Saturday, 7 July 2012

Re: [wanabidii] Hongera Hasheem Thabeet kwa kingia mkataba wa miaka 2 na Oklahoma City

Ila aongeze bidii..taarifa za ndani ni kwamba hafanyi vizuri sana NBA,na hafahamiki kivile kama tunavyodhani hata huko Marekani kwenyewe...wengi ya wapenda kikapu huko hawamfahamu...na Magesa anafahamu hilo,he is struggling to stay NBA..Watanzania ni wanafiki mara nyingi..kama mtu hafanyi vizuri tuseme ukweli..mnakumbukwa aliazimwa na timu nyingine hapo nyuma..kwa ufupi ni ufahari ameingia NBA ila bado hajatupa ule ujiko wa wengine kama Hakeem Olajowoni,Manut Bol,Mutombo Dikembe nk.

Watanzania tuwe watu wa kufanya mambo zaidi ya "kawaida" /MEDIOCRE ...NA hizi sifa za kijinga tuziache..Thabit anahitaji kufanya juhudi zaidi...watu wengi hata Wapenda kikapu marekani hawamjui...nilijitia  kusema natoka Tanzanai..unamjua Hashim Thabit anacheza NBA..hii ilikuwa New York..kila mtu akawa anamwangalia mwenzake...hawamjui kivile...tetesi ni mvivu..ukweli unasaidia...kwa hiyo Magesa naomba kama una ufafanuzi kwa hilo utusadie..Tanzania  isiwe ni nchi ya MEDIOCRITY...

2012/7/7 Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>

Hakuna jambo zuri la kujisikia furaha unapokutana na mtu akakuuliza unatokea wapi we unajibu tu nchi anayotokea Hasheem Thabeet! thats simple ilikuwa inatuhuzunisha kuona hafanyi vizuri but kule alikopelekwa ni vijana wenzie i hope he will step u for challenges and makes it Mungu ibariki africa, tanzania.....(kipandekingine kimenitoka) dumisha uhuru na umoja .... kwingine kote wimbo huu ni mzuri tuuuuuuuuuuu

2012/7/7 richard bahati <ribahati@gmail.com>
Mara moja moja tunapata furaha kuona kwamba jambo zuri linaweza kutokea hata Tanzania?
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Hasheem Thabeet

2012/7/7 Phares Magesa <magesa@hotmail.com>

Hasheem Thabeet, Mtanzania anayecheza mpira wa kikapu Marekani amesaini mkataba wa miaka 2 na timu ya Oklahoma City Thunder..!!!

Watanzania ni wakati sasa wa kujivunia mafanikio ya baadhi ya watanzania wanaofanya vizuri katika viwango vya kidunia, katika historia ya michezo tangu tupate uhuru ni Hasheem Thabeet pekee ndio ameweza kufanikiwa na kucheza ligi ya juu kabisa duniani katika michezo.

Wako watanzania wengi wamefanikiwa katika michezo mbali mbali na kufanikiwa kucheza katika ligi za mchezo mbali mbali  na katika nchi mbali mbali ila kila mchezo una ligi zake ambazo ni za kiwango cha juu  juu kabisa ni yeye pekee ndio amweza kufanya hivyo kwa kufanikiwa kucheza mfulilizo. Hasheem amecheza timuza Memphis na baadae kucheza Houston Rocket na mwshoni mwa msimu uliopita alicheza Portland Trail Blazers. Katika timu ya Blazers alicheza michezo yote 16 liyokuwa imebaki kabla ya msimu kumalizika.

Hasheem kwa sasa ndio mwafrika mwenye kiwango cha juu kabisa miongoni mwa waafrika wanaocheza kikapu Marekani na ni mchezaji pekee anayecheza huko toka ukanda wa Afrika , Mashariki, Kati na Kusini. Hasheem ni mchezaji wa Afrika ambaye ameingia NBA akiwa na kiwango cha juu kabisa katika historia ya mchezo huo, yaani No. 2 NBA Draft ya 2009.

Kwa Hasheem kuchukuliwa na timu kama Oklahoma City ambao ni mabingwa wa kanda ya magharibi ya NBA na mwaka huu walicheza fainali ya ubingwa wa NBA na kushindwa na Miami Heat, inaonyesha jinsi ambavyo bado mchezaji huyo anathaminiwa na bado uwezo mkubwa wa kuisaidia timu kubwa kama OKC ili iweze kufikia malengo yake.

Hivyo basi kwetu sisi Tanzania tunampongeza na kujivunia mafanikio hayo. Hasheem pia amekuwa ni mchezaji pekee wa kiwango cha juu ambaye amekuwa akirudisha fadhila nyumbani na kila anapo pata mapumziko huwa anarudi nyumbani kuja kushirikiana na watanzania wenzake ili kuwainua na kuibua vipaji.

Kwa niaba ya shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania, natoa pongezi nyingi kwa Hasheem na tunamtakia kila heri na tumuombee kwa Mungu ili afanikiwe zaidi katika kikapu.

Mungu Mbariki Hasheem, Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

Phares Magesa
Makamu wa Rais
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF)

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment