Ahsenteni, kwa maelezo ya mtu aliyeona madhila, kwa nafsi yake, na kuamua kutueleza.
Uzuri wa huriya ya maoni na fikira ni kusaidiana tujenge muelewano bora na kutambua
ya KWELI na ya UZUSHI.
Kuzuia mazungumzo sio dawa ya kutoa UTATA.
KIZA huondoshwa na MWENGE!
Bwanatosha

> Date: Sun, 8 Jul 2012 02:33:07 -0700
> From: hamisznz@gmail.com
>
> Utangulizi
>
> Sheikh wa kwanza kudhalilishwa na serikali ya Tanzania alikuwa Mufti
> wa Tanzania kwa wakati ule Sheikh Hassan bin Amir ambae kwa amri
> iliyotolewa na Julius Nyerere alikamatwa nyumbani kwake usiku wa
> manane akiwa kavaa khanga tu na akachukuliwa hivyo hivyo hadi uwanja
> wa ndege na kurejeshwa "kwao" Zanzibar. Kisa cha yeye kufukuzwa Bara
> ni kirefu na kwa sasa hapa si mahali pake kueleza. Nimekiweka kisa cha
> Sheikh Hassan bin Amir mwanzo kwa kuwa kina nafasi ya pekee katika
> historia ya Waislam na mapambano yao na serikali toka uhuru upatikane
> mwaka 1961. Lakini mwaka wa 1964 masheikh wengi waliwekwa kizuizini
> kwa amri ya Nyerere hiki nacho ni kisa kingine kinachohitaji wakati
> maalum kuhadithiwa. Baada ya haya ndipo kwa mara ya kwanza moto wa
> makumbi ukajitokeza juu na Waislam wakapambana na serikali katika
> mitaa ya Dar es Salaam mwaka 1993 na mabomu ya machozi na risasi
> zikapigwa. Haya ndiyo yalikuwa maandamano ya kwanza kufanywa na
> Waislam baada ya uhuru. Hili lilikuwa sakata la kuvunjwa mabucha ya
> nguruwe. Damu ya Waislam ilimwagika. Masheikh kumi na moja wa Wilaya
> ya Kinondoni walikamatwa pasi na adabu usiku wa manane majumbani mwao,
> wakapigwa pingu na kutupwa katika malendrova ya polisi kama majambazi.
> Lakini haya yote si kitu tokeo lililotokea siku ya Jumatano tarehe 4
> Julai lilifurtu ada. Sheikh Nurdin Kishki akiwa na ugeni wa masheikh
> wenzake kutoka Yemen ndani yao akiwapo Mufti wa Yemen walivamiwa na
> askari waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia wakiwa njiani wakitokea
> Tanga na wakagaragazwa chini huku wakionyeshwa mitutu ya bunduki. Hii
> ilikuwa habari kubwa lakini vyombo vyote vya habari kama ilivyo ada
> kwa mambo yanayowahusu Waislam vyombo vyote muhimu vilipuuza stori
> hii.
>
> Baada ya utangulizi huu naeleza kisa kilichonifika mikononi mwa vyombo
> vya dola miaka sita iliyopita:
>
> Mkasa Wangu wa Kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Mwl. Nyerere, Dar es
> Salaam Mwaka 2006
>
> Mohamed Said
>
> "Mwaka 2006 Radio Tehran walipendekeza jina langu rehekwa Wizara ya
> Mambo ya Nje Iran wanialike katika hawli ya Imam Khomeni. Sababu ya ya
> mie kualikwa ni kuwa mara kwa mara nilikuwa nikifanya mahojiano na
> Radio Tehran Idhaa ya Kiswahili kuhusu siasa za Tanzania hususan
> wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 na ikatokea kuwa yale mahojiano
> yangu yakawa yanapendwa na wasikizaji wa Afrika ya Mashariki na Kati
> na sehemu za Emirati. Nilkwenda Iran na waalikwa walikuwa kutoka dunia
> nzima na wa kila aina, waandishi, wahadhiri wa vyuo vikuu, wasomi wa
> kawaida, mawaziri wa serikali kutoka nchi tofauti na watu wengine
> wengi. Msafara wetu wa wageni kwenda mahali ulikuwa ni msururu wa
> mabasi zaidi ya kumi yakisindikizwa na kimulimuli cha polisi. Kutoka
> Tanzania nilikuwapo mimi pamoja na waandishi kutoka Daily News na
> Kituo Cha TV cha Channel Ten. Nikiwa Tehran niliingia studio za Radio
> Tehran Idhaa ya Kiswahili na tukafanya mahojiano na mtangazaji wao
> mashuuri Abdulfataa Mussa na wenzake na vilevile kurekodi vipindi
> vingi kuhusu hali ya Waislam Tanzania.
>
> Mambo yalianza wakati sasa narudi Dar es Salaam na ndege ya Emirates
> iliyokuwa inatua usiku. Inaelekea maofisa wa pasi pale uwanjani
> walikuwa na taarifa zangu mapema na walikuwa wakinisubiri kwa hamu
> kubwa kwani nilipotoa pasi yangu kwa afisa wa pasi hapo ndipo shughuli
> za kunishughulikia zilipoaanza. Mimi sikuwa na hili wala lile. Nikawa
> namuona yule dada aliyekuwa kwenye kile kizimba akikukurika na pasi
> yangu akiitia katika mashine na kuitoa mara kadhaa. Fikra iliyonijia
> kwa haraka ilikuwa mashine ni mbovu na harakati zile zilikuwa ni
> kurekebisha mitambo. Kumbe sivyo wahusika nadhani walikuwa
> wanahakikisha kuwa mimi ndiyo huyo waliokuwa wakimwinda na kumsubiri
> na sasa kapatikana, kaingia mwenyewe kwenye mtego na kanasa. Yule
> afisa wa pasi akanambia nikae pembeni natakiwa kwa mahojiano na watu
> wa usalama. Hofu haikuwa imeniingia kwa kuwa nilikuwa natambua kuwa
> harakati dhidi ya ugaidi zilikuwa zimepamba moto na labda nilitakiwa
> kwa mahojiano mafupi kutaka kujua nyendo zangu. Sikujua wala kutarajia
> kuwa mshtuko mkubwa ulikuwa unanisubiri.
>
> Nilichukuliwa hadi kwenye chumba kimoja na hapo niliwakuta maofisa wa
> usalama watatu wakanikaribisha kwa taadhima kisha wakanambia kuwa niko
> chini ya ulinzi kwa kuwa zimewafikia taarifa zangu kuwa mimi
> nasafirisha mihadarati. Mpaka hapa sikuwa na hofu bado ilinijia picha
> kuwa yawezekana wamefananisha majina. Niliwaambia huenda Mohamed Said
> muuza madawa ya kulevya siyo mimi niliye mbele yao. Wakaniambia kwa
> kujiamini kabisa kuwa taarifa zao ni madhubuti muuza unga ni mimi na
> wamekuwa wakinifuatilia siku nyingi. Hapo ndipo walipotoa pasi yangu
> na kuniomba niitambue kama hiyo pasi ni yangu au la. Niliwajibu kuwa
> hakika hiyo ndiyo pasi yangu khasa. Wakaniamuru sasa tutoke twende
> nikachukue mizigo yangu ili wafanye upekuzi wa mihadarati katika
> mizigo niliyotokanayo Tehran. Hapo ndipo nilipojuwa kuwa niko katika
> lindi kubwa la matatizo na ubongo wangu ukaanza kufanya kazi kwa
> haraka huku nikosoma dua kumuomba Allah ulinzi wake kwani kwa hakika
> nilijua kama ni njama zimekamilika na leo imefika siku yangu.
> Nikajiuliza itakuwaje watakapotoa madawa kwenye mizigo yangu. Nikaanza
> kufikiri vichwa vya habari vya magazeti yatakavyopambwa na habari
> zangu. Ikanijia yakini kuwa watu wa usalama wameniwekea madawa ya
> kulevya katika mizigo yangu ili waniangamize na maadui zangu wapumzike
> na shari yangu.
>
> Nilimgeukia yule ofisa mkuu aliyekuwa ananihoji nikamwambia kuwa
> sitokubali kugusa mizigo yangu bila kuwapo mashahidi isijekuwa mizigo
> yangu ishawekewa hayo madawa ya kulevya kwani nilikotoka mizigo
> ilikuwa imekaguliwa na ilikuwa salama. Hoja yangu kubwa kwao ilikuwa
> kupata uhakika kutoka kwao kuwa wananijua vizuri kiasi cha
> kuthibitisha kuwa kweli mie ni msafirishaji wa madawa ya kulevya. Jibu
> nililopewa ni kuwa wao wanafanya kazi kutokana na taarifa
> zilizowafikia. Wakasema, "Sisi tunazo taarifa zako kamili kuwa wewe ni
> msafirisha madawa ya kulevya." Nikawauiza, "Baada ya kupata taarifa
> hizo zangu nyie mmechunguza kutafuta ukweli?" Wakasema, "Ndiyo maana
> leo tumekukamata." Nikawaambia, "Si kweli kama kwa sababu mie
> nafahamika Dar es Salaam takriban kwingi maana ndio nilikozaliwa na
> kukulia. Hapo Kariakoo ukiwaambia watu kuwa Mohamed ni "Mzungu wa
> Unga" kila mtu atacheka maana huo kwao ndugu zangu ni mzaha mbaya."
> Walitaka kujua nilkwenda kufanya nini Iran. Niliwaambia nilialikwa na
> serikali ya huko kuhudhuria mkutano. Wakataka kujua vipi nilipata
> mwaliko. Nikawajibu kuwa hilo swali sina jibu labda waiulize serikali
> ya Iran. Nikawaeleza kuwa mbona siku zote napita hapo uwanjani nikenda
> sehemu tofauti duniani kwa mialiko na kutoa mada sijakamatwa kimezidi
> nini katika hii safari ya Iran? Niliwaeleza kuwa miezi michache
> iliyopita nilikuwa Chuo Kikuu Cha Ibadan kwa mwaliko tena mkutano
> umefadhiliwa na serikali ya Amerika na wamenipa na tiketi toka Dar es
> Salaam hadi Lagos na kuniweka hoteli na kunilipa fedha. "Mbona
> hamkunikamata wakati ule?" Ikawa swali na jibu swali. Nikafungua
> mlango mwingine nikawaambia, "Nakuapieni nyie msingethubutu kumkamata
> Mkristo anaetoka Vatican mkutanoni. Lakini kwa kuwa mie ni Muislam
> sina wa kunitetea. Nchi hii nani atakuuliza kwa kumnyanyanyasa
> Muislam?" Walishtuka na wakawa wanyonge sana wakasema si kweli kuwa
> naponzwa na dini yangu.
>
> Baada ya kukurukakara nyingi na mabishano makubwa kuhusu mie kukubali
> kufanyiwa upekuzi wa mizigo yangu alikuja binti mmoja katika wao na
> yeye akanihakikishia kuwa wao ni serikali na sio wahuni. Hawathubutu
> kuniwekea dawa katika mizigo yangu hivyo akanisihi sana kwa upole
> nikubali ili wajitoe wasiwasi na wataniachia endapo hakuna kitu.
> Niliomba apatikane shahidi wa kushuhudia mizigo yangu kabla ya
> kufanyiwa upekuzi lakini hakuna mtu aliyekubali kuchukua dhima ile
> katika maofisa waliokuwa kazini pale uwanja wa ndege usiku ule.
> Upekuzi ukafanyika hadi mwilini. Hakuna kitu. Wakanipela katika choo
> maalum cha kutolea madawa kwa njia ya haja kubwa. Nikakataa kujisaidia
> pale. Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuona choo kama kile. Choo
> chenyewe ni cha aluminium. Tofauti na vyoo vya pale ambavyo siku zote
> ni vichafu, hiki kilikuwa kisafi sana kiasi mtu unaweza hata kutengewa
> chakula na akala bila ya kuhisi kinyaa.
>
> Nilitegemea wataweka ahadi yao kuwa ikiwa hawatakuta madawa ya kulevya
> katika mizigo yangu watanirejeshea uhuru wangu wataniachia niende
> nyumbani. Haikuwa hivyo. Wakanirudisha ofisini kwao. Sasa wakaacha
> madawa ya kulevya wakahamia katika vitabu na "audio cassette"
> nilzokuwa nimepewa kama zawadi kule Tehran wakaniluliza kwa nini
> naingiza vitu vile khasa kanda za Khomeni na vitabu vyake nchini.
> Nikawauliza, "Kwani kanda na vitabu vya Khomeni haviruhusiwi kuingizwa
> Tanzania? Maana mimi hata nyumbani kwangu hii leo mkifika nina vitabu
> vya Khomeni na wanafalsafa wengine kama Karl Marx ambao nimesomeshwa
> pale Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam." Sasa hapo ikaja kejeli. "Ala wewe
> mtu wa Kariakoo lakini umefika hadi Chuo Kikuu!" Sikujibu kitu. Awali
> waliponitia mbarani waliniuliza kwetu na nikawaeleza kuwa nimezaliwa
> Kariakoo.
>
> Hawakunipa jibu kuhusu kuingiza vitabu na cassette za Khomeni. Ikawa
> sasa kama vile wameishiwa maswali. Nikaona kuwa sasa ni zamu yangu
> nami kuwapiga maswali. Yule aliekuwa akinihoji nikamwambia, "Mimi wewe
> nakufahamu vizuri sana kwa sababu ukicheza mpira Simba Sports Club na
> mie ni mpenzi wa club hiyo toka utoto wangu wakati huo ikiitwa
> Sunderland na mmoja wa baba zangu alikuwa mchezaji marufu wa club hiyo
> katika miaka ya 1950 akafiikia hadi kucheza Kombe la Gossage."
> Nilihisi amepata mfadhaiko kidogo akanambia,"Unanifananisha yule
> aliekuwa akicheza Simba ni ndugu yangu." Alikuwa anasema uongo lakini
> mie nikamkubalia. Hapo nikajua kuwa nishampata sasa hana nguvu tena ya
> kuuliza maswali. Kusema uongo ni dalili ya kujihami. Nikamrushia
> kombora lingine, "Sasa tuhuma za madawa ya kulevya zimekwisha tuko
> katika kwa nini naingiza vitabu vya Khomeni nchini?" Akanijibu
> kinyonge, "Tumeridhika huna madawa." Kufika hapa tukawa tumemaliza
> mahojiano.
>
> Wakati huo sasa ni usiku wa manane na nishapeleka SMS kwa sahib yangu
> mmoja bingwa wa mambo ya mtandao wa kompyuta kumjulisha kuwa
> nimekamatwa uwanja wa ndege kwa tuhuma za uongo za kuvusha mihadarati
> na yeye ile kuipata tu ule ujumbe wangu akaifahamisha dunia kuwa
> nimekamatwa uwanja wa ndege nikitokea mkutanoni Iran na
> nimebambikiziwa tuhuma za kuingiza nchini mihadarati. Waliponitia
> mbaroni tu walinionya kuhusu kutumia simu yangu ya mkononi lakini
> bahati nzuri hawakuninya'ganya. Aliyenipa onyo hili alikuwa mkuu wa
> kituo cha polisi cha uwanja wa ndege. Huyu rafiki yangu akawa
> kanisaidia sana maana hadi kumekucha wapenzi wangu wote ndani na nje
> ya nchi pamoja na vyombo vya habari vinavyonifahamu walikuwa na
> taarifa za kukamatwa kwangu. (Kwa kipindi takriban miaka ishirini
> nyuma kwa nyakati fofauti nimekuwa nikifanya mahojiano na radio zote
> muhimu kama, BBC, VOA, Sauti ya Ujerumani, Sauti ya Iran nk.).
>
> Nikawaomba wale watu wa Usalama waniachie basi nende zangu kulala
> nyumbani nirudi hapo kesho asubuhi kwa kuwa sikuwa nimebeba madawa ya
> kulevya. Wakaniambia, "Itabidi tukulaze hapa hadi asubuhi wakubwa wetu
> watupe amri ya kukuachia. Maana amri ya kukukakamata wewe imetoka
> juu." [IMG]file:///C:/Users/MOHAME~1/AppData/Local/Temp/
> msohtmlclip1/01/clip_image001.gif[/IMG]Sasa hapo ikawa nimelipata
> jingine. Kumbe wauza unga hawakamatwi hadi amri itoke juu. Sasa kama
> amri haikutoka ndiyo muuza unga atapita aingize sumu zake mitaani?
> Hili likazidi kunidhihirishia kuwa kukamatwa kwangu hakukuwa na
> uhusiano wowote na vita dhidi ya mihadarati bali ni vita vile vile
> vikongwe dhidi ya Uislam.
>
> Nikawa pale usiku kucha. Sasa wakati niko pale wakidhani nimelala.
> Wakawa wenyewe kwa wenyewe wanazungumza kuhusu hii 'operation' neno
> walilotumia ni kuwa 'leo tume-dial wrong number.' Wakawa wanasema,
> "Huyu bwana mbona hakuelekea kama muuza unga tena huyu mtu bwana
> kasoma kweli kweli" Wanadhani mie nimelala kumbe ni macho
> nawasikiliza. (Vipi utalala katikati ya michongoma?). We umeona jinsi
> alivyokuwa akijibu na kuchambua mambo." Hilo ndilo likawa gumzo lao
> wakinisifia kwa ufasaha na mantiki lakini wakizungumza kwa sauti ya
> chini kabisa. Hapa ikanidhihirikia kuwa hawa vijana walikuwa
> wanatimiza wajibu wao wa kazi tu lakini kiini khasa cha kukamatwa
> kwangu hawakuwa wanakifahamu.
>
>
> Walionikamata walikuwa vijana kama wanne na wote walijitambulisha kwa
> majina ya Kiislam. Nilijua ni waongo kwa kuwa Muislam anonekana katika
> uso na katika matumizi ya lugha. Lakini yule mchezaji wa Simba ni
> Muislam na yeye ndiye aliekuwa mkubwa pale akiongoza ile shughuli yote
> tena kwa kujidai na kujifaharisha sana. Kisa kile kile cha mtumwa
> anelimishwa na yule anefanya kazi za ndani nyumbani kwa bwana. Ila
> kitu kimoja lazima nikiri. Wale vijana walikaa na mimi kwa wema na
> hawakunibughudhi hata kidogo. Hata nilipokuwa nakwenda msalani kijana
> alienisindikiza alinitaka radhi akasema, "Nakusindikiza kwa sababu ni
> sheria lakini sisi tunakustahi kwa hiyo utuwie radhi kwa kukufuta hadi
> msalani."
>
> Asubuhi wakubwa wakaja kazini lakini hakuna alienikabili. Walikuwa
> wakinichungulia kutoka mlangoni kama simba ndani ya kizimba kwenye
> zoo, nami nikawa najifanya siwaoni. Ndipo akaja mkubwa mmoja tena
> akaniita kwa jina langu na kwa heshima na bashasha sana, "Bwana
> Mohamed tuwie radhi sana pamekuwa na makosa kidogo tuwie radhi sasa
> hivi tutakuruhusu uende nyumbani. " Akatoka nje akawa akipiga simu.
> Kisha akarudi ndani akaamrisha nibebewe mizigo yangu na gari la polisi
> linirudishe nyumbani. Kistaarabu kabisa nikakataa gari ile huku
> nikifanya maskhara kuwa naogopa gari ya polisi asijepiga simu akasema
> mrudisheni huyo mtuhumiwa. Ofisi nzima ikacheka. Hapo ndipo wale
> wakamataji wangu wa usiku wakabeba mizigo yangu nami nafuata nyuma
> tunatoka nje ya uwanja.[IMG]file:///C:/Users/MOHAME~1/AppData/Local/
> Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.gif[/IMG]
>
> Kilichobaki sasa ni kueleza sababu ya mimi kukamatwa. Mwaka wa 2006
> Chuo Kikuu cha Ibadan, Nigeria kilifanya kongamano la kimataifa hapo
> chuoni kwao kuzungumza kuhusu Ugaidi katika Afrika ya Mashariki na
> Maendeleo ya Afrika (Conference on Islam, Terrorism and African
> Development). Mimi ninlitoa mada iliyokuwa na anuani hii: Terrorism in
> East Africa the Tanzanian Experience. Katika mada hii nilijikita
> mahsusi katika kuisema Marekani kwa udhalimu wao duniani. Nikaeleza
> kuwa huo udhalimu wao ndiyo unaopelekea wao kuchukiwa dunia nzima.
> Hapa ningependa kufahamisha kuwa mkutano huu wafadhili wakubwa
> walikuwa Iran na Marekani. Saudi Arabia ilikataa kuchangia mkutano
> ule. Wakati nasema maneno haya ya kuwakanyaga wenyewe Waamerika wapo
> hapo mkutanoni.
>
> Baada ya kuwalani Waamerika sasa nikaigeukia serikali ya Tanzania na
> kuishutumu vikali kwa kupitisha Sheria ya Ugaidi. Hapa nikaeleza kuwa
> Waamerika wasione kuwa Tanzania imepitisha sheria hiyo ya ugaidi kwa
> haraka kwa sababu Tanzania ina tatizo na ugaidi. Nikaeleza kuwa sheria
> hiyo imepitishwa kwa sababu Bunge la Tanzania limehodhiwa na Kanisa na
> kupitishwa kwa sheria hiyo hakuna uhusiano wowote na ugaidi ila
> Wakristo wamepata fursa ya bure ya kupambana na Uislam wakitumia
> serikali ya Marekani kama upawa wao wa kuopolea chinyango ya moto
> kwenye chungu kinachotokota. Nikauchekesha mkutano kwa kuwaambia kuwa
> Wamarekani wamefanywa wajinga na Kanisa kwa kuchonganishwa na Waislam
> wa Tanzania ambao hawana ugomvi nao asilani. Baada ya kusema hayo
> nikahitimisha kwa kueleza nguvu ya Waislam Tanzania, kwanza kwa wingi
> wao na kisha kwa historia yao iliyotukuka iliyodumu takriban miaka mia
> wakipambana na ukoloni wa Wajerumani kwa silaha (1905 1907), kisha
> ukoloni wa Waingereza (1929 1961) na kuhitimisha kwa kuleta uhuru na
> kuanzia 1961 hadi sasa wanapambana na nguvu ya kanisa katika kupiga
> vita Uislam.
>
> Kufikia hapa ukumbi ukawa umepata joto. Wanigeria wamesimama kutaka
> niwaeleze vipi Waislam watakuwa wamepigania uhuru kisha wako wengi
> nchini wanaruhusu wao kufanywa raia daraja la pili. Wakashangazwa kuwa
> hata historia ya mashujaa Waislam waliopigana Maji Maji na kunyongwa
> na wakoloni na mashujaa walipigania uhuru wa Tanganyika hawatajwi
> katika historia ya ukombozi. Nilitoa majibu kadri Allah
> alivyoniwezesha. Nakumbuka kitu kimoja walichosema wale ndugu zetu
> Wahausa. Walisema hali hiyo iliyoko kwenu haiwezekani kutokea Nigeria
> kwa kuwa hiyo itakuwa na sawa na kutangaza vita. Kisha
> wakanihakikishia kuwa sheria hiyo ya ugaidi haitapitishwa Nigeria hata
> siku moja.
>
> Wapashaji habari wangu wakajanieleza baadae ni hili hitimisho langu
> ndilo lililosababisha Wamarekani kuleta taarifa Dar es Salaam kutaka
> taarifa zangu za "ugaidi" ikawa sasa sababu imeptikana ya mimi
> kushughulikiwa na vyombo vya dola. Ndipo ikatengenezwa hadithi ya kuku
> jike na ng'ombe dume (cock and bull story) kuwa Mohamed Said ni Mzungu
> wa unga kwa hiyo akamatwe.
>
> Mkasa huu ulinifika miaka sita iliyopita lakini hadi leo kovu la mkasa
> ule limebaki katika pasi yangu. Sielewi pasi yangu inaonyesha nini
> inapotiwa katika compyuta baada ya mkasa huu kwani kama mara tatu
> husimamishwa kwa muda na kuombwa nitoe maelezo ya ziada kuhusu
> niendako kila nisafiripo nje ya Tanzania. Nimeshuhudia hali hii Uwanja
> wa Ndege Amsterdam na Detroit, Marekani. Berlin, Ujerumani niliambiwa
> mzigo wangu umepotea lakini hata kabla sijatoka uwanjani nikatafutwa
> na kukabidhiwa mzigo wangu na kwa hili sikuwa peke yangu nilikuwa na
> mwenzangu, jamaa wa Kiarabu kutoka Misri. Sijui kama mizigo yetu
> ilikuwa imebakishwa nyuma kwa upekuzi zaidi. Amsterdam, Uholanzi baada
> ya kupita sehemu zote muhimu za upekuzi wakati naelekea kituo cha
> mwisho niingie kwenye ndege inayoelekea Detroit, Marekani
> nikachopolewa kutoka kwenye mstari na nikawekwa pembeni peke yangu kwa
> usaili wa ziada. New York kadi yangu ya benki ilikataa kutoa fedha kwa
> siku nzima hadi siku ya pili. Nilikujafahamishwa baadae kuwa "system"
> ilikuwa inanichunguza kwanza. Ilikuwa siku ya pili baada ya kuonana na
> maofisa wa benki ndipo kadi yangu ikaanza kutoa fedha. Geneva, Uswisi
> kadi yangu ilikataa kutoa fedha katika mgahawa. Sikujua kama ni yale
> yale au haya yalikuwa mengine. Lakini pasi hii afisa wa uhamiaji wa
> Tanzania alipoiingiza kwenye compyuta yake alimwita mwenzake kuja
> kutazama kisha wakawa wanacheka. Waliona nini kwenye pasi yangu Allah
> ndiye ajuaye."
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:
Post a Comment