Sunday, 8 July 2012

Re: [wanabidii] Ushauri wa mbowe juu ya msongamano wa magari

Shirikisho,
jia la mtu asiyeoa ni kipofu, jina la mtu mwenye ulemavu wa viungo hasa miguu ni kiwete. kusema mlemavu wa viungo hilo siyo jina bali ni sentensi au tafsiri ya jina.
Nawashangaa watu wanakwepa kuwaitwa walemavu wa gozi zeruzeru badala yake wanawaita jina hilo hilo ila kwa kiingereza yaani albino na huu nao kwangu naona ni ulimbukeni.

sidhani asiyeona kuitwa kipofu basi utu wake umeondoka, ingekuwa hivyo inabidi kubadilisha majina yote maana yanadhalilisha kama vile mwizi, jambazi, fisadi, malaya, kahaba hayo yote wanaitwa watu na yanadhalilisha.

Kila mtu aitwe jina linalostahili maana utu wa mtu hauko katika jina analoitwa bali katika matendo anayotenda.

2012/7/8 SHIRIKISHO LA VYAMA <shivyawata@yahoo.com>
Ndugu Hosea,
 
Naheshimu mawazo yako, ila napenda kukosoa matumizi ya lugha inayoondoa utu. Hii si kwako tu bali na kwa yeyote ambaye hakuwa na uelewa huu.
Wenye ulemavu nao ni watu, na kwa heshima ya utu wao hatutumii majina yasiyobeba utu kama ulilotumia la 'Kiwete' badala ya mtu mwenye ulemavu wa viungo. wengine hutumia vipofu badala ya watu wasioona au wenye ulemavu wa macho.
Naomba wote tuutumie ufahamu huu. Asante
 
Novat
From: Hosea Ndaki <hosea.ndaki@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, July 7, 2012 1:21 PM
Subject: [wanabidii] Ushauri wa mbowe juu ya msongamano wa magari

Nimesoma katika magazeti kuwa Mbowe katoa mapendekezo kadhaa juu ya kupunguza msongamano wa magari dar, baadhi ya point nilizoona ni;
1. Kuwekwa ada za magari kuingia mjini
 
2. Ziachwe njia za watembea kwa miguu
 
3. Yajengwe madaraja ya watembea kwa miguu.
 
Labda namie niseme;
1. Kuwekwa ada za magari kuingia mjini
Tayari ada zipo kwa jina la "parking fee" lakini haijasaidia, kuiongeza ni kumuumiza binti anaetumia usafiri wake kwenda kazini achilia ka mkopo ka benki anakokalipa kwa shida. Kwa maana nyingine anasema watu wanaendesha magari kwenda mjini kwa ufahari, la hasha adha za daladala ndo zinasukuma, wengine ni wafanyabiashara hubeba mauzo. labda angeshauri makampuni kama NSSF na PPF waache kujenga business complex katikati ya mji. maeneo ya mlimani city na mawasiliano house hayapo azikiwe mbona yanafanya biashara vizuri tu.
 
2. Ziachwe njia za watembea kwa miguu
Sidhani kama unaweza egesha gari yono watalifunga mnyororo na kuliburuza. hata hivyo hakuna mtu anaweza tembea kwa miguu kutoka mwenge hadi posta kama tukiondoa haya magari anayozungumzia bwana mkubwa. Ningeshauri sumatra waweke madaraja ya usafiri yenye nauli tofauti mfano economy coaches (nauli 300/=) business coaches (nauli 1000/=) executive coaches (nauli 5000/=) mkazi wa makongo juu anaweza kuegesha gari mlimani city then anapanda bus hadi posta.
 
3. Kujenga madaraja ya watembea kwa miguu
Bado viwete na wasukuma toroli hawataweza kuvuka barabara kwa kutumia hayo madaraja kama ya manzese, labda wakati waupanuzi wa barabara tufikirie kujenga subways ambazo hata viwete na wasukuma toroli na guta watatumia kuvuka barabara. Tuangalie uwezekano wa Tanroad kushirikiana na sekta binafsi kujenga parking yards, mfano mtu anaweza egesha gari mbezi mwisho akapanda basi hadi kariakoo au posta, jioni akalipitia kwenda nyumbani.
--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
0 comments:

Post a Comment