Wasichana wanaweza wakaonekana warembo hata kama watavaa nguo ya kusitiri mwili kwa mishono ya kisasa. Waache wakucheke 'ushamba' lakini utakapokuwa sexy na kupata mimba hutomaliza masomo, utapata ukimwi-watakucheka tena, watakunyanyapaa kipi bora? Uvaaji mwingine unaweza kumpa mtu hisia kuwe wewe u rahisi wakakutendea uovu au kukuonea kumbe upo na nidhamu. Ndicho kinachowaponza vijana wetu wakienda ulaya na kumuona msichana bar muuza pombe na kumpika mkono takoni (akidhania mambo sawa na bongoland)akajikuta anaitiwa polisi. Kumbe sio kila mtu Ulaya auzae pombe bar ni malaya. wengine ni university students wenye nidhamu yao wanaganga njaa kupata hela ya ada au kujikimu.
Siku hizi TZ vijana (wa kiume)hadi vyuo vya juu wanavaa suruali (sio tu hizo sare za shule)ikiwa imeshushwa chini mkanda kati ya matako hadi anashindwa wengine wanashindwa kutembea vizuri. Bado hao sharobaro sijui mitaani mavazi yao. Mtu anapata taabu kutembea kashusha dengrizi tabu ya nini-f'ashion has no weather and culture!? Balaa. Wadada pia, kuvaa vimini mnavyosema lakini pia kutunisha (ashakum) matiti yanafurisha kupandisha juu anaingia darasani (Tazama kiambata) au anapita katika kadamnasi au anaingia kanisani.
Mzazi anakwenda nyumba ya Mungu (kanisani) na msichana mkubwa kiasi kavaa kiajabu. kinyume cha maadili. Imefikia baadhi ya makanisa kuweka ulinzi wa wanajumuia wenye zamu kumrudisha mlangoni asiingie. Hasa wasichana na wamama hurudishwa mara nyingi.Jimama lenye unene na shape isiyowiana anadiriki kuvaa suruali ya kumbana na kishumi zisidiria nje na kakweza matiti juu. Maadili yapo? Bado hao wa kuvaa na kucheza na khanga moja iliyoloweshwa na wasanii wa kuvaa vichupi na kucheza juu ya jukwaa tuonavyo magazetini. Lakini hao wana watoto ambao nao huwaona wazazi waokatika TV, nyumbani na magazetini. Wanajenga kizazi gani. Haya yote yanatokea kitaifa pamoja na kuwepo Balaza la Utamaduni; kamati za maadili na ushauri hata mashuleni. Bado hujaingia vyooni kwa wasomi uone kulivyo wanavyofanya vijana Me na Ke.
Kusema kweli kuna haja ya cultural revolution na mafunzo ya stadi za maisha sio tu kama somo shule za msingi lakini hata vyuo vya elimu ya juu na katika vipindi vya radio na TV ili tujikumbushe maadili ya kiafrika na utaifa. Hiyo JKT inayorudi ijitahidi kurudisha nidhamu ya utaifa na pia ile sheria ya kuvaa uniform ya JKT kwa miezi 6 au mwaka.
Zamani vyuo vya juu vilikuwa na sare-Suti. Sasa tunasema 'Private Life' na demokrasia yake ya watu kuwa huru na mambo binafsi. Lakini tunajiaibisha. Hii inatugharimu.
Uchangudoa na ubakaji pia umeoongeze-tunalindana. Na ndio unakuta vibinti mitaa ya Sinza, kijitonyama etc vimevaa vichupi vipo barabarani vinajiuza. Kwani akivaa vizuri kawaida akisimama katika kona yake inayojulikana ya mauzo hatoonekana? TZ inatia huruma. Bado hao ombaomba waliojaa mji mzima wa DSM na Idara ya ustawi wa Jamii na Serikali za Mitaa husika zipo intensive care!! Wasichana wanaweza wakaonekana warembo hata kama watavaa nguo ya kusitiri mwili kwa mishono ya kisasa.
From: moses <mosesgasana@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, 24 July 2012, 18:55
Subject: Re: [wanabidii] Letter from a student in Ruathia girls
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, 24 July 2012, 18:55
Subject: Re: [wanabidii] Letter from a student in Ruathia girls
Matinyi,
Hongera kwa kuitukuza NGUVU YA MWANAMKE! Safi sana
Moses
Sent from my iPhone
Sent from my iPhone
On Jul 24, 2012, at 4:36 PM, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:
Monica, Pia, kwa mwanaume mkware, hata mwanamke akijifunga magunia kumi yeye atahema naye. Lakini hii haiondoi ukweli kwamba msichana wa shule anapaswa kuvaa kiheshima na kujisitiri kwa kadri inavyowezekana. Umbo la mwanamke, na hasa likianikwa kirahisirahisi tu, linaweza kumtia kichaa hata mwanaume muungwana ingawa atabaki anakufa na tai shingoni - hasa kwenye jamii ambayo wanawake hawajianiki hovyo hovyo kumfanya mwanaume astuke anapoona ambacho hakukitarajia, mathalani upaja mdogo unaochomoza. Hatuwezi kupingana na asili. Asante kwa ushauri wako.From: moninaike@hotmail.com To: wanabidii@googlegroups.com Subject: RE: [wanabidii] Letter from a student in Ruathia girls Date: Tue, 24 Jul 2012 13:30:28 +0000Unajua tatizo ni nini LR. wanafunzi wanachukia kwa kuambiwa wasivae vimini shuleni. Wanajitetea wanataka kupata hewa na kulook sex. Just imagine mwalimu mwanume anafundisha halafu nusu ya wanafunzi wake wa kike wametinga vimin atafundisha kweli? Tunachojadili hapa ni kuunga mkono headmaster aliyekataa vimini school kwasababu nadhani alishaona madhara yake. So what he is tying to do is to protect those students also the teachers cause wanakuwa tempted na vivazi hivyo. Tuwafunze binti zetu maadili mbona wakivaa sketi za kawaida wanapendeza tuu.From: rugambwa@hotmail.com To: wanabidii@googlegroups.com Subject: RE: [wanabidii] Letter from a student in Ruathia girls Date: Tue, 24 Jul 2012 13:18:43 +0000Monica na Pius, Mjadala huu ni mpana, na inawezekana wote tunazungumza kitu kile kile kwa muktadha tofauti. Kwahiyo kama watu wako kama fisi na mbuzi hapa tuna maanisha wanaume, ndio dawa hiyo? Those are just social evils which we all need to condem as a society, sio kusema mavazi fulani ndo yanafaa. I think, we should speak against those people who Pius( mafisi na washenzi) is referring to not just one aspect of dress. Na wale wanaobaka watoto wa miaka 4, sasa watoto tuwafanyeje? Hili la mavazi linatatua tatizo dogo sana, tatizo kubwa ni sisi wenyewe hasa hao wanaume wenye tabia kama za mbuzi za kuona paja la binti ukataka kumbaka. Why? haya yataisha tu huku kwetu Afrika, muda si mrefu, mambo ya kuishi kama wanyama wa porini. Hata Kuku anatongoza, hambaki kifaranga, iwewe sisi? Tuijadili kwa mapana yake, tutibu root cause sio ka sehemu ka tatizo, LRFrom: moninaike@hotmail.com To: wanabidii@googlegroups.com Subject: RE: [wanabidii] Letter from a student in Ruathia girls Date: Tue, 24 Jul 2012 12:17:37 +0000Waambie Laurean, Kuna watu wanapenda kusema mradi wana midomo, kweli kumsapoti mwanafunzi kuvaa kimin kwa kivuli cha mandeleo ni upotoshaji wa jamii na matokeo yake kila mtu anayajua. Ni jukumu la kila mwenye akili timamu na busara kuhakikisha tunawalinda hawa binti zetu kwa gharama yeyote kwani kuna mafisi wanao wawinda kwa tamaa ya kuona maungo yao.Date: Tue, 24 Jul 2012 13:00:08 +0100 From: malagila01@yahoo.co.uk Subject: RE: [wanabidii] Letter from a student in Ruathia girls To: wanabidii@googlegroups.com CC: tomlaiser@yahoo.com
Laurean,
Mungu kamuumba mwanamke kwa maumbile ambayo yana mvuto kwa mwanaume. Yapo maeneo ya mwili ambayo yakiwekwa wazi wanavuta na kutia ushawishi wa ngono. Huu ni ukweli utakaobaki umesimama whether you are objective or not. Kupuuzia haya kwa jina la maendeleo, watu wanavaa nguo za aibu na kubakiza maeneo yao ya mwili wazi halafu unataka watu wawe objective! Kwa lipi!
Wewe, subiri ukae na watoto wako uwaeleze hayo. Waambie wavae hata nguo za ndani watembee hivyo na usubiri watazamaji wawe objective. Inawezekana kabisa wasibakwe, lakini watakuwa wanazongwa na watu/wanaume kana kwamba ni mzoga unaofuatwa na nzi. Why??
Kama wewe ni mzazi, simamia maadili mema. Kila mzazi anawajibika kwa mtoto wake sio kwa chakula na vingine bali kwa kujali maadili mema. Huu ni wajibu alioukabidhi Mungu kwa wazazi wote na watawajibika kwa hilo hapa na baadaye.
Mwenye sikio na asikie
Martin Pius
P. O. Box 561, BABATI
Manyara
Tanzania
Mob: +255 78 447 4940 / +255 71 3474940
Email:malagila01@yahoo.co.uk
--- On Tue, 24/7/12, Laurean Rugambwa B. <rugambwa@hotmail.com> wrote:
0 comments:
Post a Comment