Sunday 30 March 2014

[wanabidii] Msingi wa Rasimu ya Katiba ni muundo wa Muungano

Na Kitila Mkumbo

Wabunge wakikataa muundo wa muungano unaopendekezwa Rasimu hii inakufa kwa sababu karibu ibara zingine zote zimewekwa kwa kuzingatia muundo huu wa muungano. Kwa kifupi kukataa muundo wa muungano unaopendekezwa ni kuikataa rasimu yenyewe. Swali, ni je wabunge wakiikataa rasimu hii wana uhalali wa kuendelea kujadili? Kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba, kazi ya bunge maalumu la katiba ni kujadili na kupitisha rasimu ya katiba. Sheria haikutoa nafasi ya kuikataa rasimu hii. Kazi ya kuikubali au kuikataa wameachiwa wananchi wakati wa referundum. 

Kwa wale kama mimi ambapo ni wazoefu wa kujadili na kupitisha proposals mbalimbali tunajua kwamba ukiikataa proposal fulani haimanishi kwamba unachukua jukumu la kuiandika hiyo proposal. Unachofanya ni kutoa mapendekezo ya kuboresha na unamrudishia mwandishi akaiboreshe proposal yake kutokana na mapendekezo uliyompa. Mantiki ni hiyo hiyo. Kama wabunge wetu wataikataa rasimu (proposal) ya katiba hawawezi kujivika jukumu la kuandika rasimu ingine. Hiyo itakuwa sawa na kuipokonya tume kazi yake. Ambacho wangeweza kufanya ni kupitisha mapendekezo na kuirudishia tume iyaingiza mapendekezo hayo. Kwa mfano, wakikataa muundo wa serikali tatu na wakaamua muundo wa serikali mbili, wangepaswa kuwarudishia rasimu tume ili wabadilishe huo muundo. Bahati mbaya sheria haitoi mwanya huo. Hapa ndipo tunapoona deadlock itakayosababishwa na uking'ang'anizi wa CCM wa kutaka serikali mbili. Unaweza ukaona kwamba zoezi zima hili ni kutwanga maji. Ndio maana mie naona wale wanaokesha kuombea swala hili la katiba wanapaswa kumuomba Mungu awalainishe na kuwalegeza CCM ili wakubaliane na mapendekezo ya tume.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment