1. Maalim Seif kutumbua jipu leo
Hii ni habari inayopewa nafasi ya kwanza na mtandao wa mjengwablog.com.Maalim Seif ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Katika sintofahamu iliyopo sasa kwa muda mrefu hajanukuliwa akitoa kauli. Tayari msimamo wa CCM Zanzibar umefahamika, kuwa wako tayari uchaguzi urejewe. CUF wao wanasikika wakiweka msimamo kuwa wao ndio washindi, watangazwe tu.
Katika hili wa kutangaza hilo ni Tume, na ni Tume hiyo hiyo iliyoyafuta matokeo na maamuzi kuchapwa kwenye gazeti la Serikali. Hilo likitoa tafsiri kuwa Tume haiwezi katika mazingira ya sasa kuyapitia upya maamuzi ambayo inadai yamefanyika kisheria.
Maalim Seif kwa kuongea na Wahariri leo anamtangulia njiani Dr Shein kwa hotuba yake ya kesho kwa Wazanzibar kupitia maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi. Kauli ya Maalim Seif leo itatoa mwanga wa Wazanzibar wanakokwenda.
Tumepata kulitolea maoni hili, kuwa, katika mazingira ya sasa, hekima na busara ikitangulizwa, hakuna namna yeyote ile nyingine kwa Wazaznibar kusonga mbele bila kukubaliana kwa pamoja, kuwa wanarejea uchaguzi chini ya taratibu na uangalizi usio tia mashaka ya pande mbili kuchezeana rafu mbaya. Matokeo ya uchaguzi kwenye uchaguzi huo lazima yaheshimiwe na pande zote mbili na yatapelekea kuunda Serikali nyingine ya Umoja wa Kitaifa, maana, kwa Zanzibar ilivyo sasa, na kwa Katiba yao mpya inavyoruhusu, muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa- GNP ni tiba mujarab kwenye yenye kuwasibu Wazanzibar.
2. Ukifanya hivi hutabomolewa nyumba yako..
Gazeti Mwananchi limekuja na habari ambayo sisi wa mtandao waMjengwablog.com tunaipa nafasi ya pili kwa ukubwa. Inaelezea hatua ambazo mtu akizizingatia, hawezi kubomolewa nyumba yake.
3. Waraka ' tenganishi' kwa wanaofunga ndoa Kanisa la Wasabato
Imeripotiwa kutoka Mbeya kuwa Mwenyekiti wa Kanisa hilo kanda ya Nyanda za Juu Kusini ametoa waraka kwa waumini wake kuwa ili ndoa zao zifungwe kwenye kanisa hilo wasiwe waliopata kuugua magonjwa ya zinaa , upungufu wa damu na kutoa mimba. Ni habari yenye kukanganya na yenye sura ya kibaguzi. Inapewa nafasi ya tatu kwenye mtandao waMjengwablog.com.
Soma habari nyingine ikiwamo katuni bora ya leo. Ni kwenyehttp://mjengwablog.com
Maggid Mjengwa,
Mhariri/Mchambuzi Habari za Mtandaoni Mjengwablog.com
0754 678 252
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment