Monday, 9 July 2012

Re: Fw: [wanabidii] Waraka wa Lema kwa JK

Ukisoma waraka wa Lema kiushabiki ni wazi huwezi kugundua mambo ya msingi ambayo Lema anayaamini na kutokuyatilia shaka. Jambo la pili ni kuwa Lema ameandika waraka huu kwa mtu ambaye bila shaka hawezi kushtushwa na yaliyomo kwa kuwa anayafahamu. Hata ukisikiliza badala ya kuusoma utaisikia tone ya Lema ni ya mtu anayewasilisha jambo analolifahamu kwa mtu ambaye si mgeni wa kinachoelezwa.

Pengine Lema kwa makusudi ameacha kudisclose chochote kuhusu mkutano wa Oysterbay kwa kuwa aliamua kuubinafsisha waraka huo kwa mlengwa japo ameufanya kuwa public document. Taarifa za lengo na maudhi ya mkutano alioutaja Lema haviwezi kwa mtizamo wangu kutumika kama turufu ya kuuamini au kutokuuamini waraka huu. Waraka unajitosheleza wenyewe na kama watu wakiusoma kama mwl.Lwaitama alivyosema- 'between the lines ' ni wazi kuwa uzito wa kilichosemwa utaonekana.

Nionavyo mimi Lema anaupa umma kazi ya kufanya katika kipindi hiki ambacho serikali inatumia nguvu kubwa sana kupambana na nguvu ya mabadiliko kuliko kupambana na maadui wa maendeleo. Kazi anayoupa umma ni kuamua hatma ya maisha yao wao wenyewe sasa na kuacha kupambana na adui wasiyemjua. Amemuweka wazi adui wa ustawi wa taifa kuwa ni mfumo mbovu hatarishi wenye sura ya kiimla uliotaifisha mamlaka,haki na stahiki za raia na kuzifanya kuwa miliki za wachache. Lema halalamiki wala hajakata tamaa. Ameandika HATI ya mapambano na anachosubiri ni walengwa wa vita hii wapokee na kusoma hati ya mashtaka ili hali umma ukiandaliwa kupigania haki na mamlaka yao. Hii siyo vita ya kificho kama waraka huu usivyokuwa wa kificho

On Jun 4, 2012 12:40 PM, "Fred Alphonce" <fredrick197958@yahoo.com> wrote:


Ndungu zanguni nimeupata waraka huo....Source Jamii Forum...


IKULU ILIINGILIA KESI YA UCHAGUZI. – GODBLESS LEMA.

"Ndugu Wananchi;


Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo . ( J.K . KIKWETE.)

"Narudia tena , IKULU iliingilia kesi yangu ya Ubunge".

Mh Rais nimekusikiliza kwa makini sana ila nakupa pole kwani bado unafikiri unaongea na Tanzania ya mwaka 1961 , umesema sasa Arusha ni shwari tofauti na miaka miwili iliyopita kwani sasa kuna amani na utulivu wa kutosha ndio maana hata mkutano wa AFDB umefanyika Arusha . 

Mh Rais , najua IKULU iliingilia kesi yangu kama ilivyoonekana na ndio sababu hata Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati anaapisha Wakuu wa Wilaya alimpongeza Jaji kwa hukumu nzuri aliyowafurahisha wakati kesi hiyo iko mahakama ya Rufaa , lakini jambo moja la msingi ambalo huwezi kulitambua kwa sasa ni kuwa Haki na Ukweli haviwezi kushindwa na dhuluma, ubaya wala mamlaka , natambua wewe ni Rais na unayo mamalaka makubwa katika Taifa hili lakini vile vile nataka utambue kuwa huna mamlaka makubwa dhidi ya haki , utu na ukweli.

Mh Rais hakuna Amani Duniani inayozidi Haki na usawa ,utu na ukweli , haipo na wala haitakuwepo , ndio maana kila siku nasema ni"Afadhali Vita Inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu"umefurahia sana mkutano uliokupa fursa ya kutoa maneno ya kebehi na kudhihirisha ila chafu iliyofanywa na Serikali yako na kujaribu kuhadaa Umma kama ilivyo kawaida ya Serikali yako na Chama chako. Hata hivyo wakati huu kuna mambo ya msingi yakushughulikia zaidi ya kebehi na hadaa, Uchumi wa Nchi umeyumba, huduma za msingi za jamii zimepuuzwa, Mpasuko katika suala la Muungano na vururugu zinazoendelea Zanzibar, mfumuko wa bei hizi ni sababu chache ambazo haziwezi kuruhusu wakati huu kuwa wakati wa kebehi na mizaha isipokuwa kazi .

Mh Rais, Mama Theresa, Nelson Mandela, Martin Luther Jr na Malcom X hawakuwa Wabunge kupigania haki za Nchi yao na watu wao. Sihitaji Ubunge kupigania ukweli, haki na utu, nahitaji dhamira safi, nia njema na huu utakuwa wajibu wangu mpaka nakwenda kaburini, nitakapomaliza mbio hizi najua nitapata fursa ya kutazama nyuma yangu nione nini nilifanya. Ukweli nisingependa kuona vituo vya mafuta, magorofa, magari na viwanja vingi kila kona ya Nchi bali Haki, Usawa na utu vikiwa kama nguzo ya imani ya watawala wetu watakaokuwepo. Pengine sitaishi miaka mingi sana kama utachukizwa sana na waraka wangu huu kwani Polisi, Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi wanakutii wewe, hata hivyo siogopi kufa kwani nisipokufa kesho, nitakufa siku moja ambayo siijui, napenda kuishi maisha marefu nimwone mke wa mtoto wangu kama itawezekana, lakini kuliko iwezekane kwa kuishi kwa hofu ni bora ishindakane kwa kuthamini haki. Kwa hiyo kama utakuwa umekasirika sana, unaweza kufanya jambo lolote baya kwa kutumia mamlaka yako, niko tiyari sio kesho wala leo isipokuwa sasa hivi, najua IKULU imewazulumu watu wa Arusha Mbunge wao.

Mh Rais ninajua wazi njama zote na hasira hizi zinaweza kuwa zimetokana hasa na mkutano tuliokaa Osterbay Dar mimi na wewe kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hata hivyo sikupuuza maongezi yetu isipokuwa nilichagua kufuata dhamira yangu na wito wangu wa utumishi wa kweli katika Jimbo langu na Nchi yangu.

Mh Rais nimekuelewa na Wananchi wamekuelewa kila mahali , wewe ni Rais unayo mamlaka makubwa na mimi ni mwananchi mamlaka yangu makubwa ni kwa mke wangu tu , sina Polisi wala Usalama wa Taifa lakini nitawaomba wanyonge wafunge na kusali tuone kama mamlaka yako inaweza kushindana na haki na ukweli .

Mh Rais "Mtu anaweza kuzini kwa siri lakini hawezi kuugua ukimwi kwa siri" Serikali na Chama cha Mapinduzi kimepuuza watu na haki zao kwa muda mrefu , lakini wakati umefika ambapo hawatapuuzwa tena hata hivyo kwa kauli yako hii naamnini haiwezi kuwafundisha kazi majaji wa mahakama ya rufaa .

"ONLY TIME WILL TELL".

GODBLESS .J. LEMA.
 

----- Forwarded Message -----
From: Fred Alphonce <fredrick197958@yahoo.com>
To: wababidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, June 4, 2012 12:23 PM
Subject: [wanabidii] Waraka wa Lema kwa JK

Habari ya mchana,
Aliefanikiwa kuuona waraka wa Lema kwa Mhe. Kikwete atuwekee hapa jukwaani tusome tupate kujua alichokisema kwa ujumla wake pia tudadii kuona relevance ya kile alichokiandika.

nimesoma kwa ufupi quote moja wapo katika moja gazeti la leo.

Wasalaamu
Fred 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment