Wednesday, 27 February 2013

Re: [wanabidii] Zanzibar Ni Kwetu yaicharaza Dawasco kuacha unyama mara moja!!!


Mwizi ni mwizi hakuna haja ya kumtetea kwa kulinganisha Eti anaiba maji aache kwa sababu kuna walioiba hela zipo nje ya nchi! Huwezi ukasema ninaiba kwa sababu mbona mjomba alikuwa anaibaga? Ninaua kwa kumchinja kwa sababu mbona yeye ndugu yake kamuua ndugu yangu? mbona kaiba kwa nini mimi nisiibe!!  Ninatukana kwa sababu mbona mama akitukanaga watu? Sidhani kama hivi ndivyo na  haya sio reasoning kwa maadili na ufanisi tutakao kujenga au tuyatakao. Wenzetu ulaya wamefanyakazi kubwa sana kuweka zile tabia za usafi na uaminifu pamoja na kuwa sio 100 uaminifu na usafi-wapo wanaokosea na picha zao zinatoka magazetini na ni watu wa dini na origin mbali mbali. Hata mbakaji picha yake inatolewa, mwizi ktk photo au ya kuchora, au camera inavyomwoshesha hata ktk bukha alilobakiza macho tu. Hapa sisi tunatoa picha ya msichana aliyebakwa tunamzima macho sio mbakaji au jambazi tenga (upelelezi unaendelea). Ulaya waziri, padri, baba muuaji, mbakaji picha inakuwa wazi. Sisi hata mwizi wa maji mwiko.

Taarifa imetoka magazetini kuwa Kijana kamteka nyara msichana akanamuweka ktk chaga chini ya kitanda miezi 4 akimbaka. Hatuweki picha yake kijana na juhudi za kwenda kuchukua virago hivyo for DNA kuhakikisha akilala juu ya godoro ya juu ya chaga-kitanda hicho hazitokuwepo ktk kuleta Haki. Uchunguzi unaendelea, akipatikana na hatia atapelekwa mahakamani!! Chukua godoro hizo, mashuka, nguo hizo chafu za msichana for DNA test kabla hawajachoma virago hivyo. Uliza mshichana maumbile ya mbakaji na alama zake mwilini. Unasubiri nini tena? Toa picha yake na ya Wenzake ili wakitoroka wakamatike. Usalama gani utakao kwao na ni waouaji na huenda wamefanya mengi zaidi ya haya!! Na hatutoandamana kwenda kuzoa magodoro hayo kupeleka Ocean Road hospital kuchangia gharama za DNA test. Kuwe na shirika lipate hela za GVT kwa vitu vya haraka namna hii  (DNA Test) kuondoa gender-based violence zinazolala kimahakama kutokana na vidhibiti kutokuharakishwa kupatikana na GBV inazidi kukua kutokana na mwanya huu.

Ndio maana tunaona picha ya mama huyu asemwae hapa kuwekwa gazetini haifai kwani ni tabia ya kuficha ukweli tulio nayo waswahili hata watu wa damu yetu wanapotendewa uovu/maovu. 

Kwa taarifa-nilichangia kwa picha huko nyuma- Wauzaji maji wengi DSM ni wenye uwezo waliounganisha ktk bomba kuu au kuchimba visima virefu, kuweka tanks, kupambu maji kwa umeme na kuuza hayo maji. Wenye uwezo wengi huko mitaani ni Wapemba au watu wa Unguja hasa mitaa ya uswahilini. Wauza maji, wanapenda uhaba uwepo ili wauze maji na huugharimia utengenezwe na vishoka na wahusika wa hayo mabomba. Mtu mgeni mwekezaji anapoibia nchi maji au umeme etc-apewe masaa 24 aondoke -Non persona Grata aende kwao, kiwanda kitaifishwe kilipe gharama zake za ufisadi. Mtandao wake wa watumishi-mafao yao waingie kulipia gharama hizo za uharibifu na wizi.

Tulipata shida sana kuingia nyumba za wageni wakazi na haza Wapemba walio mitaani uraiani DSM. Kazi za tathimini ya shughuli za Dawasa/Dawasco zilitupa picha aliyoiongea Mfumwa Mh Maghembe ambapo niliweka picha kibao humu mtandaoni huko nyuma kuhusu suala la maji DSM picha za Buguruni, Ilala kati, Keko, Mbagala, Mwananyamala ni kazi sana kuingia nyumba za wa ZNZ hasa wapemba kufanya tafiti (ya aina yoyote si maji tu).

Hakuna haja ya kujaza mapicha hapa ya hayo majumba yao na matangi makubwa mengi tena yaliyounganishwa na pump za umeme kuvuta maji kujaza tanks hizo kutoka distribution main. Umeme unalika ktk kupampu maji na ndio hayo maunganisho ya vishoka. Wengine wana generator ili kupunguza gharama. Unaingia uhoji familia wanagoma kutoka nje eti baba au mama hayupo ila wakati mnakwenda msindikizaji mwenyeji anakuambia alimuona akiingia ndani alipoona watafiti maana wewe humjui unaona mtu tu. Wengi wakitujibu-haituhusu!! yaani wao sio watu wa bongoland hayo tuendayo kuwahoji haituhusu wanasema. Wachache sana wakitoa ushirikiano ktk tafiti.

Kingine ni watu wa Dawasco kubana nati ya distribution main (bomba kuu la maji) na kuachia pale penye ungio liendalo kwa mtu fulani alipoungiwa kupeleka kwake ili apate maji auze. Lile la WUA (water user association) lipate mchuruziko kidogo na foleni iwe kubwa waende kununua ya matanki ya gari zinazouza, mikokoteni na hao wauzaji wenye matanki ambapo picha niliweka humu. Sabotage inafanywa na watumishi na vishoka. WUA zitakueleza matatizo kibao. Na hizo WUA baadhi zina ufisadi na kugombania madaraka kuvinjwa kamati na kuunda upya kutokana na ulaji baadhi yao na zipo zifanyazo kazi kwa ufanisi.

Nilichangia kusema, uchimbaji visima hovyo na kupampu maji toka ardhini itakuja kutuathiri kutokana na kuweka nyufa ardhiri kupitia visima na kuondoa balance aliyoweka muumba ya maji chini, mawe na miamba na juu sisi na nyumba zetu. Kuna siku maghorofa yatakuja kukatika na kuanguka kutokana na kutitia ardhi kutokana na overpumping ya maji. maji ndio biashara kuu mojawapo ya kipato kwa sasa.

Nyumba zina unregistered open and medium deep and deep boreholes zinazochimbwa na makampuni binafsi zaidi. Wala hayo maji huenda hayapimwi. Watu wanauziwa maji yanachumvi sana na wauza maji ktk matangi wanachanganya maji ya chumvi na maridi. Ukitaka sofy water bei ghali kuliko saline water. Madini yanaweza kuwa maji ya chumvi yaingiayo visimani kutoka baharini DSM au madini asilia au muingiliano na maji ya viwandani wamwagayo hovyo na kuchuruzikia visimani. Pia, baadhi ya wauza maji-tankers huchota toka unprotected sources. bado hayo madini yatokayo na garage bubu, uchimbaji madini na uchafuzi wa vyanzo vya maji. Afya zetu zipo rehani.

Hata Jangwani-Sunna bondeni kwenye uchafu kibao kuna visima vya open na vya handpump vilivyojengwa na watu binafsi na mashirika ya dini waliowapa madrasa au mzee fulani. pampu imezungukwa na maji ya kijani machafu ya kichesi nna yapitayo. Miferehi cemented/reinforced ya maji ya mvua lakini miejaa maji ya kinyesi kila mtu anatupia hapo na taka nzito na mambomba ya maji ya kunywa yanakuwa yanapita juu au ndani ya maji hayo na kila mwananchi anaona afanyavyo mwenyewe na hajali. Picha zote niliweka huku. Lakini daima lawama inapofika watu hao kukamatwa. Kama unatupa takataka hata mchanga zitaziba tuu bomba chini ardhini maji hayatopita, yatafurika majumbani na mtaani. kama unazibua mfereji na manholes unakuta viroba vya maganda ya viazi, mboga, mapira ya fundi viatu, magamba ya miti ya mchonga vinyago na mataka mengine, kuzima na kufurika lazima. Tujenge tabia za usafi amba sivyo miundo mbinu hata iwe mipya vipi haitatusaidia. Tuwe waaminifu tuache wizi na kuibia Taifa na kujiibia Afya Zetu pia-Tunajidanganya.

Lakini, hii sio kusema hakuna wauza maji waaminifu au efficient  WUA na wenye visima vya haki na vinafanyakazi za haki kutoa huduma kama picha nilizokuwa nimeweka za Dar, Bagamoyo, Kibaha kwa kuchangia.

Wapo wanaokata mabomba ya wenzao kwa makusudi ili wapate maji ya dezo kama wale wanaokataa kuchangia uzoaji takataka na kutupa viroba vya taka ktk mashimo ya mabomba ya maji taka, open drains na kufurisha kinyesi kwa kuunganisha majumba yao makubwa, hoteli, makampuni, viofisi katika mitaro-wazi.

Mwesiga, wapite wakikagua na kusiliba kuziba mabomba ya maji safi ambapo miunganisho si legal. Akirejesha-jela miaka 5 bila kesi mahakamani  kafanya makusudi gharama ya kesi kwa GVt ya nini? Pia yale ya maji taka yaliyounganishwa kumwagwa kinyume na sheria yasibwe ili uchafu urudi umwagike ndani ya mahoteli husika ili wajue jinsi ya kuunganisha rasmi ktk city sewer pipes na kulipia gharama. easy come easy go na tumboni street kwa vishoka na wateja wao iishe.

--- On Thu, 28/2/13, Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com> wrote:

From: Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Zanzibar Ni Kwetu yaicharaza Dawasco kuacha unyama mara moja!!!
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, 28 February, 2013, 4:28

Sina shaka na uandishi huu kuwa umeandikwa na mtanzania mzalendo na
mwenye mapenzi mema. SUALA la maji...speechless

On 2/27/13, John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com> wrote:
>  Zanzibar ni kwetu yaicharaza dawasco kuacha unyama mara moja!!!
> Lile blog kutoka Visiwani linalojiita kama "The Mouth of the South" - yaani
> Zanzibar ni Kwetu leo liliacha kuandika mambo ya UAMSHO na badala yake
> likatuingilia huku Bara na kuicharaza kampuni yetu ya maji ya Dawasco kwa
> kuandika kwenye page ya mbele kabisa ya blog hilo kwa herufi kubwa tena in
> colours kuwa....
>>
>>"YALISEMWA ZAMANI NA MWALIMU NYERERE KUWA UBEPARI NI UNYAMA NA KUWA THE
>> VERY NATURE OF CAPITALISM IS CRUDE, BARBARIC AND ANTI-PEOPLE! LEO NDIO
>> TUNAIABUDIA SIASA HII HII YA KINYAMA. HATUSEMI KUWA MWIZI AACHIWE AU KUWA
>> NI SAWA KUIIBIA DAWASCO, LAKINI TUNASEMA KWA SAUTI KALI KUWA UBEPARI NI
>> UNYAMA AND MWALIMU WAS RIGHT!!!
>>
>>PIA, TUNASEMA KUWA HUYU ANAEIBA MAJI SIO MWIZI. MWIZI WA DAWASCO NI YULE
>> ALIETOROSHA MABILIONI YA HELA ZETU ZA KIGENI NA AKAZIWEKA SWITZERLAND -
>> HUYU NDIO MWIZI. HUYU NDIO ANAETUIBIA MAJI NA KILA KITU KATIKA NCHI HII NA
>> SIO HUYU MAMA MNAEMUONEA BURE
>>TU!
>>
>>KAMA KWELI MNAWAKAMATA WANAOTUIBIA BASI KAWAKAMATENI HAO WALIOFICHA HELA
>> ZETU HUKO SWITZERLAND!!!
>>
>>ANAONEWA YULE ANAEKWIBA MAJI, LAKINI YULE ANAEKWIBA FOREIGN EXCHANGE NA
>> ANAEPOKEA COMMISSION HATA HAULIZWI KITU!!!
>>
>>WENGI KATIKA NCHI HII NI WEZI NA WENGINE WAMEJIFICHA HUMO HUMO NDANI YA
>> DAWASCO, LAKINI HAWAGUSWI NA ANAGUSWA YULE MWIZI WA MAJI,  HAYA
>> YANAMWISHO!!!"
>>
>>Mwisho kumewekwa picha za kukamatwa kwa yule mama kule Tandale (DSM) na
>> huku akiburuzwa na wafanyakazi wa DAWASCO!
>>Katika kumalizia blog liliuliza..."Hivyo tunafanya haya ya kuwadhalilisha
>> watu wetu kwasababu Mwalimu Nyerere hatunae leo? Kweli siku za Nyerere
>> tungeliyafanya haya? Miaka 50 baada ya Uhuru na maji bado ni shida kwa
>> wananchi wetu, hivyo hatuoni vibaya wala haya???"
>>
>>"DAWASCO ACHENI UNYAMA HUU WA KUWADHALILISHA BINAADAMU WENZETU KAMA
>> WANYAMA. KAMA MNATAKA KUWAKAMATA WEZI WA NCHI HII BASI NENDENI SWITZERLAND
>> NA SIO TANDALE!!!"
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment