Pole sana Miruko
Naona unajitahidi kuelimisha watu ambao wanajifanya hawajaelewa kilichosemwa na mhe. Mbowe. Hii imetokana na mfumo tuliyoujenga ndani ya nchi yetu kwamba usipopenda chama fulani chukia na michango ya watu wake hata kama ina maana taifa.
Kimsingi suala la msongamano ni pana mno na linahitaji capital investment ya kutosha. Niungane nanyi kwa michango mliotoa. Watu wengi wanaamini flying over
ndio suluhisho la kudumu la msongamano kitu ambacho si sahihi sana. Hii inafanya kazi vizuri kama planners wa makazi wamefanya kazi yao vizuri kitu ambacho ni tatizo kubwa Tanzania kwenye miji yake mikuu. Kiufupi ningependekeza yafuatayo ili kupunguza msongamano wa magari hapa kwetu:
1) Kutawanya huduma za kijamii kama masoko,benki, posta, hospitali na stendi kuu za mabasi kila pembe ya mji. Mfano Tegeta, Gongo la Mboto, Mbezi/ kibamba, na Mbagala.
2) Kuweka miundombinu ya reli kwaajili usafiri wa umma. Mfano reli toka Tegeta, mbagala, gongo la mboto na mbezi kimara. Hii ndo njia kuu inayotumika nchi nyingi zilizoendelea
3) Parking fee/ mileage fee - hii inafanya kazi vizuri kama tutaboresha niliyoyasema hapo juu. Kuna nchi kama swaziland free parking zipo chache mno na supermarket zote unalipia parking. Nchi kama South Africa wameanza mfumo wa mileage fee( unalipa kulingana na kilomita ulizotembea kutoka eneo lenye zuio)
4) Kubadili Tabia za uendeshaji magari kwa madereva (change of driving behaviour). Kama madereva wa mabasi ya umma na binafsi wataweza kuzungatia alama za barabarani na sheria zake tunaweza kupunguza msongamano na ajari zisizo za lazima.
5) Mipango mizuri ya barabara. Tuwekeze nguvu zaidi kwenye barabara zinazo generate magari kwenda barabara kuu. Mfano: Si lazima mtu atoke posta mpya mpaka kibamba kupitia morogoro road, tutengeneze njia za pembeni mfano kigogo - mabibo -
External- kimara, pia hii yaweza kutumika na watu wa kisukuru na Tabata. Watu wa Goba wapitie makongo juu- chuo cha ardhi, hii itapunguza msongamano wa Bagamoyo road, mifano iko mingi sana ndugu zangu.
6) Kuratibu matumizi ya baadaye ya ardhi( coordinate future land use). Tabu tuliyonayo sasa ni kila taasis ya serikali kufanya bila ushirikiano kwenye mipango yao na taasisi zingine ambazo ni wadau. mipango ya barabara ya wizara ya ujenzi, manispaa na wizara ya ardhi hakuna kuaoanisha mipango yao. Hii ndo kero kubwa ya mipango miji na miundombinu mbalimbali. Mfano mzuri angalia stendi ya mwenge, shekilango road, morogoro road, na mwenge - moroco section. Angalia utoaji wa vibali wa ujenzi wa maghorofa na hati milki wakati huo huo tunatarajia kupanua barabara zenye lane say 2au 3 kila uelekeo wa magari. Shekilango imeboreshwa 2006 chini ya mramba akiwa waziri wa ujenzi baada ya miaka 5 imezidiwa na ghorofa zinajengwa sijui wakitaka kutanua itakuwaje! Matokeo ya kushindwa kuratibu ni kuwa na fidia kubwa sana bila sababu na migogoro isiyoisha ya kutaka kulipwa fidia na serikali, pia hii imesababisha kujenga miundombinu isiyokidhi mahitaji mfano stendi ya mwenye. Stendi ilijengwa ndogo huku wakitanua samunujoma na bagamoyo roads. Sasa hapo utarajie nini???
7) Mengine ni makosa ambayo hatuwezi kusahihisha mfano mahali ilipo ikulu.
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
-----Original Message-----
From: Reginald Miruko <rsmiruko@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sat, 7 Jul 2012 15:29:16
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Ushauri wa mbowe juu ya msongamano wa magari
Kwenye ada ya kuingia mjini, Mbowe haongelei parking. Jibu ni kwamba
unatia ada, let's say 10,000 kwa gari kuingia mjini. Wataingiza gari
wenye sababu za msingi na pesa. Lakini pia, usafiri wa umma uboreshwe.
Shughuli za watu wa 'kawaida' zihamishwe katikati ya jiji.
On 07/07/2012, Mbeso Society <mbeso_2000@yahoo.com> wrote:
> Je! asingetoa hayo mawazo ya kwako ungetoa lini? bora huyu kiongozi mwenye
> maono kuliko hawa aliokaa miaka arobaini kazi yao ni kununua magari ya
> misafara,ya mawaziri,ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kila baada ya
> miaka mitatu.Bora ameonyesha njia kuliko wenye macho lakini awaoni.
>
>
>
> --- On Sat, 7/7/12, Hosea Ndaki <hosea.ndaki@gmail.com> wrote:
>
> From: Hosea Ndaki <hosea.ndaki@gmail.com>
> Subject: [wanabidii] Ushauri wa mbowe juu ya msongamano wa magari
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Date: Saturday, July 7, 2012, 3:21 AM
>
> Nimesoma katika magazeti kuwa Mbowe katoa mapendekezo kadhaa juu ya
> kupunguza msongamano wa magari dar, baadhi ya point nilizoona ni;
> 1. Kuwekwa ada za magari kuingia mjini
>
> 2. Ziachwe njia za watembea kwa miguu
>
> 3. Yajengwe madaraja ya watembea kwa miguu.
>
> Labda namie niseme;
> 1. Kuwekwa ada za magari kuingia mjini
> Tayari ada zipo kwa jina la "parking fee" lakini haijasaidia, kuiongeza ni
> kumuumiza binti anaetumia usafiri wake kwenda kazini achilia ka mkopo ka
> benki anakokalipa kwa shida. Kwa maana nyingine anasema watu wanaendesha
> magari kwenda mjini kwa ufahari, la hasha adha za daladala ndo zinasukuma,
> wengine ni wafanyabiashara hubeba mauzo. labda angeshauri makampuni kama
> NSSF na PPF waache kujenga business complex katikati ya mji. maeneo ya
> mlimani city na mawasiliano house hayapo azikiwe mbona yanafanya biashara
> vizuri tu.
>
>
> 2. Ziachwe njia za watembea kwa miguu
> Sidhani kama unaweza egesha gari yono watalifunga mnyororo na kuliburuza.
> hata hivyo hakuna mtu anaweza tembea kwa miguu kutoka mwenge hadi posta kama
> tukiondoa haya magari anayozungumzia bwana mkubwa. Ningeshauri sumatra
> waweke madaraja ya usafiri yenye nauli tofauti mfano economy coaches (nauli
> 300/=) business coaches (nauli 1000/=) executive coaches (nauli
> 5000/=) mkazi wa makongo juu anaweza kuegesha gari mlimani city then
> anapanda bus hadi posta.
>
>
> 3. Kujenga madaraja ya watembea kwa miguu
> Bado viwete na wasukuma toroli hawataweza kuvuka barabara kwa kutumia hayo
> madaraja kama ya manzese, labda wakati waupanuzi wa barabara tufikirie
> kujenga subways ambazo hata viwete na wasukuma toroli na guta watatumia
> kuvuka barabara. Tuangalie uwezekano wa Tanroad kushirikiana na sekta
> binafsi kujenga parking yards, mfano mtu anaweza egesha gari mbezi mwisho
> akapanda basi hadi kariakoo au posta, jioni akalipitia kwenda nyumbani.
>
>
>
> --
>
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
--
=RSM=
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment