Saturday 29 March 2014

[wanabidii] re: [Wanazuoni] WAZEE NA WASTAAFU WANAPASWA KUANGALIWA

Viongozi wetu kimsingi tunahitaji kuwaenzi lakini katika kufanya hivyo tuangalie na michango yao kwa taifa. Wapo waliosababisha majonI na hasara kubwa kwa taifa kiasi cha kuathiri maisha ya umma. Sasa tutakuwa na huruma gani inayoangalia mtu mmoja huku tukiwalazimisha watanzania wakila nyasi? Wapo mawaziri wamewahi kutamka kuwa hata kama wananchi wanakufa kwa njaa potelea pote ila maamuzi ya wizara yanaendelea, je na hawa watengewe kodi ya kuwalea? Napendkeza kuwa na utaratibu wa kuangalia ufanisi ili kuwaenzi

----------
Sent from my Nokia

------Original message------
From: LAURENT RUGE <lazanex@yahoo.com>
To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>,"wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>,"wanataaluma@googlegroups.com" <wanataaluma@googlegroups.com>
Date: Wednesday, March 26, 2014 11:44:36 PM GMT-0700
Subject: Re: [Wanazuoni] WAZEE NA WASTAAFU WANAPASWA KUANGALIWA

Kwa maelezo ya Yona, serikali , vyama vitabidi vishughulike na makundi ya watu wote.
Mfano, wazee au watu wenye madaraka sehemu mbalimbali , je ni makampuni au taasisi walizofanyia kazi ndizo ziwalinde?
 
Maprofesa wa vyuo mbalimbali, walimu , madaktari, mahakimu, polisi, listi  ni ndefu nani anawajibu wa kutunza hawa?
 
Nchi nyingine wanafanyaje au ni Tanzania tu?
 
Je hawa uliowaita viongozi, ni kweli walikuwa viongozi au walikalia nafasi tu?
 
Kama walikuwa viongozi kwanini mguso wao usionekane katika jamii? Kwa kuendelea kuwa wenye tija kwa nchi, kuliko kuomba serikali tena ibebe mizigo hii Serikali ina wajibu wa kubeba mizigo binafsi kama hiii????


________________________________
From: "mruahdeo@yahoo.co.uk" <mruahdeo@yahoo.co.uk>
To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>; wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; "wanataaluma@googlegroups.com" <wanataaluma@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, March 25, 2014 12:23 PM
Subject: Re: [Wanazuoni] WAZEE NA WASTAAFU WANAPASWA KUANGALIWA



 
Mipaka ya wapi wajibu wa serikali unaishia na wapi wajibu wa mtu binafsi unaanzia inabidi ibainishwe kwanza kabla hatujaamua wapi lawama ziende.
Regards,
Sent from Yahoo Mail on Android



________________________________
From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>;
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; Wanazuoni <wanazuoni@yahoogroups.com>; wanataaluma@googlegroups.com <wanataaluma@googlegroups.com>;
Subject: [Wanazuoni] WAZEE NA WASTAAFU WANAPASWA KUANGALIWA
Sent: Tue, Mar 25, 2014 9:57:40 AM


 
Ndugu zangu ,

Leo katika harakati zangu za kutafuta gazeti Fulani nilikutana na kitu ambacho si cha kawaida katika maisha yangu , ilibidi nirudi nyuma niangalie picha yake vizuri nikadhibitisha ni yeye .

Nilikutana na Waziri wa Zamani Stendi ya Mabasi makubwa ubungo , amekaa pembeni ya muuza magazeti anapigwa na vumbi linalotoka barabarani na jua kali la maeneo hayo jumlisha na kelele za magari na wapiti kwa miguu kule nje .

Huyu ni waziri tena aliyekuwa kwenye wizara nyeti tu na wakati wa kupokea uwaziri wake aliapa kulinda siri za nchi , za baraza la mawaziri pamoja na nyingine za majukumu yake ya kila siku .

Alikuwa waziri wakati wa kipindi cha Benjamin Mkapa .

Nilijiuliza maswali mengi , hivi mzee kama huyu aliyepanda cheo kuwa mbunge mpaka waziri kamili amekosea nini nchi hii , amekosea nini chama chake cha CCM mpaka kuwa kwenye hali ile ? Mbona nilisikia kuna baraza la wazee huko CCM , vipi hawa tunaokutana nao mtaani ?

Hii ni aibu kwa chama kilichomlea yaani CCM , serikali ya Tanzania na watanzania wote kwa ujumla kwa kushinda kupanga maisha yajayo kwa wazee na wastaafu wengi wanaoendelea kuishi maisha ya tabu na ya shida kama haya pamoja na kutumika kwa miaka mingi .

Wabunge wa bunge la katiba waangalie na suala hili la wazee na wastaafu liwe vizuri kwenye katiba ili tuweze kuokoa wazee wetu wengi pamoja na wastaafu siku zijazo .

--


Yona Fares Maro


Institut d'études de sécurité - SA




--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment