Lile blog kutoka Visiwani linalojiita kama "The Mouth of the South" - yaani Zanzibar ni Kwetu leo liliacha kuandika mambo ya UAMSHO na badala yake likatuingilia huku Bara na kuicharaza kampuni yetu ya maji ya Dawasco kwa kuandika kwenye page ya mbele kabisa ya blog hilo kwa herufi kubwa tena in colours kuwa....
"YALISEMWA ZAMANI NA MWALIMU NYERERE KUWA UBEPARI NI UNYAMA NA KUWA THE VERY NATURE OF CAPITALISM IS CRUDE, BARBARIC AND ANTI-PEOPLE! LEO NDIO TUNAIABUDIA SIASA HII HII YA KINYAMA. HATUSEMI KUWA MWIZI AACHIWE AU KUWA NI SAWA KUIIBIA DAWASCO, LAKINI TUNASEMA KWA SAUTI KALI KUWA UBEPARI NI UNYAMA AND MWALIMU WAS RIGHT!!!

PIA, TUNASEMA KUWA HUYU ANAEIBA MAJI SIO MWIZI. MWIZI WA DAWASCO NI YULE ALIETOROSHA MABILIONI YA HELA ZETU ZA KIGENI NA AKAZIWEKA SWITZERLAND - HUYU NDIO MWIZI. HUYU NDIO ANAETUIBIA MAJI NA KILA KITU KATIKA NCHI HII NA SIO HUYU MAMA MNAEMUONEA BURE
TU!

KAMA KWELI MNAWAKAMATA WANAOTUIBIA BASI KAWAKAMATENI HAO WALIOFICHA HELA ZETU HUKO SWITZERLAND!!!

ANAONEWA YULE ANAEKWIBA MAJI, LAKINI YULE ANAEKWIBA FOREIGN EXCHANGE NA ANAEPOKEA COMMISSION HATA HAULIZWI KITU!!!

WENGI KATIKA NCHI HII NI WEZI NA WENGINE WAMEJIFICHA HUMO HUMO NDANI YA DAWASCO, LAKINI HAWAGUSWI NA ANAGUSWA YULE MWIZI WA MAJI, HAYA YANAMWISHO!!!"

Mwisho kumewekwa picha za kukamatwa kwa yule mama kule Tandale (DSM) na huku akiburuzwa na wafanyakazi wa DAWASCO!
Katika kumalizia blog liliuliza..."Hivyo tunafanya haya ya kuwadhalilisha watu wetu kwasababu Mwalimu Nyerere hatunae leo? Kweli siku za Nyerere tungeliyafanya haya? Miaka 50 baada ya Uhuru na maji bado ni shida kwa wananchi wetu, hivyo hatuoni vibaya wala haya???"

"DAWASCO ACHENI UNYAMA HUU WA KUWADHALILISHA BINAADAMU WENZETU KAMA WANYAMA. KAMA MNATAKA KUWAKAMATA WEZI WA NCHI HII BASI NENDENI SWITZERLAND NA SIO TANDALE!!!"