Tuesday, 26 February 2013

Re: [wanabidii] Matokeo kidato cha 4 Zanzibar : Ujumbe wa Serikali kwa wananchi wake

MNHHH..ULOYANENA MAZITO...HASA HIYO HAYA YA MWISHO KUWA RAIS WETU NI MTU WA MISIBA TUU ILA HUU MSIBA MZITO WA KITAIFA WALA HAUMTII PRESHA NA KESHASAFIRI KWENDA NJE KAMA KAWAIDA YAKE.


From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, 25 February 2013, 5:11
Subject: [wanabidii] Matokeo kidato cha 4 Zanzibar : Ujumbe wa Serikali kwa wananchi wake

Na Maalim Omar Sheikh Kisisyina,
Kwa muda mrefu sasa Wazanzibari tumekuwa tukipiga kelele juu ya uonevu tunaofanyiwa na baraza la mitihani la Taifa yaani NECTA. Pamoja na kuwa kelele zetu hizi zilipuuzwa sana, na hali zikiwa na ukweli asilimia tisiini na tisa, bado hatujapata nusura.
Hatujapata nusura kwa sababu wenzetu wa NECTA bado wanafanya mchezo wao mchafu dhidi yetu na hakuna aliyekuwa na ubavu wa kuwahoji, kwani wana uhakika Zanzibar si nchi na kwa hio hakuna kiongozi mwenye mamlaka ya kuwahoji wao, kwa vile viongozi walioko huku ni wananchi wa kawaida tu kama wao kule bara.
Mchimba kisima kuzamisha wenziwe kuna siku huingia yeye bila kutarajia. Mwaka huu ule usemi wa kifo cha wengi harusi, umesadifu. Kama mlivyokwishaona kuwa matokeo ya mwaka huu ya kidato cha nne yamevunja rekodi kwa ubaya kiwango ambacho hakijawahi kutokea tangu liundwe baraza la Mtihani la taifa Tanzania.
Takwimu zinaonesha wanafunzi zaidi ya nusu ya waliofanya mtihani wamefefeli kabisa kabisa, na kubakia bila cheti wala muelekeo wowote katika Elimu. Wakati haya yakitokea nchi nzima, kila mmoja kati yetu ana mitazamo yake juu ya hili.
Kuna baadhi ya wazazi wanawalaumu watoto wao kwa kufeli. Nasema hawajakosea kwani kuwalaumu kwao huko ni matokea ya matumaini makubwa waliyonayo dhidi ya nchi yao na Serikali yao inayowapa Elimu hiyo. Na kwa maana hii kufeli kwa mtoto kwa mtazamo wa baadhi ya wazazi kunatokana na ucheza wa mtoto mwenyewe. Hii ni moja ya sababu kweli, lakini sio kwa wote namna hii.
Kuna watu wanaamini kuwa matokeo mabaya namna ile ni matokeo ya kukosekana kwa miundo mbinu ya kufundishia, vifaa, na hata walimu na suali zima la uwajibikaji wa utumishi wa Elimu nchini. Suali hili lina ukweli mtupu pia. Kwa kweli hali ya msukumuo wa usimamizi thabiti wa Elimu nchini umeshuka mno, na kwa maana hii lawama kama hizi haziepukiki.
Lawama na visingizio vyengine tunaweza kusema vimetoka vinywani mwa wakubwa wenyewe. Navyo bila shaka hatuna budi tuviangalie kwa jicho pevu pia. Bibi Ndalichako, katibu mkuu wa NECTA alisema sababu kubwa ya kufeli kwa wanafunzi ni kutoandika lolote katika karatasi zao za majibu au kuandika mambo mbali mbali yakiwemo mapenzi, na kulaumu bunge.
Hata hivyo, Bi Ndalichako hakujibu iwapo wanafunzi hao waiokuwa hawakuandika lolote, kuwa waliosomeshwa lolote pia.Pia hakusema kwanini wanafunzi walindika kuhusu Bunge lililo mbali na shule zao badala ya kuandika kilicho ubaoni shuleni mwao. Kuna maswali mengi yasiyo majibu hapa.
Kwa mtazamo wake Bi Ndalichako aliwaona wanafunzi wajinga sana kufanya kwao huko na aliona kwamba wao ndio wakubebaba msalaba wa lawama hizi. Na kwa mtazamo kama huu Bi Ndalichaka tutamchukulia kama ni mtu aliekosa hoja, na mfa maji ambae haachi kutapatapa baada ya mambo kumsonga.
Kisingizio cha mwisho kimetoka kwa Waziri Kawambwa anaposema hali kama hii imetokea kwa kuwa usimamizi wa mitihani ulikuwa imara sana mwaka huu. Yaani kwa lugha nyepesi mara hii mitihani haikuvuja, wala wanafunzi hawakufanya udanganyifu na kwa maana hio matokeo yalitoka mara hii ni safi na hayana doa.
Hoja hii ina utata mkubwa na upotofu uliotukuka, lakini hapa sitaijadili kwa upana kwani nikiichambuwa itamlazimu Waziri Kawambwa kuliomba radhi taifa kwa kuwasingizia wananchi kuwa waliofaulu wote walipitia njia za panya, njia ambazo zingefungwa wasingekuwa hapo walipo, akiwemo yeye mwenyewe na Mawziri walioko Bungeni wote kwa ujumla, ni vihio.
Pamoja na lawama na visingizo vyote, mtazamo wangu ni kuwa matokea tuliyoyapata mara hii ni ujumbe maalum ambao Serikali imekuwa ikitafuta njia ya kutufikishia sisi wananchi kwa njia amabyo tungeifahamu kwa urahisi. Lakini kwa vile sisi tuliotumia dalili mbalimbali za ujumbe huu, ni mbumbumbu tuliofeli kama walivyofeli wenetu juzi, hatukufahamu kitu pia.
Serikali yetu kwa muda mrefu imeiingiza Elimu katika siasa tasa ya Tanzania na kuuwa viwango tangu mwaka 1967. Na kuna lengo zima kwa Serikali kuisiasisha mno Elimu. Lengo lao ni kupunguza idadi ya wasomi ili waweze kuwakandamiza zaidi na kujihalailishia utawala. Na hoja yangu hii inaungwa mkono na tafiti lukuki hapa nchini hivi sasa na tangu zamani.
Mfano mzuri angalieni kisa kilichopelekea Serikali kutuwekea Sera ya lugha mbili ya Elimu hapa nchini yaani 'Bilingual language policy'. Sera hii ni zaidi ya sera za kikoloni zilizotumika kuikandamiza nchi yoyote duniani na haijatumiwa na hata mkolini mmoja duniani katika koloni lake. Tunaitumia sisi Tanzania leo.
Kwa kurahisisha maneno, hii ni sera inayolenga kuwa Kiswahili kitumike kufundishia Shuleni, kuanzia shule za msingi na Kiingereza kitumike shuleni Sekondari. Huu kama si ujuha ni kitu gani. Ikiwa mwanafunzi amesoma na kukulia katika kiswahili tangu mdogo hadi anafika miaka 15 ndio anaanzishwa kusomeshwa kwa kizungu alichokuwa hajakilalia wala kukiamkia, miujiza hii ya lugha itaotka wapi?
Jambo lolote laanza na msingi, na ikiwa kiingereza hakikuanzwa mapema tena kwa misingi madhubuti mwanafunzi atatarajiwa wapi kukijua akifika Sekondari baada ya miaka nane ya Kiswahili? Isitoshe kwa mujibu wa tafiti, Kiingereza hakina walimu kwani hao walimu wenyewe wa Kiingereza akija mkaguzi wa Kizungu au wakimuona mzungu njiani huingia mitini wasijekuulizwa 'Good Morning'.
Hebu leo nambieni waumini wa vitendawili; 'Wafu kwa wafu wakokotana?' – Jahazi na Tanga. Lakini hali hii haiji kwa mwalimu asiejuwa kitu akamfundisha mwanafunzi ajue kitu. Na hivi ndivyo Serikali ilivyotujenga. Walimu wengi wanaosomesha wametokana na mfumo huu wa elimu ya kuhifadhi midesa, kwa vile kizungu hakimo, na wakipewa ualimu huwa kama makasuku, tu maana hawakusoma wala kuelimika. Katika hali kama hii tutegemee nini?
Tatizo hasa ni Serikali, tatizo ni sera ya lugha. Nakumbuka mwaka 1978 Waziri wa Elimu bara Thabitha Siwale walijadili sana juu ya hoja hii. Ikaundwa Tume ya Jackson Makweta mwaka 1983, na ikapeleka ripoti kwa Mwalimu Nyerere kwamba Kiswahili kitumike moja kwa moja shuleni kwani Kiingereza hakisikiki shuleni. Nyerere alikataa. Miaka ya 1990 hali hii ikasemwa, hakuna mwanasiasa aliyejali. Kwanini? Wanachokifanya wanakijua vizuri. Ni kutunyima Elimu ili watunyonye na kututawala.
Mbali ya suala la Sera ya lugha, Serikali imeondosha vipaumbele vya kuisimamia na kuihudumia Elimu. Matokeo yake Elimu imefanywa kuwa Biashara badala ya haki ya lazima ya kila mwananchi. Shule za Serikali zinanuka uvundo, hazina lolote lilioko. Nani anajali, wenye nchi watoto wao husoma ng'ambo, watajuaje shida zetu hapa?
Baraza la mitihani limefanywa Biashara. Na bila haya wala aibu, wanawafelisha vijana kwa kuwapangia alama maalum wanazoamini watashajiika kununuwa tena mitihani kwa wingi ili wapate fedha zile zile za mnyonge anaekubali kukosa nguo ya kuvaa na kula vizuri kumlipia mtoto wake akasome tena. Tena bila kujua kuwa mtoto huyo atasoma lakini sio kwa kunufaika yeye bali kuwanufaisha maafisa wa baraza la mitihani wanaukanyaga mgongo mnyonge huyo kama daraja la kupitia kuelekea katika utajiri wao na familia zao.
Tunapofika hatua kama hii, tufike tukubali kuwa Serikali haina nia nzuri na wananchi wake. Na matokeo haya mabaya hakuna anaestahiki kubeba lawama asilimia mia moja na khamisni kama sio Serikali. Na bahati mbaya Serikali hata haina habari juu ya maumivu tuliyonayo dhidi ya janga hili la taifa lililotupata mwaka huu.
Tena mimi nashangaa sana Rais Kikwete ni mtu hodari sana wa kuhani, kwenda mazikoni, na kujulia wagonjwa, kwa hili tunamshukuru sana, lakini cha ajabu haoni haja kutangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka huu kuwa janga la taifa au angalau kuuita msiba wa kitaifa na kuyafuta matokeo haya kabisa. Kwa vile haoni haja wala haoni kuwa huu ni msiba na janga la taifa, tutaachaje kuamini kuwa Serikali imeyapanga haya tunayoyaona?
Natoa hoja
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment