Sunday, 8 July 2012

Re: [wanabidii] Ushauri wa mbowe juu ya msongamano wa magari

Pamoja na Ushauri wa Mbowe, Tukiamua kulipisha ushuru bado yatajaa mzee, mbona parking watu wanalipa mpaka magari yanakosa sloti za kupaki?Nchi hii haina magari ya kuweka msongamano mpaka muanze kulipishana. Kitu ambacho viongozi wetu hawajakiona ni kuwa watu wengi wanaoendesha magari hawajui kutumia barabara. Suala la kuendesha ni tofauti na kujua kutumia barabara.Nashauri mabo yafuatayo yafanyike:
1.Madereva wa daladala wafundishwe kutumia barabara, na kama hawataki kufuata masharti waondolewe barabarani kwa sheria.(SUMATRA +POLISI)

2.Ufanyike mpango wa kufanya kampeni kama inavyofanyika  ya Ukimwi kuhusu matumizi bora ya barabara, matangazo, vipeperushi, sinema,makongamano na hata kwenye nyumba za ibada na Bungeni wahamasishaji wapewe nafasi ili kila mtumiaji wa barabara aelimishwe. Hii ikifanyika kwa ufasaha hata ajali zitapungua.(WIZARA YA UJENZI+POLISI+SUMATRA)

3.Utaratibu wa kukagua viwango vya magari yanayotumia barabara zetu unaotekelezwa na TBS kwa magari yanayoingizwa kutoka nje utiliwe mkazo hata na yanayotumika nchini ili kupunguza magari mabovu barabarani (Mandatory Vehicle inspections for conformity to road worthiness).
Baada ya hapo mtaniambia kama foleni hazitapungua kama sio kuisha kabisa!

From: heche suguta <hechesuguta29@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, July 8, 2012 8:05 AM
Subject: Re: [wanabidii] Ushauri wa mbowe juu ya msongamano wa magari

Hii nchi wala haina magari ya kusema sasa tuna magari ya Foleni, wala suala hapa sio kusema tulipe ushuru wa kuingia mjini, Wazo langu mimi ni Mabadiliko ya Kifikra kwa wenye maamuzi, kwamba sio lazima ujenge orofa posta ndio litaonekana orofa hata KIMARA,BOKO,BUNJU,KIBAMBA, jengo hilo litakaa na kubadili kabisa madhari ya eneo husika na hivyo kuondoa msongamano wa kienyeji pale Posta...unashangaa serikali yenyewe hii inayopiga kelele za Foleni Taasisi zake zinainua Mijengo mjini kati kule isiyo na parkin wala mfumo mzuri wa maji taka matokeoyake mavi yanajaa kila mtaa sijui ustarabu gani wa hawa watu wanasema wamesoma!!!

Nadhani tunahitaji kiongozi anayeweza kutambua mipango ya usafi wa Mazingira na miji misafi iliyopangwa vizuri kwa sasa kwenye hii serikali huo msukumo siuoni!!

From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, July 7, 2012 11:20 AM
Subject: Re: [wanabidii] Ushauri wa mbowe juu ya msongamano wa magari

Meja,

Wataalamu wetu wa miji walaji wa fedha tu hao while brnding impressive qualification (vyeti kibao) lakini ni kwa ajili ya kuhalalisha uvurugaji wa mipango miji kwa maslahi yao!

Dar iliingizwa kwenye satellite cities baada tu ya uhuru na ndipo sinza na hata miji mingine ikapimwa na kujengwa chini ya Mzee Kikenya na Idd Simba. Mradi ule ukaachwa, wakaleta program ya "sustainable cities" nayo imeachwa wakati mji wa Mexico ulikuwa na mpango kama huo umefaulu sana na kupunguza polution kwa 70pct. Mexico was the most polluted city in the world!

Sasa wakaja na program nyingine ya upimaji viwanja elfu ishirini, sijui inaitwaje nayo; ni njia ya kunyang'anya watu waliopewa viwanja kwa kufuta hati. Nayo imekwama baada ya kesi kibao kufunguliwa maana fidia walizokuwa wanalipa ni kiduchu na watu wakawastukia.

Sasa unaachia jengo la orofa 40 kujengwa city center, akili yako timamu kweli, maana jengo kama hilo likipangishwa maofisi ni karibu watu elfu mbili. Sasa hata kama 20pct yao ndio wana magari, ina maana additional 400 vehicles zinanyang'anyana parking slots maana majengo hayo hawaweki parking nyingi kukidhi wateja.

Akiingia rais kichaa, watu wa kwenda segerea ni wapanga miji yetu! Wamesababisha maafa eti kisingizio cha wanasiasa. Mbona madaktari hawasingizii kuingiliwa? Na kama ukiingiliwa kwanini ukubali na usijiuzulu na kupiga kelele? Wanafaidika ndo sababu hiyo wanaitumia sana! Hawana la maana hao, vyeti wangevirudisha vyuo walikosomea ili tujue hawana lao.
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.

From: mejah mbuya <mejaah@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sat, 7 Jul 2012 20:52:09 +0300
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Ushauri wa mbowe juu ya msongamano wa magari

kaka Tikooza,

Ushauri kamambe na wenye tiba...hayo yote yanazungumzwa sana..ila vitendo je?

Watu wetu wa pale Ardhi wanaomaliza mbona wanenda kuwa ma-cashier bank?wasipange miji yetu?Je umeiona Dar Master plan?Je nani anayetoa vibali vya majengo marefu down town ilihali hakuna parking achilia mbali barabara kwa hao unaowamasisha waje mjini?na yale majengo ya vioo tupu..AC inahitajika je umeme upo?Mkoloni hakuwa mjinga..angalieni Ocean Road Hospital,hadi leo mtu ahitaji AC...Je raisi anayepima maendeleo ya nchi kwa majengo("Dar itakuwa kama Manhattan",namnukuu raisi wetu wakati wa ufunguzi wa pension house-Ohio street mwak huu)..Mwalimu alisema maendeleo hayapimwi kwa majengo na mabarabara...sasa sijui Dar ikiwa kama Manhattan ndiyo maendeleo?Je,nani anasimia usalama wa barabarani ikiwa trafiki wetu ni mtandao wa kukusanya mapato ya maendeleo binafsi?Je wasomi wetu..wanapenda kufauata sheria za barabarani,ingawa wanazifahamu sana(Elimu hata iwe vipi,siyo kigezo cha mabadilko ya tabia),mimi kama mpanda basikeli nakutana na kero kila siku,hasa kwa dada zetu madereva dharau ni kubwa sana,ikiwa na wewe "hau-drive"...anakuchmekea ukimuuliza anakutukana na anafunga vioo...na wanaume wanakwambia wewe una kichaa kabisa..hebu toka hapa na mambo yako ya haki za wapanda baisikeli.

Hapa nilipo nina kesi 2 mahakamani,1 ya kushtkiwa na jiji,kisa nimehoji kwa nini  muuza machngwa kwenye baisikeli   akamatwe na anaeuza ice cream za bakhresa ameachwa..wa machungwa anachafua mazingira(ingawa ni bio-degradeable) na mara nyingi huwa wanauza kwa wanaorudi nyumbani jioni kwenye foleni..Ice cream za bakhresa tukikula..tunatupa vikopo vya plastic ambavyo haviozi..miaka 200!Bado hawa mgambo wa jiji wanalipwa kuwatoa hao,wengi wao ni wala rushwa za buku buku toka kwa mama zetu,dada zetu,kaka zetu wanaojaribu kuuza chochote wajilinde..wanaambiwa wanachafua..kubwa kuliko zote.ikiwa unifomu mbaya za daladala,zinauzwa zaidi ya 40,000/- je zile za mgambo wa jiji(Sijui kama umezichnguza) ni za ubora wa juu kuliko hata za polisi wetu..ni shilingi ngapi zimelipiwa kwa bajeti ghani?

Mengi yanakera,yanasikitisha,yanakatisha tamaaa...ni nchi yetu ni watu wengi..nini jukumu letu?..
WALK THE TALK,AND LETS STOP POLITIKING..nchi yetu inajengeka..we need few hanful of committed people,huna haja ya kuwa mwanasiasa..just be ashame kama siku imepita bila kufanya chcochote cha kuboresha jamii iliyokuzunguka..siyo kwa sifa wala kwa ufahari...wanafunzi wetu wa udaktari watengeneze health clubs,waendee Tandale,Manzese,Tandika,watoe ile elimu ya zamani ya Sayansi kimu,kuhusu mazingira,afya kwa ujumla..mazalia ya mbu,matumizi ya net,nk..hapo tutafika..
na sisi wanabidii tuwe na mbinu za kujipanga..hata haya tunayoandika wangapi huwa tunayasoma ya wenzetu?Mwaka jana uliitishwa mkutano wa wachangiaji wote wa wanabidii pale Book cafe(Hivi bado ipo?) nakumbuka walikuja watu 4 tu!

Tukiacha kuongea na kutenda,hakika walaji nchi ni wachache sana na kuwadhibiti ni rahisi..TUAMKE!

MUNGU IBARIKI TANZANIA

2012/7/7 mejah mbuya <mejaah@gmail.com>
Kwa ndugu Hosea na Jovias,

Hayo yote kuhusu kupunguza msongamano wa magari,usalama wa watembea kwa miguu,wapanda baisikeli,parking kupandishwa bei,magorofa yasiyokuwa na parking na wala umuhimu wa kujengwa kule posta kama lile jengo jipya la next to PPF tower..ambapo Mhe.alitoa kauli kwamba Dar iwe kama Manhattan wakati wa ufunguzi na mengineyo  mengi...tumekuwa tukiyasimamia toka mwa 2006!

Nenda kwenye tovuti yetu ya www.uwaba.or.tz ni chama cha kuhamasisha matumizi ya baiskeli katika jiji la Dar Es Salaam,UMMA WA WAPANDA BAISIKELI(UWABA)..ni shirika pekee linaendeshwa na watu watu kwa kujitolea..nimejitolea kama mwenyekiti na mwanzilishi wa Uwaba toka 2006...

Lengo ni;

Nenda kwenye website usome mapendekezo yote ya Mbowe na wengine yapo..kasoro suala la Fly over..na pia utaona utata uliopo kwenye mpango kamambe wa jiji la Dar(Master plan) linasimamiwa na JICA..hakuna chcote cha maana..bado huu mradi wa Dart(Successful story yetu maana tumeahidiwa barabara za baisikeli na watembea kwa miguu)..ina utata mwingi...Mfano lengo kuu la Dart ni kuboresha usafiri wa umma na usio wa moto,ila basi katika kuboresha usafiri wa umma,daladala zinaondolewa..na kutakuja mabasi makubwa ya watu 60-160...swali...je nani ataendesha mradi huo?Jibu unalo..mwekezaji...ajira za mwenye daladala(maana wengi wenye nazo ni ajira yao pia,sijui nani mwenye daladal 10,wengi ni moja au mbili,wachache sana 5) sasa basi "tajiri" wa daladala,madereva 2(1 ni dei waka),konda,mpiga debe na yale mateja pia yanayoponea daladala hawana kipato...wote hawa wankosa ajira...bomu kubwa jingine la vibaka..sasa basi ukiwauliza Dart je mmewapanga dala dala waungane wamiliki haya mabasi?Hakuna jibu..maaan kuanzia World bank wanaotoa mikopo na survey toka mwaka 1998 ni ulaji wa watu...riba ya mikopo,ada za consultant...(mama mmoja aliyefanya utafiti wa kwanza mwaka 1998,alikuwa nalipwa Dola 500 kwa siku..mwaka 1998)...

Kaka,mie nimechoka kuandika na kusema..vitendo ndiyo hulka yangu..nendeni www.uwaa.or.tz na pia www.fasta.co.tz soma harakati za kupunguza msongamano wa magari,usafiri wa wanafunzi,usalama wa watembea kwa miguu,baisikeli afya ya wakazi wa jiji,mazingira yetu na yote yanayotukera tunavyoyapigania kwa vitendo...

Samahani kama nilivyosema..sisi tunafanya kwa vitendo...ingia kule utaona hadi ni chama ghani kilichojibu barua zetu kuhusu sera zao za usalama barabarani..tuliandikia vyama vyote 2010 wakati wa uchaguzi..NI TLP,ambao angalao walijibu vizuri kidogo,CCM walipiga kijumla bila sera kamili juu ya ajali na foleni Dar,na CUF.Vingine vyote havikujibu pamoja na juhudi kubwa za kutaka kukutana na kamati zao za sual la usafiri..

UWABA tunaamini 5 E'S
1.Miundo mbinu(Barabara,plans,parking plan,fee etc)(Engineering and Infrastructure)..ndiyo DART,TanRoads,etc
2.Utekelezaji wa sheria(Enforcement of the laws) trafiki wanaingia,je adhabu za  wanaotumia vibaya barabara wanafanywa nini?nini service road?nini walking pedestrian lanes,na bike lanes?traffic wenyewe hawana jibu...hadi leo tumebaki hatujui nani anajua...TOFAUTI yake atusaidie..
3.Elimu(ya usalama barabarani na utunzaji wa jiji letu)
4.Mazingira(Enviro) wengi tukitumia usafiri wa umma na vyombo visivyo ma moto tutalinda mazingira yetu.
5.Encouragement(Uhamasishaji) ni vipi wewe na gari lako la mkopo ili na wewe uwe na status ni mbinu ghani itumike,ndiyo suala la executive coach ect linaingia..

Kama  nilivyosema..siasa ni ngumu kupiga..na pia kuandika pia ni mvivu mno...nenda kwenye tovuti au kama unaweza nitumie namba yako nikupugie nikuezee vizuri ..

Namba yangu ni 0713 652 642.

ASANTE,

Mejah

2012/7/7 Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
Some Tanzanians are useful mammals mr. Ndaki could be one of them NIMEFURAHISHWA SANA  na mchanganuo wa kuondoa kero za magazeti. Inachukua dk 15-45 kwa mpiga chabo kumaliza kusoma gazeti au zaidi ahali anaelekea kazini. Kama jiji liko kwenye kuondoa kero za wakazi wa jiji meya anatakiwa awe karibu na wadau na mdau kama bwana Hosea anacho chakuchangia.
 
Iko wazi msongamamno ni jambo moja ila visababishi ni vingi unapoamua kuondoa kero hizo hunabudi kuhakikisha unfanya homework ya kutosha

2012/7/7 Hosea Ndaki <hosea.ndaki@gmail.com>
Lipo tatizo pia la wapiga chabo, utakuta wauza gazeti ni wawili lakini kuna watu kumi na tano wanapiga chabo akitoka huyu anakuja mwingine, wameziba njia yote, nadhani haya magazeti yauzwe kwenye gift shops, book shops na supermarkets. Pia ziwepo direct services yaani muuza gazeti anatembea nazo hadi atakapomaliza anarudia zingine.

2012/7/7 Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
It makes sense ila nafikiri sasa labda turudi kwa jiji na utaratibu wa usamamizi wa jiji la dar es salaam mfano huu uuzaji magazeti na karanga pamoja na mafundi viatu usiokuwa na mipangilio hasa kati kati ya jiji ni uchafuaji wa jiji na unapunguza creativity kwa mtazamo wangu. Najua kuna watu watasema hawa jamaa wanapata kipato chao lakini zingetengewa sehemu maalum za kufanyia shuguli hizio hata jiji lingepata mapato na usafi ungeimarika

2012/7/7 Hosea Ndaki <hosea.ndaki@gmail.com>
Mwesiga, njia za watembea kwa miguu zimezibwa na wauza magazeti na mafundi viatu hasa mitaa ya posta, hakuna magari yanayoegeshwa kwenye walkways, yanayoegeshwa na yono hawayavuti basi ni ya polisi au wanasiasa wabishi. Hata ukiegesha kwa bahati mbaya watu wa parking fees huwa wanatwambia na anakuelekeza mahali salama pa kuegesha, tatizo hizo parking ndo chache.
 
Yapo mambo yasiyohitaji fedha kwa mfano, tukianzisha "walk to work for health program", watu wanaweza tembea au kutumia baiskeli hasa wakazi wa upanga na Oysterbay hivyo wataacha magari nyumbani.

2012/7/7 Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
Kama unapinga kuachwa njia za watembea kwa miguu kwa kigezo cha huwezi tembea toka mwenge hadi posta mchango wako umekosa ka umakini kidogo kidogoo labda ufafanue zaidi mkuu

2012/7/7 Hosea Ndaki <hosea.ndaki@gmail.com>
Nimesoma katika magazeti kuwa Mbowe katoa mapendekezo kadhaa juu ya kupunguza msongamano wa magari dar, baadhi ya point nilizoona ni;
1. Kuwekwa ada za magari kuingia mjini
 
2. Ziachwe njia za watembea kwa miguu
 
3. Yajengwe madaraja ya watembea kwa miguu.
 
Labda namie niseme;
1. Kuwekwa ada za magari kuingia mjini
Tayari ada zipo kwa jina la "parking fee" lakini haijasaidia, kuiongeza ni kumuumiza binti anaetumia usafiri wake kwenda kazini achilia ka mkopo ka benki anakokalipa kwa shida. Kwa maana nyingine anasema watu wanaendesha magari kwenda mjini kwa ufahari, la hasha adha za daladala ndo zinasukuma, wengine ni wafanyabiashara hubeba mauzo. labda angeshauri makampuni kama NSSF na PPF waache kujenga business complex katikati ya mji. maeneo ya mlimani city na mawasiliano house hayapo azikiwe mbona yanafanya biashara vizuri tu.
 
2. Ziachwe njia za watembea kwa miguu
Sidhani kama unaweza egesha gari yono watalifunga mnyororo na kuliburuza. hata hivyo hakuna mtu anaweza tembea kwa miguu kutoka mwenge hadi posta kama tukiondoa haya magari anayozungumzia bwana mkubwa. Ningeshauri sumatra waweke madaraja ya usafiri yenye nauli tofauti mfano economy coaches (nauli 300/=) business coaches (nauli 1000/=) executive coaches (nauli 5000/=) mkazi wa makongo juu anaweza kuegesha gari mlimani city then anapanda bus hadi posta.
 
3. Kujenga madaraja ya watembea kwa miguu
Bado viwete na wasukuma toroli hawataweza kuvuka barabara kwa kutumia hayo madaraja kama ya manzese, labda wakati waupanuzi wa barabara tufikirie kujenga subways ambazo hata viwete na wasukuma toroli na guta watatumia kuvuka barabara. Tuangalie uwezekano wa Tanroad kushirikiana na sekta binafsi kujenga parking yards, mfano mtu anaweza egesha gari mbezi mwisho akapanda basi hadi kariakoo au posta, jioni akalipitia kwenda nyumbani.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment