kama ninyi wote mjuavyo kuwa radio mbili za dini zimefungiwa.Radio imani ya morogoro na radio kwa neema ya mwanza.Radio kwa neema imefungiwa kisa eti ilifundisha wakristo kuhusu haki yao kuchinja kiimani na hata sasa mkurugenzi wake,bishop Augustino Mpemba anatafutwa ili ashitakiwe na polisi.radio imani imefungiwa kutokana na kushawishi waislam wasihesabiwe wakati wa sensa.Najiuliza maswali mengi. kwanza,ni muda mrefu sasa umepita tangia suala la sensa limepita.na nakumbuka watu wengi walipiga kelele kwa nini wanaopotosha suala la sensa hawachukuliwi hatua na serikali iliamua kukaa kimya mpka leo hii ndio imechukua hatua dhidi ya radio hiyo. Je,ni kwa nini iwe leo na si wakati ule wa tukio?swali la msingi jingine ninalojiuliza, je kosa la radio kwa neema ya mwanza liko wapi?askofu mpemba anakosa gani kuwafundisha watu kuhusu kuchinja na wakati hata katiba yetu inatamka wazi wasuala ya kuchinja ni masuala ya imani?ni mawazo yangu tu,kama ni mjinga
nielimisheni.Ngupula
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment