Friday, 28 March 2014

Re: [wanabidii] Re: mvua dar tishio

ni kweli Yona.Hata hivyo watendaji wengi sasa hivi wa serikali kwa kweli hawatendi ipasavyo.Wengi wanahujumu nchi.Mimi ninao mfano hai kabisa.Barabara hii ya Morogoro inayojengwa ni wenzetu waliolipa kodi zao huko nje ili sisi tupone.Lakini wafanyakazi wanaofanya kazi wengi wao sio waaminifu.Mfano STRABAG wameajiri watanzania wengi na nimeshuhudia sana kokoto zikiibiwa kila iitwapo leo zinapelekwa maeneo mbalimbali zinauzwa na barabara zinajengwa chini ya kiwango.Mfano pale External wanauza kokoto michanga n.k lakini nyingi inatoka pale ubungo nk.

Nimeona hata magari yao yakipeleka vifusi kwa matajiri na tulipouliza uongozi wao wakasema magari hayaruhiwi kwenda mahali pasipo jengwa barabara.Kila leo haya yanaendelea na utashangaa wapo viongozi wanaona lakini hata viongozi wanashiriki kupata kitu kidogo sasa tutafika.Kama kweli tumedhamiria lazima wote tuungane na kusema basi.Wakati mmoja niliwaona wenzetu wajerumani kule kwao vijana wakipanda kwenye miti kuzuia ukataji ovyo miti uliokuwa ufanywe na serikali.Wakasema kama mnataka kufanya basi tukateni sisi na miti lakini hatushuki ngo.Mbona serikali ilitii na kuacha kufanya zoezi.

sisi tunaona mambo yanaenda ndivyo sivyo tunakaa kimya tunawangojea wapinzani waende bungeni huku wanachukua posho n.k mbona mengine sisi tunaweza.Ndio kuna miundo mbinu je umefanya nini kuzuia hiyo miundo mbinu isiharibike,au iwekwe n.k wananchi wanaona wananyimwa haki zao n.k ndio maana wanagoma na kuchafua zaidi au kujenga holela.

kwani hakuna mipango miji je wamezingatia hayo au kazi nikula hela na kutafuta posho ama vikao na kusafiri.Unakwenda jiji hakuna hhuduma wizarani ndio usiseme nani anafanya kazi ipasavyo.Ndio maana ukimleta Mkenya hapa nchini,Mnaigeria ama Mzungu utafanya tu kazi kwani wao si binadamu?watanzania tumelogwa na nani?wote tumebakia wanasiasa tu.Hebu jiulize hapo ulipo je humwibii mwajiri wako muda,hela n.k tumebakia wote kuwa wanasiasa ukienda katika ofisi ya serikali ya mtaa kijiji,halmashauri,wilayani,mkoani,wizarani kila mtu ni mwanasiasa.Anataka tu kuelekeza sasa mtendaji ni nani.

Tubadilike na mabadiliko yaanzie kwako huna wa kumlaumu.mimi na wewe tukubali kuwa wote tuna mahali tumeenda ndivyo sivyo.
Niliona Moshi mji ukiwa msafi kwa sababu haijalishi  wewe ni askari au mkulima au mita njia lakini wote ni walinzi kwa mwingine. Na sisi tuliwa na usalama mitaani hutakubali kujenga mahali ambapo hapastahili.Hutachafua mazingira.Utafuata taratibu zilizowekwa na hutamvumilia mtu yoyote anayekwenda kinyume hata kama ni boss wako.kweli itabakia kuwa kweli.

Mimi nimeanzisha kampeni za usalama mitaani.Na ninatamani uniunge mkono.Mahali ulipo waza kuifanyia kitu nchi yako kwa kuanza na wewe mwenyewe.
Penda kuwa wazi usimtegemee mtu kutoka ulaya kuja kukubadilishia wewe nchi.Utabadilisha wewe mtanzania na ujivunie kuitwa mtanzania mzalendo.Kama umepanga nyumba hebu angalia mazingira ya nyumba unayoishi.Je wewe kama ni kijana baba au mama je huwezi kuorganize angalau siku moja kwa mwezi kufanya kampeni ya usafi na kuweka mazingira safi katika nyumba yako chumba chako na mtaa wako?

je wakitokea watu watano mwezi ujao watakuwa kumi hadi n.k je hamwezi kupita na mafagio,hamwezi kuwa na dawa za kupulizia mbu,mazalia ya mbu hata kuchanga hela kidogo na kununua dawa na kufanya tu hapo unapoishi baadaye eneo na hata mtaa wako?

je huwezi kujitolea kwenda hospitali na kutoa hata mche mmoja wa sabuni kwa mama aliyejifungua,mgonjwa asiye na msaada n.k au watoto wanaohangaika mitaani n.k je huwezi hata kufanya lolote? je kumkemea afande anayechukua rushwa na wewe kutii sheria za barabara na kukataa kutoa rushwa ama kufuata taratibu zilizopo au kama wewe upo serikalini kuweka sheria na taratibu vizuri na kuhakikisha zinafuatwa bila kupenda kitu cha ziada wakati wewe unalipwa na mwajiri wako?

Ni lipi unaweza kufanya basi jaribu hata kama ni dogo kisha utafanya makubwa.Wewe kijana umesoma una ajira wakati wapo maaelfu ya vijana hawana kazi je huna hata wazo la kufanya.

Majirani zetu wako mbali vijana wanafanya mawazo yao kujulikana na kuyatendea kazi wanashiriki kwenye matamasha na makongamano.je wewe toka umalize chuo kikuu umefanya nini au unawaza serikali ikulishe chakula hadi mdomoni.

Wenzetu wanatamani ardhi yetu sisi hatuna hata mawazo ya kwenda kufanya kazi huko vijijini wote tunangangania mijini kisha tunasoma kisha itakuwaje kuna Online na e-learning now days  sio tatizo forums mbalimbali je mbona hatuna tofauti na wasiosoma.

Hebu tuwaze mambo kama wewe sio mwanasiasa hebu fanya mambo hebu usiwe msemaji bali mtendaji.Jipime mwaka hadi mwaka je umefanya nini wapi ulipo na wapi unaenda.

Muda unao usiwe ukaja jutia baadaye muda unao fanya unaloweza .chukua vijana baadhi wafanye wajitolee katika maeneo mbalimbali tafuta wenzako wachache kwa pamoja fanyeni kitu katika maeneo yenu kwa kufanya hivyo vijana wasio kuwa na ajira watajiajiri na kufanya mambo makubwa wasimamieni waelekezeni watawapenda sana baadaye.

ANZISHA HATA CLUB ya kujitolea fanya kitu.wajengee uwezo vijana na kwa kutumia elimu yako unaweza kuona wengi wakifaidika kwa wewe kuwepo usijidharau na kuona kwa vile uanakazi inatosha.

wafanye vijana waweze kufanya kitu hata kama ni internship kama unaweza fanya kitu sio lazima wawe madaktari hata hapo ofisini ulipo wanaweza kujifunza kitu







2014-03-28 11:00 GMT+03:00 Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com>:
Wananchi wafuate taratibu tu na wakubaliane na mipango ya maendeleo ya maeneo yao inayopangwa na serikali , nitaeleza machache .

- Serikali inataka kupanua barabara kuwe na misingi mikubwa ya maji na maeneo ya shuguli nyingine watu wanagoma zinapotokea mvua kama hivi wanaosubiri serikali , hata huko mitaani watu wamejijenga majumba na kuta ndefu bila vipimo sahihi .

- wafanyabiashara ndogondogo walitakiwa kuwa kwenye maeneo yaliyotengewa kwa ajili ya biashara zao , ni rahisi kupata huduma mbalimbali kutokea hapo na hata kupanga mipango mingine kuliko kuwa skatad .


On Friday, March 28, 2014 10:45:59 AM UTC+3, lesian mollel wrote:
Mvua kubwa inaendelea kupiga/kunyesha maeneo yote hapa jijini, changamoto kubwa iliopo nadhani wengi tuishioa hapa twaijua, tuna miundombinu mibovu sana ya maji na bara bara kati kati ya jiji, kwa leo mjini kwenda ni tatizo kwani magari hayatembei na wale watembea kwa miguuu wawe na pesa za nauli ya ziada za kubebwa kuvushwa ktk madimbwi makuubwa.
hatar sana dar mvua ikinyesha, sjui maeneo ya mabondeni leo hali yao ikoje? sjui wale wafanyabiashara ndogo ndogo wanaopanga bidhaa zao chini, ni vurugu tupu mvua ikinyesha dar
nini kifanyike kuondoka kero hizi? serikali, wakaazi na wafanyabishara, nini kifanyikie, au tupeleke ktk bunge la katiba nalo hili maana sku hizi mtu akiibuka tu, oooh peleka Dodoma

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--
"In accepting the trusteeship of our wildlife we solemnly declare that we will do everything in our power to make sure that our children's grand-children will be able to enjoy this rich and precious inheritance."- Dr. Julius K. Nyerere

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment