kwa kweli mmomonyoko wa maadili kwa upande mwingine wazazi ndio chanzo
miaka minne boarding!?ndio hao watoto kuwa mafisadi wa baadae coz
nidhamu hawana na hili mimi nmeliona hata kwa baadhi ya watoto wa
jirani zangu pia wanakuwa kama mazuzu!
On 2/24/13, Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com> wrote:
> Shalom
>
> Siku hizi imekuwa ni kama fasheni kwa wazazi kuwapeleka watoto wadogo
> shule za kulala. Watoto wengine wanapelekwa huko wakiwa wadogo sana,
> miaka minne au mitano. Huwa najiuliza sana, ni nini hasa
> kinachopelekea wazazi kufanya uamuzi kama huo? Ni ubize au kwenda na
> wakati? Wengine wanajitetea kuwa wanafanya kazi mchana kutwa na
> wanarudi nyumbani usiku hivyo mtoto hashindi nao hivyo ni sawa tu
> kumpeleka boarding, mimi sikubaliani na hili. Hata kama unarudi
> nyumbani usiku angalau unaweza kupata muda wa kuongea na mtoto wako
> na kuangalia afya yake na kujua anaendeleaje na sio kumpeleka shule ya
> kulala na mnaonana mara moja kwa wiki au mwezi kabisa.
>
> Mtoto anatakiwa ajifunze maadili ya familia yake na za kiMungu akiwa
> na wazazi wake na afahamu jinsi ya kuishi na wazazi, ndugu, jamaa na
> marafiki kwanza kabla ya kumpeleka kufundishwa na watu wengine? Je,
> unadhani unamjengea nini mtoto wako kwa kumuacha kuishi na kulelewa na
> watu tofauti wa wazazi wake katika umri mdogo kiasi hicho? Je,
> unajuaje kama watoto wenzie hawamfundishi mambo yasiyofaa maana
> haonani nawewe kila siku? Ni rahisi kugundua kama mtoto ana tatizo au
> hofu fulani kama unakaa naye nyumbani kuliko kumuona mara moja kwa
> mwezi.
>
> Unafanya kazi kwa bidii kwa sababu ya maisha bora ya mtoto wako, sasa
> kwa nini umjengee msingi mbovu kwa sasa kwa kisingizio cha kujenga
> maisha bora ya baadaye? Mtoto umleaavyo ndivyo akuavyo, hata kama
> umeenda kusoma mbali, ni vyema akikaa na mzazi mmoja kuliko kukaa
> kwenye jumuia ya watu tofauti wenye maadili tofauti. Ni wakati sasa
> wazazi tukabili na kutekeleza majukumu yetu hata kama ni magumu kiasi
> gani na sio kuwasukumia watu wengine.
>
> Kumbuka mtoto ana haki ya kudeka kwa mzazi wake japo isizidi sana,
> sasa huko boarding atamdekea nani jamani???
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment