Thursday, 28 February 2013

Re: [wanabidii] Neno La Leo: " Inuka Twende Ni Kwa Walioagana!"

Magid,

Mungu akubariki. Tatizo ni fikra finyu za baadhi yetu. Tulidhani watu wanaweza kujitawala bila uwapo au ulazima wa kutumia sheria.

Urusi walijaribu, wakashindwa. Waliamini ukiona mtu anaiba basi ana njaa. Ikawagomea, wakarejesha utawala wa sheria.

Hapa kwetu tumejaribu kuachia uhuru, tumeutumia bila nidhamu. Imetufikisha hapo. Tusimamie matumizi ya sheria, vinginevyo...

Balile
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 28 Feb 2013 12:27:32 +0000
To: wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania<mabadilikotanzania@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Neno La Leo: " Inuka Twende Ni Kwa Walioagana!"



Ndugu zangu,

Hakuna wawili watembeao pamoja pasi na maelewano.
Ukiwaona wanadamu wawili wanatembea pamoja, basi, wana makubaliano. Ni watu waliopatana.

Kwenye kundi la watu wa mataifa tofauti ukimsikia Mtanzania anamtamkia Mtanzania mwenzake, tena kwa Kiswahili; " E bwana inuka twende zetu!", na Mtanzania huyo mwingine akabaki amekaa bila kushtuka, basi, utilie mashaka UTanzania wake.

Ndio, " Inuka twende ni kwa waliogana". Ni watu wenye kufahamiana. Ni ndugu.

Nimeanza kuingiwa na hofu kuwa Watanzania tumeanza kupoteana kama ndugu. " Inuka twende' yetu imeanza kuangaliwa kwa sura ya udini, ukabila na itikadi.

Hatujafika pabaya sana, lakini, tunakoelekea ni kubaya. Tumeshaziona ishara. Miongoni mwetu Watanzania tumeanza kuzisikia kaauli za ; " Umewasikia jamaa zetu Wakrito? Umewasikia jamaa zetu Waislamu? Umewasikia jamaa zetu WaZanzibar? Umewasikia jamaa zetu wa Bara?......"

Hizi ni ishara za undugu unaosambaratika. Zamani sisi sote tulikuwa ni ndugu. Tulitembea pamoja, ishara ya watu tuliopatana.

Leo kuna Watanzania wanaoambiwa; " E bwana wee, siku hizi nakuona unatembea na kuongea na wale jamaa zetu wa upande mwingine!"

Ndio, Watanzania tumeacha kuwa ndugu. Tunagawanyika kwenye mapande. Ni kwa kuzitazama tofauti za dini, kabila na itikadi.

Hatujafikia pabaya, lakini, tunakoelekea ni kubaya. Tukumbuke; " Inuka twende ni kwa waliogana". Watanzania tulishaagana. Tulishakubaliana. Tulijua tunakokwenda kama Taifa. Kama ndugu. Tumeanza sasa kusambaratika.

Tuinuke sasa twende kupambana na yote yenye kutugawa kama ndugu wa taifa moja. Tuna kila sababu, nia na uwezo wa kushinda mapambano haya dhidi ya ubaguzi wa aina zote.


Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
http://mjengwablog.co.tz/

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment