Monday 31 March 2014

[wanabidii] BOKO HARAM NA KATIBA YETU

Ndugu zangu ,


Nadhani wengi wanawajua Boko Haram , kile wanachofanya nchini Nigeria na Maeneo ya Jirani .


Mwezi huu pekee Wamefanikiwa kurudisha kikosi maalumu cha jeshi la Nigeria kilichotumwa kwenda kupambana nao sehemu Fulani huko Maiduguri , Wamejaribu walivamia jela moja yenye ulinzi mkali na kufanikiwa kukomboa wenzao waliokuwemo ndani na wakapiga picha za video wakati wa uvamizi huo , Weekend hii wamejaribu kutoroka kwenye jela moja ya usalama wa taifa iliyopo mji wa Abuja ambapo watu 21 wamefariki katika mapigani ya saa 4 .


Boko Haram wanaonyesha kupata nguvu zaidi nchini Nigeria na kuendelea kupanua harakati zao baada ya Serikali ya Nchi hiyo kuamua kutumia nguvu na kutangaza hali ya hatari kwenye baadhi ya maeneo ya nchi hiyo ambayo Boko Haram wana nguvu .


Serikali ya Nigeria imeanza kutuhumu baadhi ya raia wa nchi jirani kama ndio wanaotoa misaada kwa book haram na kuwaficha wakati wanatafutwa au kuwapa misaada ya mbinu ili kwenda kushambulia wanajeshi wa Nigeria na maslahi yake .


Ni wakati wa kuangalia harakati za Boko Haram zilivyoanza na serikali ya nchi hiyo ilivyopuuza mpaka hali ilivyosasa na upande wetu sisi Tanzania ambao tupo kwenye mchakato wa kuandaa katiba mpya .


Kwetu tuna matatizo ya wakulima na wafugaji , suala la gesi huko mtwara , suala la madini kanda ya ziwa na mengine kadhaa ambayo yameanza kuwa sugu na kuanza kuzalisha Boko Haram wetu ambao miaka michache ijayo wanaweza kuchukuwa silaha na kuingia kupambana na mamlaka iliyopo kipindi hicho .


 Wakati wetu ni sasa , tujadili masuala ya katiba kwa kuangalia yanayowakuta wenzetu , tuwe na nzuri itakayotuma maelewano na amani zaidi kwa watanzania wa sasa na miaka 100 inayo .


--

Yona Fares Maro

Institut d'études de sécurité - SA


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment