kilichomo kwenye madaraka katika Afrika nzima ni kwa sababu kimepitia madharuba mengi sana ndio kipo hapo kilipo yaani bado kwenye madaraka. Wale wabunge wote wasiotaka kuelewa ukweli ni kwamba CCM ndio wengi ndani ya Bunge sio kwa bahati mbaya ila kwa mujibu wa sheria kwa hiyo ni lazima Wabunge hao waelewe hilo katika kazi zao zote humo Bungeni.

Demokrasia ipo wazi katika Dunia nzima inapotumika kwamba siku zote wengi wape, kwa hiyo CCM ndio wanaotakiwa kuwa na mkono wa juu katika maamuzi mengi na wala hawana sababu ya kuogopa au kujisikia vibaya au kuanza siasa za huruma. Kwa wale wasiotaka kuelewa hilo ni muhimu wakajitoa huko Bungeni sasa hivi kuliko kupoteza muda bure wa Taifa kubishania hoja zisizo na mashiko za kuilaumu CCM kwa wingi wao bungeni ni ujuha wa hali ya juu sana ambao usingetegemea kuonekana Bunge la Taifa. Wabunge wakubali ukweli kwamba wananchi wengi wa Tanzania wanaridhika na CCM na ndio maana wapo madarakani kwa miaka 52 toka tupate Uhuru mpaka leo, huu ni ukweli usiopingika kwamba hata wanayoyasimamia ndio yanayoungwa mkono na wananchi wengi wa Taifa hili. Sasa tunakubali kwamba kutakuwa na misuguano ndani ya mchakato huu ni muhimu sana wabunge wasio wa CCM wakalielewa na kulikubali hili kwamba CCM ndio wenye mkono mrefu kutokana na wingi wao unaotokana na kukubalika zaidi na wananchi wengi wa Taifa hili. Kwenye waraka wa leo nimeshindwa kwa makusudi kabisa kutumia mifano ya Demokrasia zingine ni kwa sababu ya kuelewa sana kwamba katika suala la mchakato kama huu huwezi kutumia mifano ya mataifa mengine kwa sababu mazingira ya kila Taifa lililohusika na michakato ya namna hii hayafanani kabisa.

Kwa kumaliza ninapenda kuwakumbusha Wabunge wa bunge hili la Katiba kwamba wafike mahali wajiridhishe na ukweli wa mazingira ya kisiasa tuliyonayo kwamba CCM ndio chama Tawala na ndio kwa mujibu wa Sheria na kwamba pamoja na Demokrasia kuwapa nafasi ya kushiriki kwa kutoa mawazo yao, bado inapofikia mahali pa kushindana sana basi zitapigwa kura za wanaotaka na wasiotaka na sio siri kwamba kwenye kura za namna hiyo CCM watakuwa ndio wenye mkono mrefu kuliko wengine. Wakubali kwamba uamuzi wa kufanyika marekebisho ya Katiba umefanyika kutokana na kilio cha wananchi wengi wa Taifa hili na ni kilio kilichosikilizwa na Chama Tawala CCM, tunategemea wabunge wote wafanye kazi pamoja na kutuletea Katiba mpya yenye tija kwa wananchi na Taifa. Wafike pahali waachane na malumbano ya kitoto yasiyo na tija kabisa kama yalikuwa yakifanyika jana juzi Tarehe 27/3/2014, ilikuwa ni moja ya siku ya aibu sana kwa Taifa hili na hasa watoto wetu na wajukuu wetu, ninaomba kuwakumbusha wabunge wetu kwamba Taifa limekwisha tumia Shiilingi Billioni 85.6 na mpaka leo siku ya 40 bado hatujaona la maana walilokwisha lifanya kuelekea kutuaminisdha kwamba tutapata Katiba mpya na bora kwa Taifa. Tumewasikia kwamba wengi wao ni wasemaji wazuri sana, wengi wao ni wasemaji wazuri sana, lakini mwisho wa yote CCM ndio wengi ndani ya bunge na ndio wenye nafasi ya kuamua maamuzi mengi iwapo kutatokea utata au msuguano kwenye hoja, na wajaribu sana kuweka Tanzania kwanza.

MUNGU AIBARIKI TANZANIA

WILLIAM J. MALECELA +255 717 618 997
williammalecela.com/willymalec@gmail.com


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment