Saturday, 7 July 2012

[wanabidii] Ziara ya waziri Mkuu Songea na Tatizo la Umeme

Mheshimiwa Waziri Mkuu amekuwa na Ziara hapa Songe tokea jana 6 July 2012, Wakati Mji wetu ukiwa bado na lile Tatizo sugu la Ukosef wa Umeme na maeneo mengi kuwa Gizani  katika maeneo mengi ya Municipal Na bila Taarifa yeyote kutoka Shirika la Tanesco kwa nini Hakuna Umeme meneo mengi.
 
Je Viongozi wetu wa Wilaya ya Songea Municipal wameshirikisha tatizo hili Waziri Mkuu au wameendela kumueleza kila kitu kipo Shwari.
 
Napenda kufahamu kutoka kwa Viongozi wetu na kwa nini tatizo hili limekuwa sugu na wala wakazi hatupewi taaraifa zozote. Shgui nyingi za Kiuchumi za waazi wa Songea zimekuwa katika hali mbaya sasa kwa miaka mingi Kutokana na tatizo hili la Umeme na Kwa kiasi kikubwa kupotea kwa Pato la taifa.
 
Napenda Ufananunuzi kama kuna Viongozi wetu katika mtandao huu.

--
CoDeC Africa
Community Development Consultants
P.O.BOX 52
Songea
Tanzania

codec.africa@gmail.com
Tel +255 787 010797

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment